Chama Cha Mapinduzi Tanzania Ruling Party Youth Wing, Senate Member @uvccm_tz DSM, MCC/I @UVCCMS & Fmr Secretary General @uvccm_open | Educator & Entrepreneur.
Wananchi wameaswa kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye Biashara ya Kaboni kwa kuanzisha miradi mbalimbali kulingana na jeografia ya eneo husika na kuachana na dhana ya upandaji miti na misitu ndio inakopatikana Biashara ya Kaboni.
Hayo ameyasemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi wakati akifungua Kikao cha Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026 akieleza kuwa kuna fursa katika program hiyo ikiwemo Biashara ya Kaboni.
Amesema fursa ya Biashara ya Kaboni haipo pekee kwenye upandaji miti kama ambavyo wengi wanadhani, bali katika Nishati Safi ya Kupikia, Miradi ya Taka, Usafishaji wa Miji, Taka Nngumu na taka zingine zote zinaweza kuwa fursa katika Biashara hiyo.
Baada ya Serikali kuzindua Dira 2050 Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa Programu ya Mageuzi ya Kukijanisha Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2026 hadi 2030, inayolenga kuchagiza matokeo makubwa ya kurejesha uoto wa asili, kuimarisha ustawi wa mifumo ikolojia na kuongeza mchango wa rasilimali katika Pato la Taifa, sambamba na kuchangia katika kufikia malengo ya Dira 2050.
“Ili tuwe na mchango mkubwa kwenye Dira 2050 tunatakiwa kuwa na mpango maalum na hatutakuwa tukiangali katika upandaji miti pekee bali tutaangali pia kwenye Nishati safi ya Kupikia ili kuwafikia wananchi.
Ameongeza kuwa kutokana na heshima ambayo mazingira yamepewa na kuwekwa kwenye Dira 2050 ni vyema sekta ya mazingira nayo ibadilike ili mchango wake uonekane kwa kuyasimamia mazingira vizuri.
“Awali, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda alisema Programu hii inalenga kuchagiza matokeo makubwa na ya haraka katika kurejesha uoto wa asili, ustawi wa mifumo ikolojia na kuimarika kwa huduma za kiikolojia ambazo zinachangia katika sekta mbalimbali za uzalishaji nchini.”
Ameongeza kuwa Maeneo ya kimkakati ya utekelezaji wa Programu ya Mageuzi ya kukijanisha Tanzania ni Upandaji Miti katika Mikoa ya Tabora, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Geita, Singida, Simiyu, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Rukwa na Zanzibar.
Nchi yetu imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa kwanza barani Afrika wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Shirikisho la Jumuiya ya Madaktari wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (WFNS) ambao leo nimeufungua jijini Dar es Salaam. Uamuzi huu unadhihirisha imani kubwa katika maendeleo yetu na utayari wetu katika kuimarisha zaidi huduma za afya, hususan huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.
Matokeo ya kazi kubwa tuliyofanya katika miaka mitano iliyopita katika huduma za afya za kibingwa na ubingwa bobezi yanaonekana ambapo;-
1. Hospitali zinazofanya upasuaji wa kibingwa wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu zimeongezeka kutoka 2 hadi 7.
2. Madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wameongezeka kutoka 12 hadi 37.
3. Tumeongeza kwa kiasi kikubwa vifaa muhimu kama MRI, CT-Scan na X-ray.
Uwekezaji huu umeifanya Tanzania kuwa moja ya nchi chache Afrika zenye uwezo mkubwa wa kufanya upasuaji huo, na sasa inahudumia wagonjwa kutoka nje ya nchi.
Ninashukuru Chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Tanzania kwa tuzo mliyonipa, hakika, hii ni heshima yetu sote. Serikali yetu itaendelea kushirikiana na taasisi za kikanda na kimataifa kuimarisha huduma za afya kwa kuzifanya kuwa bora, nafuu na za uhakika ili kuokoa maisha ya wananchi na kurejesha tumaini kwa jamii.
Wataalamu 1,483 Kunufaika na Mpango wa Samia wa Utaalamu wa Juu Sekta ya Afya
Kupitia Mpango wa Samia Health Super-Specialization Program, jumla ya wataalamu 1,483 wanafadhiliwa kusomea fani za ubingwa na ubingwa bobezi ndani na nje ya nchi.
Nauungana na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwatakia Waislamu na Watanzania wote Sikukuu njema ya Eid el-Fitri.
