Kuna wakati unapaswa kujipa nafasi ya kutoka kwenye mazingira ya mjini, ukaenda kijijini na kuona maisha wanavyoishi kwa uhalisia wake. Utajifunza mengi sana namna watu wanavyoishi, wanavyothamini vitu vidogo, jinsi tabia zao zinavyotofautiana kabisa na maisha ya haraka ya mjini.