Mnaonalalamika tuzo ya Mwezi zimetolewaje wakati wengine wana mechi moja wengine wana mechi mbili
Tufanye wote tumecheza mechi moja bado Kocha Fadlu ana takwimu nzuri za mechi ya kwanza kuliko Kocha yeyote maana alishinda 3-0
Jean Charles Ahoua katika mechi ya kwanza alikua na takwimu nzuri kwa kutoa Assist kaliiii
Tuache hiyo tutumie mchezo wa mzunguko wa pili bado Kocha Fadlu ana takwimu nzuri kwa kushinda bao 4-0
Ahoua anatakwimu bora katika mchezo huo kwa kuhusika kwenye mabao 3
Mkisema mechi moja moja tunastahili tuzo mkisema mechi zote mbili bado tunastahili tuzo
"Moja ya hatua katika kushughulikia suala la utekaji kwa sababu hatujaridhika na hiki kinachofanyika, TLS inaandaa kongamano la kitaifa ambalo tutawaaalika wataalamu mbalimbali, Watanzania wote, tutakaa tujadili hatima yetu. Hata kijijini kukitokeza jambo ambalo tunaona halipati mwafaka, mila na desturi yetu kama Watanzania na Wabantu wa sehemu ile ni kukaa pamoja kujadili ili kuazimia tufanye nini. Kwa sababu hatuwezi kukaa kuendelea na haya matamko ya kitoto, ni kuhusu maisha, huu ni uhai, huu ni usalama, nani yupo salama? Kwa hiyo moja ya mambo tunayotaka na tutakayoyasimamia ni haya makongamano. Kuna moja itahusu suala la uwekezaji ardhi na wazawa tupate majibu kama Watanzania, suala la pili ambao ndilo tutakaloanza nalo ni kupotezwa kwa watu, ambao ni uhalifu wa kimataifa, siyo kosa la kikatiba la ndani, ni uhalifu wa kimataifa, huu ni uhalifu mkubwa na ambao siyo tu tujikite kwenye mahakama za ndani, tunaweza kwenda hata kwenye mahakama za kimataifa za uhalifu kama ICC"
"Kwa hiyo baada ya kongamano hilo ndipo tutakapoona tufanyeje, nia yetu kama TLS ni kuhakikisha tunalinda usalama wa Watanzania, usalama wa mipaka ya nchi yetu, usalama wa rasilimali zetu na kila alichotujaalia Mungu katika taifa letu kitumike kwa masilahi ya wenye nchi ambao ni sisi wananchi na siyo watu wachache. Nilisoma tamko la jeshi la polisi linalohusu mkutano wa Zoom maana yake kuna kufinywa haki za kikatiba, maana yake jeshi la polisi linaingilia mifumo ya mawasiliano ya watu, inasikiliza mawasiliano ya watu, na inatumia kusikiliza kwa namna hiyo kutisha watu, wametoa tamko la jumla ambalo linakituhumu chama cha siasa wakati kama polisi wangekuwa wana uhakika wangelalamika kwa Mujibu wa Sheria ya vyama vya siasa"- Mwabukusi.
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi akizungumza usiku wa Jumamosi katika mtandao wa Clubhouse kupitia jukwaa la Sauti ya Watanzania.
VIDEO:
Septemba 09.2024 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam inatarajia kutoa hukumu ya shauri lililofunguliwa Mahakamani hapo na wananchi watatu (3) dhidi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) likilenga kupinga Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kusimamiwa na TAMISEMI
Kutoka Mahakamani hapo tunakuletea kile kilichojitokeza leo, Jumanne Septemba 03.2024 kuhusiana na shauri hilo.
NB: undani wa taarifa hii unapatikana kwenye YouTube ya Jambo TV
#VIDEO: Chadema Kanda ya Kaskazini imezindua oparesheni KUCHA ambayo lengo lake ni kukataa uchafuzi na wizi wa kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa November mwaka huu 2024.
Oparesheni hiyo imetangazwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Godbles Lema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo August 24,2024 katika eneo la Soko Kuu Mkoani Arusha.
