Nimeshiriki ufunguzi wa semina elekezi ya Viongozi kuhusu umuhimu wa mawasiliano serikalini iliyofunguliwa na Dr. Samia Suluhu Hassan , Rais wa JMT ikulu Tunguu, Zanzibar.
Leo mapema nimetembelea Ubalozi wa Qatar 🇶🇦 hapa Geneva na kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Amir wa Qatar Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani kilichotokea mapema wiki hii. Tanzania 🇹🇿 kupitia Ofisi zetu za Uwakilishi wa Kudumu hapa Geneva, Nimetoa pole kwa familia na wananchi kwa kuondokewa na kiongozi wao. #diplomasiayakimataifa
*TANZANIA NA OMAN ZAIMARISHA USHIRIKIANO USIMAMIZI KUMBUKUMBU NA NYARAKA KIDIJITALI*
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumepokea vifaa vya kisasa vya Chumba cha Kanzi Data, vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na miundombinu iliyoboreshwa ya mtandao kutoka Mamlaka ya Taifa ya Nyaraka na Kumbukumbu ya Sultanate ya Oman.
Katika sherehe hiyo nimeuelezea mchango huu kuwa unalenga kuimarisha usimamizi wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali katika mfumo wa kidijitali, kuongeza usalama wa taarifa za Serikali, kuboresha upatikanaji wa nyaraka kwa wakati, kuimarisha uhifadhi wa muda mrefu wa kumbukumbu muhimu za taifa na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za umma na kwa upande mwengine ni ishara ya kuimarika kwa uhusiano wa kihistoria na ushirikiano imara uliopo kati ya Tanzania na Oman.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali za Tanzania na Oman, akiwemo Balozi wa Sultanate ya Oman nchini Tanzania, Mheshimiwa Said Hilal Al-Shidhani, Balozi Abdallah Kilima kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na viongozi na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka.
Nimeshiriki kilele cha Sherehe ya Miaka 25 ya Chuo Cha Utumishi Wa Umma Tanzania kilochofanyika katika Ukumbi wa JNICC-Dar Es Salaam.
Katika sherehe hizo ambazo zimepambwa na Mwaliko wa Wakuu waliopita wa Chuo hiko an Taasisi ambazo Zimefanya kazi na Chuo hicho katika kipindi cha miaka 25, tumepokea na kutoa vyeti na tuzo za shukrani kwa wite walioshiriki kufikia mafanikio ya Chuo Chetu leo. Katika sherehe hizo pia, nimewakumbusha umuhimu wa chuo hiki kwa Watanzania hasa umuhimu wa kuendelea kufundisha na kukuza utumishi wa Umma Tanzania.
#KaziNaUtu. #KaziInaendelea
Hotuba yangu leo niliposhiriki maadhimisho ya Miaka 60 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam. Maeneo muhimu niliyosisitiza Benki Kuu kufanyia kazi tunapoelekea kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 ni pamoja na:
1. Kuimarisha uwezo wa kung’amua mwelekeo wa taifa kiuchumi.
2. Kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi za kifedha kwa lugha inayoeleweka.
3. Kuhakikisha taasisi za kifedha zinaacha kutegemea dhamana za mikopo ambazo wananchi wengi hawana.
4. Kuhakikisha mafanikio ya mfumo wa fedha yanaenda sambamba na ustawi wa wananchi.
5. Kuimarisha akiba ya fedha za kigeni.
Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Tharman Shanmugaratnam, mimi na Waziri wa Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje, Familia na Maendeleo ya Jamii Jamhuri ya Singapore, Mhe Zhulkarnain Abdul Rahim tumesaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Singapore kuhusu Uendelezaji Ujuzi na Rasilimali Watu inayokusudia kuimarisha mafunzo ya kitaalamu, Ujenzi wa uwezo na kubadilishana uzoefu katika maendeleo ya Rasilimali Watu.
#akaziNaUtu #TunasongaMbele
Nimefungua Mkutano wa Maafisa Tawala na Rasilimali Watu uliofanyika katika ukumbi wa Gen. Mabeyo , Dodoma leo tarehe 1 Juni, 2025.
Mkutano huo ambao umewakutanisha maafisa Tawala na Rasilimali Watu toka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Zile zinazojitegemea na Zile za Serikali ya Mitaa umefanyika ikiwa ni Mkutano wa Mwaka unaokutanisha wataalamu hawa ambapo wanajadili mambo mbalimbali yanayohusu changamoto za fani yao na jinsi ya kukabiliana nazo. Mkutano huu wa Mwaka unaandaliwa na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ni mkutano ambao umuhimu wake unawezesha serikali kukutana na wataalamu ikiwa ni mpango wa kuboresha utumishi wa Umma.
Katika mkutano huo, nimewakumbusha kufuata taratibu na kuwaimarisha mawasiliano baina ya ofisi zako na ofisi ya Rais- Utumishi ili kuimarisha utatuzi wa changamoto huku msiaitizo mkubwa tukisisitiza kuweka kwenye matumizi ya teknolojia za mawasiliano yaani mifumo iliyowekwa
Na kutengenezwa na Serikali kupitia Ofisi yetu ya Rais Utumishi na Utawala Bora. Pia nimetumia nafasi hiyo kumshukuru Mh. Rais kwa kazi kubwa na maelekezo anayoyatoa yanayofanikisha utemdaji kazi wetu na kuimarisha huduma kwa wananchi uku nikigusia mafanikio makubwa ya ujenzi wa mifumo, upandishaji madaraja,ulipwaji wa madeni yanayotokana na mishahara na likizo.
