Nenda Rwanda halafu utasema masikini ana ustaarabu au hana.
Ustaarabu ni msingi muhimu sana (prerequisite) wa maendeleo. Moja ya changamoto ya maendeleo yetu Tanzania ni Swahili civilization. Corrupt, lazy, uncultured, uncouth, and unprogrammed.
Hauwezi kufanya maendeleo kama huna uniform population to certain extent. People who share values, principles and ideals and are willing to stand for and defend them.
Hapa kwetu kila kitu ni random, look at how corrupt we are as a society, bodaboda anavuka taa nyekundu, daladala linasimama barabarani nje ya kituo, raia anamaliza maji anatupa chupa chini, serikali haijengi pavement za barabara, masoko yana matope, raia hawapandi miti, think of how random we are behaving from top down.
That is a typical civilizational issue. We must fix that with laws, punishment and everything in between.
🚨🇹🇿 HATUA ZA KUFAUTA UNAPOTAKA KUNUNUA ARDHI NDANI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
..
◾Ukipanga kununua ardhi au kiwanja Tanzania, ni muhimu kufuata hatua za kisheria na kufanya uhakiki wa kutosha ili kuepuka utapeli au migogoro ya baadaye. ⤵️
Huyu ni Simai Mohamed Said Mbuge wa Jimbo la Tunguun (Zanzibar)
Wasilisho la mbunge huyu leo hii akichangia bajeti ya wizara ya fedha, limebainisha dhahiri ndani ya serikali kuna msigano mkubwa.
Mbunge huyu alitoka kabisa nje ya mada kuchangia hoja iliyokuwepo mezani na kuanza kumshambulia mtu anayedai yupo ndani ya serikali kwa kumuita Yuda
Kwa mujibu wa video hii, Mbuge huyu anamtaja Yuda kwa sifa zifuatazo
1. Anatumia vibaya nafasi ya kuaminika na rais kumsaliti
2. Mtu huyo amefitini watu ambao walikuwa wanakaa siti za mbele bungeni (mawaziri) na sasa wako backbench. Amefitini sana wafanyabiashara na kupotezea wengi ndoto zao za kisiasa.
3. Mtu huyo amekuwa akilitumia kanisa kuifitini serikali
Hadi hapa nilikuwa nimetatizika sana kumjua mtu wenye wasifu hapo juu.
Lakini mbunge huyu akanirahisishia kazi alipoongeza kuwa
4. Yuda anajidai alikuwa anapendwa na hayati Magufuli wakati enzi za utawala wake alimtupa mbali huko nje ya nchi.
Hili halikuwa tena fumbo kwangu.
Ni hivi karibuni, katika msiba wa mama mzazi wa hayati rais Magufuli, John Nchimbi, Makamu wa rais, amenukuliwa akielezea jinsi alivyokuwa karibu na hayati Magufuli wakiitana watani.
Jinsi alivyokuwa akichukua pipi za Magufuli kwa kuwa hakuwa akila pipi, jinsi alivyotaka kumteua ubunge kupitia nafasi 10 anazopewa rais, na hadi jinsi alivyomteua balozi japo alishamwambia nia yake ya kutaka kupumzika.
Nchimbi katika kutaka kuthibitisha hili, akaomba wasaidizi wake wamletee simu yenye ujumbe aliotumiwa na Magufuli ambao ameutunza mpaka leo na aliuonyesha kwa familia yake yote.
Kwa hiyo, mbunge huyu Mzanzibari ameshaanza kutupa code kuwa kuna kutoaminiana ndani ya viongozi wa juu wa serikali.
Nachelea kusema mbunge huyu hakuingea haya kwa bahati mbaya bali imetokana na vikao vilivyofanyika sehemu na kuaminishana haya aliyoyaongea leo, na ametumwa kuyawasilisha.
Ujumbe mwingine unatumwa hapa ni vita dhidi ya kanisa ambalo halijatajwa.