Tuna wajibu wa kulinda na kuendeleza tunu njema tulizozijenga katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani; tunu za upendo, mshikamano, nidhamu na kujali wengine, ili kuimarisha umoja wa kitaifa na kuijenga Tanzania yenye maadili imara, haki na usawa kwa wote.
Katika kusherehekea sikukuu hii, tuendelee kudumisha amani, kulinda utulivu wa nchi yetu na kuenzi mshikamano wa Watanzania, tukitambua kuwa umoja wetu ni nguvu yetu na msingi mkuu wa maendeleo endelevu ya Taifa letu.
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mapema leo jijini Arusha nimemkaribisha na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ghana, Mheshimiwa John Dramani Mahama ambapo tumejadili juu ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika mageuzi ya kiuchumi, kuongeza thamani ya rasilimali zetu, ajira kwa vijana na maendeleo ya uchumi wa kidijitali.
Dhamira ya waasisi wa mataifa yetu haya mawili ilikuwa ni kuiunganisha Afrika, nasi kwa pamoja tumepongeza kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja za ATCL kati ya Dar es Salaam na Accra (Ghana) ambazo zitarahisisha mwingiliano wa watu, kukuza biashara na utalii.
Tanzania na Ghana zitaendelea kushirikiana katika usimamizi wa rasilimali ili kujenga uchumi shindani na jumuishi, unaolenga kufungua fursa zaidi za biashara, uwekezaji na ajira kwa wananchi wetu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Ghana Mhe. John Dramani Mahama mara baada ya kuwasili katika Ikulu Ndogo ya Arusha tarehe 02 Machi, 2025. Rais wa Ghana Mhe. Mahama amewasili Mkoani Arusha kwa ajili ya Ziara ya Kikazi, ambapo anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mwaka mpya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, na Sherehe za kumbukizi ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo mwaka 2006.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwamiminia uji wanafunzi wa Assalaf Islamic Seminary kutoka Ummu Aisha Orphanage Centre, walioshiriki kwenye Futari aliyowaandalia pamoja na Makundi mengine ya jamii, Ikulu Ndogo ya Arusha tarehe 01 Machi, 2026.
🔴U H A M I S H O
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho na kuwapangia vituo mabalozi, Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka , mabalozi waliopangiwa vituo vipya ni :-
▪️Balozi Togolani Elvis Mavura amepangiwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa , New York
From H.E. @KagutaMuseveni ’s message, one thing is clear: the struggle now is against poverty.
As young people, wealth creation is our mission.
PDM,Emyooga, Ghetto & Boda funds are opportunities, not politics.
Let us organize, and pull each other into the money economy.
#Youth
🔹 Miundombinu – Rais Samia kukuza Ujenzi na uboreshaji wa barabara, reli (ikiwemo SGR), viwanja vya ndege na bandari ili kurahisisha usafirishaji na biashara.
DKT SAMIA KUZINDUA JIWE LA MSINGI LA UJENZI MATENKI 15 YA MAFUTA ΚΑΤΙΚΑ BANDARI YA DSM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa matenki 15 ya kuhifadhia mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam leo Machi 3, 2026. Mradi huu ni sehemu ya mpango mkubwa wa Serikali wa kupanua na kuboresha bandari hiyo ili kuimarisha nafasi yake kama lango kuu la biashara nchini na katika ukanda wa Bahari ya Hindi. Pamoja na ujenzi wa matenki hayo, serikali inaendelea na ujenzi wa gati namba moja lenye urefu wa mita 500 na uwezo wa kupokea meli mbili kwa wakati mmoja kila moja ikiwa na uwezo wa kubeba takriban tani 50,000. Maboresho hayo yanalenga kuongeza uwezo wa bandari kuhudumia shehena kubwa zaidi na kuifanya kuwa miongoni mwa bandari zenye ushindani mkubwa katika ukanda huu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiondoka Kiwanja che Ndege cha Kimataifa cha Bole, Addis Ababa, nchini Ethiopia kurejea nchini Tanzania, leo tarehe 15 Februari, 2026.
Rais Dkt. Samia alikuwemo nchini humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo pamoja na mambo mengine alishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika tarehe 14 na 15 Februari, 2026.
It has been a singular honour and a privilege to meet with H.E. Joaquim Chissano retired President of Mozambique, a highly respected statesman, in Maputo this week.
His perspective on the the liberation of Southern Africa and the situation post independence has been enlightening.