#KaziNa Utu #TunasongaMbele #KaziInaendelea
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete, amefanya kikao na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo iliyofanyika jana Novemba 24, 2025 Waziri Kikwete aliambatana na viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Rais UTUMISHI Mhe. Regina Qwaray na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka.
Katika kikao hicho pamoja na kukagua shughuli zinazofanywa na mamlaka hio, Waziri Kikwete ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha kuwa mamlaka ina wajibu wa kuendeleq kuhakikisha inasimamia na kuendeleza kazi ya kuunganisha serikaki kimtandao na kimifumo huku akiwisitiza uwekezaji katika watumishi wa mamlaka ili kuifanya serikali kuendelea kuwa salama kidigitali.
Ziara inaendelea….
Ahsanteni sana Bunda na Musoma kwa ukarimu, upendo na kujitokeza kwenu kwa wingi leo, nilipoanza mikutano ya kampeni katika Mkoa wa Mara.
Ninawapenda sana. Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumewasili salama Mkoa wa Manyara na kuanza kampeni zetu katika Wilaya ya Hanang. Kila tunapopita tumeendelea kushuhudia ukubwa na kukubalika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wananchi, kutokana na makubwa yaliyofanyika kwao, na yale ambayo tunakusudia kufanya.
Ahsanteni sana wananchi wa Hanang. Imani yenu kwa CCM ni nguvu kwetu na deni ambalo tutalilipa kwa uaminifu, kwa kuendelea kupanga na kutekeleza mipango inayoboresha maisha ya kila mwananchi na kuimarisha zaidi Taifa letu.
Katika mwendelezo wa kampeni za Urais za Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo nimezungumza na wananchi wa Arusha Mjini, kuhusu yale tuliyofanikiwa kwa miaka minne iliyopita, na tuliyopanga kuyatekeleza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Moja ya mafanikio makubwa tuliyopata ni kuimarika maradufu kwa sekta ya utalii, ambayo tumeshuhudia ikibadili maisha ya maelfu ya wananchi, hasa vijana. Nimewapa wananchi ahadi na hakika ya kuitekeleza panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu; kuwa tutaendelea kuwekeza kwenye sekta hii ili kuongeza tija zaidi, mara tu baada ya kupata ridhaa ya kuendelea kuwatumikia Oktoba 29. Uwekezaji huu utakwenda sambamba na ule wa sekta za madini, kilimo, mifugo, biashara na viwanda.
Shamra shamra za wananchi wa Pangani mkoani Tanga katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) tarehe 29 Septemba, 2025.
Ahsanteni sana wananchi wa Same na Mwanga kwa mapokezi mazuri, leo tulipoanza kampeni zetu katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkoa huu ni moja ya mashuhuda wakubwa wa maendeleo ambayo nchi yetu imeyapata chini ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mafanikio haya makubwa ni pamoja na kukamilika kwa awamu ya kwanza ya Mradi wa Maji wa Mwanga - Korogwe - Same, viwanda vipya, mapinduzi kwenye kilimo na kuimarika maradufu kwa utalii na biashara ndani ya mkoa na mpakani mwa nchi.
Azma ya CCM ni kuhakikisha mazuri haya yanaendelea, huku nchi yetu ikidumu katika amani, utulivu na mshikamano.
Nimehudhuria ufungaji wa Mkutano wa 11 wa wadau wa Lishe uliofanyika Bunju, Dar Es Salaam leo. Katika mkutano huo ambao mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ulipambwa na maazimio ambayo yalilenga kuhakikisha kuwa vita kubwa dhidi ya utapia mlo inapata sura mpya.
Nikizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,nimetumia nafasi kuwaasa mabwana na bibi lishe utayari wa serikali kuendelea kuwapa ushirikiano katika nyanja zote kuhakikisha maazimio ya Kikao chao yanatekelezwa.
Akizungumza kikaoni hapo, Waziri Mkuu wa JMT Bwana Kassim Majaliwa Majaliwa amewaakumbusha wajibu wao na kazi kubwa iliyombele yetu ya kupambana na utapiamlo ambao unaonekana kukumba baadhi ya maeneo haswa mikoa inayolima sana huku akiwakumbusha kutumia vyakula vyenye virutubisho.
Ninawashukuru sana wananchi wa Korogwe na Mombo mliojitokeza kwa wingi wakati tukihitimisha kampeni za Urais za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Mkoa wa Tanga, kabla ya kuelekea Mkoa wa Kilimanjaro.
Ahsanteni sana na Mwenyezi Mungu awabariki.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza Ndugu Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’ mara baada ya kuwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Muheza mkoani Tanga tarehe 29 Septemba, 2025.
Kibaha Mjini tayari wameitika kumsikiliza Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoan Pwani.
#oktobatunatiki#kazinaututunasongambele
Matukio mbalimbali katika picha kutoka Chalinze Mkoani Pwani kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mkuu kwa CCM leo tarehe 28 Septemba 2025.
#oktobatunatiki#kazinaututunasongambele