Kama alimaanisha kanisa la Nchimbi, basi kuna vita visivyo vya wazi kati ya watu fulani ndani ya serikali na Kanisa Katoliki.
End of evening rant
🇹🇿 Mtu aliyekuwa analipwa TSh 5,000,000 mwezi Desemba 2025 na bado analipwa TSh 5,000,000 leo (1 Juni 2026) amepunguziwa mshahara.
Kimya kimya.
Desemba 2025: 1 USD = 2466 TSH
TSh 5,000,000 = ~$2,028
Leo, June 1 2026: 1 USD = 2610 TSH
TSh 5,000,000 = ~$1,915
Ili ubaki na thamani ile ile ya mshahara wa Desemba, leo ungehitaji kulipwa karibu TSh 5,294,320.
Maana yake umepoteza karibu:
❌ TSh 294,320 kila mwezi
❌ TSh 3.5 milioni kwa mwaka
Bila kupunguza mshahara wako.
Bila kubadilisha kazi.
Ndiyo maana watu wengi duniani kwenye nchi mbali mbali wanaanza kuhifadhi sehemu ya akiba yao kwenye USD na stablecoins. - Yaani USDC AU USDT.
Sio kwa sababu wanapenda usd.
Ni kwa sababu hawataki pesa zao zipungue thamani.
Mimi naona kuna fursa kusaidia watu kununua tbills / UTT au public market stocks Tanzania ili waweze kupunguza hasara.
People are making $10k–$100k/month with one laptop.
Most people use AI like a toy.
Smart creators use AI like an EMPLOYEE.
10 AI workflows quietly making people rich in 2026:
🧵👇
#TajiriLaKihaya
Ni Ukweli Usiopingika kwamba WANAHARAKATI WANALIPWA….
hasa waliopo Nje ya nchi kwa huku kwetu na kuna foundations kibao tu za HUMAN RIGHTS ACTIVISTS karibu kila Nchi duniani kote….
ila Kwa yaliotokea Oct 29. haikuhusiana na Malipo haya wala msukumo wa wanaharakati…
Wananchi wenyewe tu walichoka… kuna raia waliandamana hata hawana SmartPhone… wengine hawapo hata mitandaoni…
Yaliotokea ni matunda ya Udhalimu wa Viongozi wetu….
Huwezi zuia chama kikuu cha Upinzani chama kinachoPendwa zaidi Tanzania nzima- KUTOSHIRIKI UCHAGUZI MKUU…
Umfunge Mgombea Urais wa Chama…anaependwa zaidi na Vijana…
Alafu u expect ZERO REACTION… HAIWEZEKANI!
Tusijifiche kwenye malipo ya FORD FOUNDATION…
Hawajaanza leo kulipwa… wanalipwa toka enzi… kila mtu analifaham hili… wanalipiwa RENT, CHAKULA na UPKEEP ZOTE na hata Kutoa Elimu, yale ma space nk. Ni kazi kama kazi zingine tu. Wengine wanaotaka kuongeza Elimu… wanapewa ufadhili!
Hili lipo wazi… na sijui kwa nn WANAHARAKATI wanalificha hili,hawataki lijulikane!
Ila haihusiani kivyovyote vile na yaliotokea Oct 29th.
Tuliweke hili sawa!
@MsigwaPeter Mjomba wewe umeshakuwa sigari Kali sasa! Pande zako zote mbili hazina msimamo.
Kama umerudi upande wa sasa basi uzibe na gundi upande wa pili ili usiww rahisi kudonolewa na kiberiti pande zote.
@IsPmar@HildaNewton21@daviddjumbe Hii nchi Kila mtu anajihami. Tumejaa woga sana.
Nilikuwa makini kufuatilia ufm-DW..unafika muda wa taarifa ya mafwele wanaweka nyimbo ya Nandi. Nimezima radio kmmk.
Zama za Ofisi ya Msajili wa Vyama kuwa mchezaji namba 12 wa CCM FC zimekwisha.
Dola isome alama za nyakati. The writing is on the walls!
