Naitwa Edger E Mwakabela maarufu kama SATIVA17. Kwa siku mbili tarehe 9 na 10 mwezi wa 4 mwaka 2025 nimekuwa na Lugha YA MATUSI dhidi ya Jeshi la polisi @tanpol
Siandiki huu waraka kwaajili ya KUOMBA MSAMAHA, nataka niwape taarifa ambao wamenijua JUZI. Kwahiyo kama unahisi huu uzi kwaajili ya kuomba msamaha ishia hapa.
Mimi ni mmoja kati ya wachache ya watanzania ambao nimefanikiwa kuponea kwenye UTEKAJI unaofanywa na SERIKALI chini ya JESHI LA POLISI. Kwa muda mrefu tumekuwa tukiambiwa SERIKALI ndiyo inateka watu na kuwapoteza, sasa hilo mimi lilinitokea na nikaishi.
Nilipigwa RISASI YA KICHWA na kuenda kutupwa PEMBEZONI mwa mto wenye MAMBA NA VIBOKO WAKALI, nikipona hapo basi niliwe na wanyama wakali waliopo MBUGANI kama FISI, simba na wengine waliopo ndani ya MBUGA YA KATAVI.
Yote hayo MUNGU ALINIEPUSHA NIKAISHI. Tangu siku hiyo mpaka leo licha ya kumtaja muhusika wa UTEKAJI WANGU ila HAKUNA hatua amechukuliwa zaidi ya kupandishwa vyeo JESHINI (MAFWELE). Na kibaya ni kwamba tangu mwaka jana mwezi wa 9 amekuwa akinitafuta kimya kimya aniue.
Nimeishi maisha ya kukimbizana na jeshi la polisi kwa muda wa zaidi ya miezi 8 sasa. Hakuna hatua kama serikali wala nchi imechukua kwenye tukio langu la UTEKWAJI. Gharama ninazotumia kujitibia majeraha ya RISASI YA KICHWA MPAKA SASA ni zaidi ya MILIONI 55.
Ndugu zangu jana wamenipigia sana simu, lengo sio kunilaumu ninavyotukana, lengo nikujaribu kunipooza HASIRA ZANGU kwa jeshi la polisi. Wanajua ninayo haki ya kufanya vile nafanya ila ndio TANZANIA.
Nikiona mtu kafanyiwa UNYAMAA na jeshi la polisi MOYO WANGU hautulii kabisa, maumivu ya kichwa yanaanza UPYA. Bora nitukane NIPONE na naona inasaidia maana naona nao MATUSI YANAWAUMA.
Hii ndio njia nimeichagua kupunguza hasira zangu maana HAKI SIWEZI KUIPATA KWENYE HILI TAIFA. Kwahiyo PUNGUZA USHAURI ULIENIJUA JUZI ACHA SHOBO.
TUTAKUWEPO๐ซต๐พ๐