Kama umekua unatamani kujifunza hizi high income skills
→Media buying & automation
→Affiliate marketing
→CPA marketing
Wiki hii tutakua na class kubwa sana na kama unatamani kujifunza basi jiunge kwenye group hapa bado mapema 👇
https://t.co/QtJL11IByP
📌
USIPUUZE SAUTI YAKO YA NDANI KAMWE
Kuna vita kubwa ndani yako kila siku.
Ni vita kati ya hadithi unayojiambia ndani ya nafsi yako na hali halisi.
STEVEN BARTLETT katika kitabu chake cha
The Diary of a CEO
anasema kuwa.
"The Most powerful force in your life is the story you tell yourself. "
Akiwa na maana ya - Nguvu kubwa zaidi katika maisha yako ni hadithi unayojiambia mwenyewe.
Ukijiona dhaifu utaishi kama mdhaifu.
Ila ukijiona mshindi utaanza kutenda kama mshindi hata kabla ya ushindi kuonekana.
Chochote ambacho akili inaweza kukifikiri na kukiamini kwa uthabiti inaweza kukitimiza.
Watu wenye mtazamo chanya wana uwezekano mkubwa zaidi wa kufanikiwa kuliko wanaoamini kwenye vipaji vya kuzaliwa navyo tu.
Moja ya makosa makubwa tunayoyafanya bila kujua ni kusikiliza sauti za nje kuliko sauti ya ndani.
Usiache kelele za maoni ya watu zizime sauti yako ya ndani
Maisha yanakupa sababu nyingi sana za kuacha ndoto zako ziishie njiani,Usiruhusu hilo kutokea.
Kumbuka 📌
Ulizaliwa ukiwa ORIGINAL usikubali kuondoka duniani ukiwa COPY.
Pambania ndoto yako.
Usiipuuze sauti yako ya ndani.
Simama nayo,iamini na iishi kila siku.
#DailyBookWisdom
#MaarifaYaKilaSiku
#FordTactics #TimelessWords
Mungu anakupenda sana hata ukiwa kwenye dhambi ila upendo hauondoi dhambi. Kazi ya upendo ni kukusogeza kwa Mungu. Uone uzuri wa Mungu. Uone neema ya Mungu. Uone msaada na nguvu ya Mungu ya kukuondoa kwenye dhambi. Siyo kukutia moyo uendelee na dhambi. Njoo kwa Yesu. Tubu.
MWANAUME.
USIRUHUSU KAMWE MWANAMKE KUTUMIA MTOTO WENU KAMA FIMBO
Mwanamke Akiamua kumchukua mtoto wako na kukuondoa kwenye maisha yako, muache tu.
Wanawake wengi hutumia mtoto kama silaha dhidi ya mwanaume wakijua kuwa mwanaume anajali sana kuhusu mtoto atataka kuwa karibu na mtoto wake au kumlea.
Baada ya kuachana, kuna aina nne za wanaume:
1. Wanaume wanaotuma pesa lakini hawapo karibu na mtoto:
Wanawake wanapenda hawa wanaume kwa sababu wanaweza kuchukua pesa zao na bado wanamwambia mtoto kuwa baba hajali na ni mbaya.
2. Wanaume wanaotuma pesa na pia wana ukaribu na mtoto:
Wanawake hawawapendi sana hawa wanaume kwa sababu huhisi kama wanashindana nao kupata upendo wa mtoto.
3. Wanaume wasiotoa pesa wala kuwa karibu na mtoto:
Wanawake huwachukia hawa kwa sababu hawana faida yoyote kwao.
4. Wanaume walio karibu na mtoto lakini hawatoi pesa:
Wanawake huwachukia hawa zaidi kwa sababu wanahisi mwanaume yuko karibu tu ili kuiba upendo wa mtoto.
Ukweli ni kua,
Mwanamke either hajaolewa, ameolewa au kaachika hutaka mtoto awe upande wao pekee.
Wana amini wanastahili hilo baada ya kupitia uchungu wa mimba, kujifungua na kulea. Hawazingatii mchango wa mwanaume katika kutoa mahitaji.
Hivyo ndivyo walivyo wabinafsi.
Ndio maana katika nyumba nyingi, utakuta mwanamke anajifanya kama ndiye anayehudumia kila kitu, hasa baba akiwa hayupo mara nyingi.
Sasa fikiria mwanamke wa aina hii baada ya kuachana — atataka pesa zako lakini hataki uwe karibu na mtoto. Atataka aonekane anamzingatia mtoto pekeake lakini bado pesa achukue kwako.
Mwanamke aliyeachika hamthamini baba anayeshiriki kikamilifu katika malezi ya mtoto kwa sababu hatakuwa na la kumtuhumu nalo.
Ndiyo maana kama mwanaume unapaswa kuwa karibu na mtoto wako kama unamhudumia. Ingawa wanaume wengi hukaa mbali kwa sababu hawawezi kutoa mahitaji.
Baada ya kuachana, kitu ambacho wanawake wengi wanataka ni mwanaume anayetoa pesa lakini hayupo karibu.
Wanataka awasaidie kumlea mtoto lakini asiwe na haki yoyote.
Ndiyo maana utaona wakiomba hela za matunzo ya mtoto huku wakimficha mtoto asimuone baba yake.
Kama mwanaume, una mamilioni ya mbegu kwa sababu. Tafuta mwanamke mwingine na uzae naye. Usimruhusu mwanamke akuangamize kiakili kwa sababu ya mtoto aliyemzaa na wewe.
Akiamua kuondoka, mwache akae na uamuzi wake. Mwache amwambie mtoto chochote anachotaka kukuhusu. Mtoto akishakuwa mkubwa ataelewa ukweli — akiamua kufuata upande wa mama yake, mwache naye pia.
Cha muhimu ni kwamba uwe na familia mpya ambayo unaijali na unaikuza ipasavyo.
Maisha ni mafupi sana kujitesa kwa vitu visivyo ndani ya uwezo wako. Ukimruhusu mwanamke kukutesa kupitia mtoto wenu, hutawahi kufurahia maisha.
Maisha ni safari ya mara moja; kumbuka, ukifa leo, mama wa mtoto na mtoto mwenyewe wataendelea na maisha yao. Hata mtoto mliyemlea pamoja, akikua atawaacha nyote na kuishi maisha yake.
Usiruhusu mwanamke kutumia mtoto kama silaha dhidi yako. Una mambo mengi zaidi ya kufanya katika maisha.
"Kukusamehe ni hiyari yake, kuomba msamaha ni wajibu wako. Kuishi na deni la samahani kwa uliyemkosea ni mzigo mzito. Usikubali kuubeba ukuelemee. Wewe tua mzigo wako, mtwishe mzigo wake." ~Togolani Mavura.
"Umbea na majungu huzaliwa watu wanapokuwa na muda mwingi wa kuongea kuliko sababu iliyowakutanisha. Kuwa mwepesi kuaga unapomaliza yaliyokukutanisha ama yaliyokupeleka. Utaepushwa na mengi." ~Togolani Mavura.
"Watoto waliofeli maishani ni mizigo ya mama zao wakati wale waliofanikiwa ni fahari ya baba zao. Ni nadra sana mama kumkatia tamaa mwanae. Ukikatiwa tamaa na mama yako akakulaani ujue umekwisha. Hata Mwenyezi Mungu hatakusamehe." ~Togolani Mavura.