USIKU WA BABERI NA SIRI ZA UTAJIRI ZINAZONG'AA GIZANI
โWakati mji wa Babeli ulipolala, sauti za biashara zilitulia, lakini HEKIMA ya matajiri wake ilibaki iking'aa kama nyota zing'aazo usiku wenye giza totoro.
โIshi ukielewa kuwa kanuni za kifedha hazilali.
Kitabu cha "THE RICHEST MAN IN THE BABYLON by George S."
Bwana George anatufundisha kuwa madeni na umaskini ni kama giza nene la usiku, lakini tunaweza kulishinda giza hili kwa kuwasha taa za HEKIMA ambazo zinaweza kuona njia ya kuelekea kwenye uhuru wenye MWANGA wa Kifedha.
โkuna vitu vya kuvitafakari usiku wa leo ili kesho yako iwe ya mwangaza
โโKwanza, Weka Akiba na Chunga Hazina Yako Isipotee.
Usiwekeze pesa zako kwenye fursa zinazoonekana kwa haraka au kwa watu wasio na uzoefu tambua ulichowekeza ni pesa na inatakiwa kuzaa na watoto wake wazae piah . Anza kuweka Akiba Leo na uilinde hazina yako.
Usipofanya hivyo ni sawa na kuacha mlango wako wazi usiku, ambayo itakufanya upoteze kila kitu. Fanya utafiti na tafuta ushauri kwa waliofanikiwa.
โโPili, Fanya Akiba Yako Iongezeke na Hazina yako ikufanyie kazi.
Kuweka akiba ni mwanzo wa kuona mwanga tu. Pesa zako zinatakiwa kukufanyia kazi. Kama vile mwezi unavyoendelea kuzunguka dunia hata tukiwa tumelala, uwekezaji wako unapaswa kuzalisha faida masaa 24.
Pesa isiyofanya kazi ni pesa iliyokufa.๐
โTafakari kichwani mwako Je, Pesa yangu inanifanyia kazi nikiwa nimelala, au mimi tu ndiye ninayeifanyia kazi nikiwa macho?
โโTatu, Panga Matumizi Yako Kabla Giza Halijaingia na Dhibiti Matumizi Yako.
Matamanio yetu ni mengi kuliko kipato chetu tunachoingiza kwenye utafitaji wetu, hivyo Bila bajeti matumizi yako yataongezeka ili kulingana na mapato yako. Panga mapema nini ni muhimu needs na nini ni anasa wants. Orodha yako ya bajeti ni kama tochiโinakuonyesha pa kukanyaga ili usijikwae.
NB. "Usiache giza la umaskini likufunike. Anza leo kwa kuweka akiba ya angalau 10% ya kila unachopata."
MALIZA NA MUNGU ๐๐ฟ
#DailyBookWisdom
โ#TheRichestManInBabylon #HekimaYaKifedha #ElimuYaPesa #Uwekezaji #TafakariYaUsiku #UhuruWaKifedha
Binafsi nipo hapa mjini takribani wiki sasa lakini cha kushangaza bado sioni mwanamke mzuri kumzidi BLESSED TILLAH hapa Dodoma
Acha niendelee kuzunguka huenda nikamuona hata anaye mkaribia tu.
MUNGU AKIKUINUA USIONE
WENGINE NI WAZEMBE, HESHIMU KILA MTU HATUWEZI KUFANIKIWA WOTE KWA SIKU MOJA. ๐
Wakati wako ukifika, shukuru na baki kuwa mnyenyekevu.
Morning Fam๐๐พโโ๏ธ
"Jifunze kuwa msikilizaji mzuri kuliko mzungumzaji mzuri. Unapoongea unarudia tu kile unachokijua tayari, lakini unaposikiliza unapata nafasi ya kujifunza kitu kipya kutoka kwa wengine."
Good Morning Everyone ๐๐๐
Ukiwa huna kitu cha msingi cha kufanya kwenye maisha yako ndio hapo utaanza kuona mapenzi yanakusumbua yani unakuwa unahangaika kwenye masuala ya ndoa na mahusiano.
Utapoteza marafiki wengi katika safari yako ya mafanikio, ndio maana basi lina siti 60, noah ina siti 12, IST ina siti 5 na buggati ina siti 2.
Unapozidi kupanda kuna unaowapunguza na kuna wanaojipunguza. Ila baiskeli haipo kwenye equation ๐
Good morning Hustlers ๐๐พ