“Hatutoki hapo tunasubiri matokeo, hakuna kitu kina nguvu kama kujiamini, hatutaibiwa kura hakuna Mgombea wetu kuenguliwa, Mimi siwezi kuwa kwenye mitaa yote, hii kazi tunaweza kuifanya kwa pamoja” —— Lema https://t.co/YpzsajBtm2
🚨🚨KESHO ANAYEWEZA AFIKE MAHAKAMA KUU DAR ES SALAAM‼️🚨👇🏾
Wakili Kisabo alifungua kwsi dhidi ya polisi katika kesi ya @DEUSDEDITHSOKA na wenzake
Imepangwa kusikilizwa kesho tarehe 27 Aug 2024
Kila mwenye uwezo afike saa 4 (10 am)
#FreeDeusdetithSoka#FreeFrankMbise #FreeJacobMlay
✊🏽
‼️POLICE BRUTALITY - BUNDA‼️
#NoJusticeNoPeace#Tanzania
Polisi wa Lalago Sub station kesi yenu imetufikia kwa mauaji ya Baraka Makongolo ambaye askari wenu alimpiga hadi kupelekea kifo chake wakati hadi pesa mlishapewa na ndugu kijana atoke
Mkamnyima hata PF3 ya matibabu!
Makatili sana ninyi
Na Kenan Kihongosi unajua kila kitu!
IGP usipowajibisha na kuwajibika ujue nyie ndo mnachafua hali ya hewa!
#JusticeForBaraka
Lazima haki itendeke na wahusika wawajibike!
#TutaelewanaTu
VIDEO:
Wananchi wa kijiji cha Kidogobasi kata ya Ruhembe Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamelazimika kufunga huduma za kijamii,shule ,zahanati pamoja na ofisi ya kijiji kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutatua mgogoro wa shamba kati ya watu 21 na kijiji hicho.
Mgogoro huo uliodumu zaidi ya miaka 20 umewalazimu wananchi hao kufunga huduma hizo kwa saa 24 na kusababisha wanafunzi kukosa masomo.
Serikali ya kijiji cha Kidogobasi inamiliki shamba lenye ukubwa wa ekari 108 ambapo ekari 78 kati ya hizo wameingia mkataba na wawekezaji ambao hulima shamba hilo kwa makubaliano ya mgawanyo wa asilimia 40 ya mapato yake hutolewa kwa Ofisi ya serikali ya kijiji hicho, ambayo husaidia pia malipo ya walimu wanne wanaojitolea kufundisha shuleni kwa miaka mitano sasa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Shaka Hamdu Sahaka akizungumza kwa njia ya simu amesema kuwa kwa sasa wananchi wawe na utulivu kwani msimamo wa serikali utatolewa.
Mtu wa kwanza kunipa 🎤 nizungumze kwenye jukwaa la kisiasa ni Jacob Mlay, leo Mlay, Deusdedith Soka na Elie's Mbise wametekwa hawajulikani walipo, vitendo vyetu vitawaleta hadharani subirini.
Wewe upo online muda huu unaweza kufanya shughuli zako kwa amani kabisa.
@DEUSDEDITHSOKA yupo MATEKA kwa kupigania nchi yake ambayo ww upo huru kufanya mambo yako saizi.
Ndugu wa SOKA wanahangaika vituo vya polisi kumtafuta mtoto wao bila mafanikio. Wewe ndugu zako wapo na amani wanafanya kazi zao kwa amani.
Unashindwa kupost hata picha ya Soka ukiogopa na ww utapotezwa?
Unaogopa kurepost post za Soka kwasababu utapotezwa?
Unahisi baada ya SOKA nani anafuata?
Hii hali unafikili itaendelea mpaka lini?
SHIRIKI KUKOMESHA UTEKAJI KWA KUREPOST , KUPOST POST ZA KUPIGANIA HAKI ZA KUISHI KWA AMANI WATU WANAONEKANA WAMENYIMWA HIYO HAKI.
REPOST 200 kwa Soka 🙏🏾
ALERT: Polis wanaye Deusdedith Soka na wenzake. OCD wa Chang’ombe na Chalamila wanajua kila kitu. Maagizo ni kuwa Deus asiuone huu ulimwengu tena. Wanadai anajifanya mjanja. Kelele mnazopiga zinawatia hofu kutimiza adhma yao ya kuondoa uhai wake. Fungeni na kusali, mbele kiza. 🙏