๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐, ๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐! ๐ฐ
Viwanja vya Mwembetogwa, Iringa Mjini, vilifurika maelfu ya wananchi, wanachama na wapenzi wa CCM waliojitokeza kumpokea na kusikiliza mawasilisho ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi.
Shangwe, nderemo na vifijo vilitawala kila kona, vikidhihirisha upendo mkubwa wa wana Iringa kwa mtoto wao pamoja na imani yao kwa CCM kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utatuzi wa changamoto za wananchi.
Hakika, mcheza kwao hutunzwa; wana Iringa wamethibitisha kuwa CCM ndiyo chaguo lao na namba moja daima.
Tembelea: https://t.co/XFsl2QgHBH
__________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#MtumishiWaWote
#Iringa
๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐, ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Iringa Mjini, ameweka wazi baadhi ya kauli za zamani za Peter Msigwa na kuzieleza kuwa ni ushahidi unaoonesha mabadiliko ya misimamo yenye lengo la kuwapotosha wananchi kwa manufaa ya kisiasa.
Kihongosi amesema viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa waaminifu kwa wananchi na kusimamia wanachokiamini wakati wote, badala ya kubadili misimamo kulingana na mazingira ya kisiasa.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
______________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#MtumishiWaWote
#CCMIpoKazini
#Iringa
๐๐๐๐๐๐๐๐๐: ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐; ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐ ๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amesema CCM si mahali pa wanasiasa wanaotafuta vyeo au kuipa Chama masharti, bali ni taasisi inayofuata Katiba, kanuni na taratibu zake katika kupata viongozi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Mwembetogwa mkoani Iringa, Kihongosi amesema kujiunga na CCM kunapaswa kuongozwa na dhamira ya kuwatumikia wananchi na kujenga Chama, si kutanguliza matarajio ya kupata nafasi za uongozi.
Amesisitiza kuwa uongozi ndani ya CCM hupatikana kwa kuzingatia sifa, uwezo, uzoefu na mchango wa mwanachama kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
"CCM haipewi masharti. Uongozi ndani ya Chama hupatikana kwa sifa na taratibu, si kwa matarajio ya vyeo," amesema Kihongosi.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
_________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#MtumishiWaWote
#Iringa
UVCC(M)GEITA ๐ฐ
KIKAO CHA BARAZA LA UVCCM MKOA WA GEITA
19 Juni, 2026
Wajumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Geita wakiongozwa na Ndugu Manjale Magambo kwa kauli Moja wamthibitisha Ndugu Meshack Joseph Kiyozo kuwa Katibu Hamasa na Chipukizi UVCCM Mkoa wa Geita
UVCCM (M) GEITA
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita Ndugu Manjale Magambo akiongoza Kikao cha Kawaida Cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita Mapema leo katika Ukumbi wa Mikutano wa CCM Mkoa wa Geita
๐ 19 Juni, 2026
๐CCM Magogo
#KulindaNaKujengaUjamaa๐ฐ
๐๐๐ ๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐: ๐๐๐๐๐, ๐๐๐๐๐, ๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐!
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, akiungana na wananchi wa Kilolo kuimba wimbo wa dini katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, akisisitiza kuwa amani, umoja na mshikamano wa Watanzania ndiyo msingi wa maendeleo endelevu na ustawi wa Taifa.
CCM inaendelea kuwa Full Package ya kuhubiri na kusimamia amani, kuimarisha umoja wa wananchi na kutekeleza maendeleo kwa vitendo kwa manufaa ya Watanzania wote.
๐ Leo ziara ya Mwenezi wa CCM Taifa inaendelea Iringa Mjini katika Viwanja vya Mwembetogwa.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
_____________
#KaziNaUtuTunasongaMbele #MtumishiWaWote
#Iringa
๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amesema kukamilika kwa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kinachojengwa Wilaya ya Kilolo kutafungua fursa kubwa za ajira na kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi.
Kihongosi ameyasema hayo leo, Juni 19, 2026, alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho katika Kijiji cha Luhindo, Kata ya Mtitu, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, amesema chuo hicho kitawajengea vijana ujuzi wa kujiajiri na kuajirika katika sekta mbalimbali za uzalishaji.
"Kukamilika kwa mradi huu kutaleta fursa kubwa kwa vijana wetu kupata mafunzo yatakayowasaidia katika masuala ya ajira, huku Halmashauri ikinufaika na wataalamu watakaozalishwa kupitia mafunzo hayo," amesema Kihongosi.
Ameongeza kuwa uwepo wa karakana tatu utasaidia utoaji wa mafunzo ya vitendo yatakayowawezesha vijana kujipatia kipato na kuchangia ukuaji wa uchumi wa familia zao na Taifa kwa ujumla.
Aidha, amesema CCM na Serikali vitaendelea kushirikiana kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati ili wananchi wa Kilolo wanufaike kikamilifu na uwekezaji huo.
Awali, Mdhibiti Ubora wa Shule, Altos Kinunda, amesema chuo hicho kinatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.6. Hadi sasa, kimepokea shilingi milioni 777.4, ambapo shilingi milioni 573.7 zimetumika na shilingi milioni 203.7 zimebaki kwa ajili ya kuendeleza ujenzi.
Amesema awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa majengo tisa, ikiwemo jengo la utawala, madarasa, karakana, nyumba ya mtumishi, jengo la mlinzi na jengo la umeme. Ujenzi umefikia asilimia 76 na ukikamilika chuo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 240.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
_____________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#VETAKilolo
Nyota wa mpira wa miguu "Michael Olise" nyota ambaye anaichezea timu ya taifa ya Ufaransa, kama kawaida yake kabla ya Mechi (France vs Senegal) alikagua Uwanja (Pitch Inspection) ambapo France waliibuka washindi wa mchezo huo Kwa 3 - 1 (France 3 - 1 Senegal)
Hii tabia ya Michael Olise imekuwa ikiwavutia watu wengi sana mtandaoni na mashabiki zake Kwa ujumla.
Unafikiri Kuna siku Olise amewahi kusahau kufanya hii tabia yake? Wengi wanasema hufanya hivi ili kujua ni kiatu gani anavaa ๐