Timu ya Walinzi wa Pwani kutoka nchini Marekani mchana huu imeripoti kuisha kwa akiba ya hewa ya oxygen iliyomo kwenye chombo cha chini cha maji (submarine) ambacho kimepotea kwenye eneo ilipotokea ajali ya Titanic.
Walinzi hao walitabiri kuwa usambazaji wa hewa ya oxygen katika chombo hicho kinachoitwa Titan kilichopotea mwanzoni mwa wiki hii, itaisha mchana saa sana nane na dakika nane mchana kwa saa za Afrika Mashariki, kwa sasa tayari kifaa maalum kilichotumwa ndani ya bahari kimefika kwenye sakafu ya bahari na kimeanza kutafuta submarine hiyo.
Taarifa kutoka kwa opereta wa chombo hicho, OceanGate Expeditions imesema submarine hiyo ina uwezo wa kusambaza hewa ya oxygen kwa saa 96 pindi inapokutana na hali ya dharura na tayari saa 96 zimeisha hivyo kuzua hofu na wasiwasi kuhusu uhai wa Watu watano walio ndani ya chombo hicho.
Kampuni ya OceanGate hutoza $250,000 (Tsh Mil 598.7) kwa kila Mtu kwa safari za kuelekea kuitazama meli ya ‘Titanic’ chini ya maji ambapo kikiwa chini ya maji kina uwezo wa kubeba Watu watano na kwa kawaida kina uwezo wa kukaa ndani ya maji na oksijeni ya siku nne, Watu watano waliokuwa ndani ya chombo hicho kilichopotea ni bilionea kutokea Uingereza, Rubani mdogo kutokea Ufaransa, Bilionea kutokea nchini Pakistani akiwa na Mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 19 pamoja na CEO wa OceanGate, kampuni inayoendesha Titan.
#MillardAyoUPDATES
UKISIKIA MAPYA YA DUNIA NDIYO HAYA!
Mmiliki wa huyu ng'ombe hapa alikuwa akisikia mbwa wakibweka kila siku nyakati za usiku ila kila akitoka nje haoni dalili yoyote ya hatari. Na kwa hiyo akaamua kuweka kamera ya CCTV.
Siku fulani, akaamua kukagua kilichorekodiwa 👇🏾
Kwanini wana Arsenal mnahisi nimefurahi taarifa za Rice na Man City ? Mimi mwenyewe sipendi aendw huko bora aje kwenu , akitua City its game over again next season 😀😀
Uongozi wa klabu unaujulisha umma kuwa hatutaendelea kuwa na mlinda mlango, Beno Kakolanya baada ya mkataba wake kumalizika. Taarifa Zaidi Simba App
#WenyeNchi#NguvuMoja
Kuna namna majobless tukifanikiwa kununua hata kijiko tuu,tunatamani mtaa mzima ujue...
Hakuna kitu kinakera kama kununua kiSabufa ama kiTV halafu muda unarudi gheto unakuta majirani hawapo qmmk😂
Tumewapa Arsenal mchezaji mwenye medali ya Ulaya, Supercup na Club bingwa dunia, kidogo na wao wakae karibu na Nyuki ili wale asali, hatupendi Madogo wa London wapate tabu wakati Kaka yao nipo.
Madogo zetu Arsenal wana jezi nzuri ila tumeona tuwape na Wachezaji wazuri.