Msajili STOP THIS NONSENSE ya kutaka kufuta CHADEMA. Utafutwa wewe, No doubt about this!
Tume ya Chande iliyoundwa na Rais imetoa Taarifa inayosema wananchi wanailalamikia Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutokutenda haki kwenye kusimamia shughuli za vyama vya Siasa. Badala ya Msajili kuchutama, kuwajibika na kubadilika anarudia makosa yaleyale yaliyopelekea mauaji yaliyoanza Oktoba 29.
Msajili anajua, Watanzania wanajua na Dunia inajua kuwa Kuna ushahidi wa kutosha wa CCM kufanya makosa makubwa kuliko hata ambayo msajili ameituhumu Chadema, hatukuwahi kuona hatua zozote zimechukuliwa na Ofisi hii ya Msajili.
Ofisi ya Msajili ijue WATANZANIA SIO MABWEGE. Tunachukulia tishio lolote dhidi ya CHADEMA ni tishio dhidi ya Demokrasia. An attack to one, is an attack to all.
Iacheni CCM ifanye Siasa za Ushindani dhidi yetu. Nasi tufanye siasa za ushindani dhidi yao.
Acheni kuwa mbeleko ya CCM. Mtaanguka nayo. Ujumbe huu sio wa Msajili tu bali pia ni kwa VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA pia. Kaeni pembeni acheni vyama vya Siasa vifanye Siasa.
Mnataka watu wangapi wafe ili mpate somo?
#TajiriLaKihaya
Kitu nlichojifunza Duniani…
Kuna mambo mengine yanatibiwa na MUDA!
kuna matatizo mengi yanaisha kwa kuyapa MUDA….
kwa mfano ; kuna umri kijana hutaki kusikia mambo ya NDOA kabisaa… na hujitazamii kama siku moja utawahi KUOA/KUOLEWA. Na unaweza fika mbali zaidi ukawaona watu waliopo kwenye ndoa kama Washamba au wehu!
Ila MUDA sahihi ukifika… unapata tu NAFSI yenyewe inakuambia SASA MUDA WA KUOA/KUOLEWA umefika!
Unaitaka mwenyewe NDOA…
Vivyo hivyo kwenye UZINIFU…
Kuna umri unaona ni sifa kulala na Wasichana wakali…. Binti yeyote unayemtaka unampata…
Binti mrembo unaemuona unatamani ummiliki wewe… hata kama sio kumiliki walau Upitemo utie sahihi yako!
Ila kuna MUDA ukifika unajiuliza maswali magumu… yote haya unayafanya kwa faida gani? Faida ya nani? Na kwa manufaa yepi??
Je kuna cheti unapata? Unaridhika? UCHI WAKO UNASHIBA?
Kila siku unawaona wazuri kuzidi wa jana…. Mabinti wazuri Hawaishi… inamaana utamaliza Dunia nzima? Uwezo huo unao? Alafu utapata nini???
Kimsingi unagundua ni TAMAA tu ya NAFSI… umeiruhusu NAFSI yako ikutawale…
TAMAA haiishi… na Haina faida yeyote!
MUDA huo Umefika kwangu, Alhamdulillah🙏🏽
Na Muomba Mwenyezi Mungu Aniongoze katika njia iliyonyooka…
Allah anasema ndani ya Quran;
Surat Ar-Ra'd (13:11)
“Hakika Allah HABADILI yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo ndani ya nafsi zao."
Nafsi yangu nmeibadili kuanzia jana usiku kwa ajili ya Mwenyezi Mungu…
Na Allah anatuahidi tunaofanya jitihada na kujinyima matamanio yetu kwa ajili yake kwamba;
Surat Al-Ankabut (29:69)
“Na wale waliofanya jitihada kwa ajili Yetu, kwa yakini Tutawaongoza kwenye njia Zetu."
Na Muomba Allah azidi kunipa Qauli na msimamo thabit katika njia hii nlioichagua🙏🏽🙏🏽