Hii sakata ya Wamachinga inaonesha umuhimu wa UTAWALA wa SHERIA.
Niliuliza walivyopewa “vitambulisho” - Kwa SHERIA gani?
Nikaonekana mbaya.
😂😂😂
Sasa wenye Nchi wanatumia SHERIA kuwahamisha.
Endeleeni kumuomba RAIS kama Mungu badala ya kulazimisha UTAWALA wa SHERIA.
Bunge haliko huru,
Polisi wanapiga na kuumiza raia,
DPP anabambika watu kesi,
Mahakama hazitendi Haki.
Mwisho wa siku watu watakuja kutafuta njia nyingine ya kupigania na kupata Haki zao.
"Uamuzi mdogo uliotolewa na Jaji leo hatujaridhika nao, Uamuzi katika mapingamizi yote mawili. Jaji ambaye kwa sasa ni Jaji Kiongozi hajaonyesha uongozi wa kutenda haki. Tutakwenda kukutana kama chama kutafakari kwa kina wakati Mawakili wakishauriana na Watuhumiwa." Mhe @jjmnyika
#BreakingNews:Jaji Mustapha Siyani baada ya kutoa uamuzi wa shauri dogo kwa kutupilia mbali mapingamizi 2 ya utetezi, Jaji huyo ameamua kujitoa kuendelea kusikiliza kesi hiyo kwa kile alichodai hataweza kusikiliza shauri hilo mfululizo kutokana na majukumu ya kuwa Jaji Kiongozi.
#Siku92MboweGerezani leo 20/10 mahakamani:njia kadhaa za #JusticeForMbowe Ama DPP awasilishe hati ya nolle prosequi mashtaka yafutwe Mwenyekiti @freemanmbowetz awe huru au Jaji Siyani aamue maelezo ya Adam yaliyochukuliwa nje ya muda kwa kuteswa yasikubaliwe.
Haki inayocheleweshwa ni haki inayokataliwa. Jaji Mustafa Siyani wakati anajiondoa katika kesi hii anatoa sababu kwamba inaweza kwenda miezi 4. Hadi sasa washtakiwa watatu wapo gerezani zaidi ya siku 380, FAM yupo kwa siku 92. Hivyo, bado kuna miezi mingine kabla ya maamuzi?
RECAP!
JAJI kiongozi, Mustafa Siyani, aliyekuwa akisikiliza shauri Na. 16/2021 la Freeman Mbowe na wenzake 3 amejitoa katika kesi hiyo punde baada ya kufanya maamuzi katika kesi ndogo leo
"Hivyo kwa majukumu niliyonayo nimeona nijitoe, aje Jaji mwingine haraka iwezekanavyo"
Jaji: Na hivyo nahairisha shauri hili mpaka msajili wa mahakama Kuu atakapoleta Jaji mwingine...
Jaji kiongozi ananyanyuka kutoka katika kiti cha maamuzi, huyo anaondoka zake...
Mahakama imerejea, kesi Na. 16/2021 imetajwa.
Jaji: ni sawa tunapaswa kuendelea na shahidi lakini nikaomba nishauriane na mawakili
Sasa nimeona kwamba shauri hili ni moja ya shauri linalopaswa kuisha kwa haraka
Kama shauri likienda mfululizo ingechukua miezi kama minne
Hakika tunahitaji rehema za Mungu. Raia ni kama hatuwezi kurejesha tena mifumo thabiti ya kisheria. Tunazo tetesi za chini sana kwamba baada ya kutoa uamuzi huu anajiondoa katika shauri hili kwa hiari yake. Kwanini asingeacha mwingine aandike rulling? Hebu tusubiri kusikia..
Jaji amekataa hoja za upande wa utetezi kwa maoni yake binafsi bila kutaja hata kifungu kimoja cha sheria cha kuonyesha sababu kutupilia mbali mapingamizi ya upande wa utetezi. Kwanini Jaji anafanya maamuzi ya hukumu kwa mtazamo wake na siyo wa kisheria? "kwa uelewa wangu" HOW?
Jaji: Ni vigumu kuondoa dhana kuwa Adam Kasekwa aliwaongoza kumtafuta Moses Lijenje.. Na Pande zote mbili hawabishani kwamba Adam Kasekwa alisafirishwa kuja Dar Es Salaam, Hata Lilian Kibona alitueleza kuwa alijulishwa kuwa mume wake alisafirishwa kuja Dar Es Salaam...
Jaji: Kwa Maoni yangu kwa kuwa Adam Kasekwa alikuwa na Moses Lijenje na Mohammed Ling'wenya alikuwepo Rau Madukani ni Maoni yangu kuwa jambo la kuanza kumtafuta linaleta MANTIKI kwamba palikuwa na Juhudi za kutaka kujua alikuwa wapi..
Jaji: Upande wa Jamhuri sasa wameniletea kesi mbalimbali kwa ajili kufanya rejea, kuhusiana na uamuzi sasa kwanini Adam Kasekwa amekamatiwa Moshi na kuja kuhojiwa Dar es Salaam..
Jaji: Hivyo kwa mujibu wa wakili Robert Kidando muda uliotumika kusafirisha watuhumiwa haupaswi kuwa sehemu ya Masaa manne. Kuhusiana na shauri hili sasa ambao upande wa Jamhuri wanakiri sasa kuwa walikuwa na Adama kasekwa.
Jaji: Hivyo baada ya kupitia pia mawasilisho ya pande zote, nawashukuru sana, Kwa Upande wa Jamhuri wao walisisitiza kuwa maelezo yalichukuliwa kwa mujibu wa sheria kwamba Kifungu cha 50(2) unaondoa muda huo katika hesabu za saa nne kutoka awekwe chini ya ulinzi
Jaji: Kwa mujibu wa Moses Ling'wenya alisikia walipokuwa Moshi akilia kwa sauti ya zege.
Lilian pia kama shahidi wa tatu ambaye ni mke wa Adam Kasekwa kwa alithibitisha kuwa alimuona Adam Kasekwa kuwa kateswa na kwa kuthibisha kwa makovu na alivyokuwa anatembea..
Jaji: Ushahidi wa Adam Kasekwa unaonyesha alipofika Dar es Salaam siku ya Tarehe 07 mwezi wa O8 alipelekwa TAZARA na Mbweni, na siku ya tarehe 09 alitishwa ilikuweka sahihi, ilithibitishwa pia kupitia Shahidi wa pili Mohammed Ling'wenya..
Jaji: Adam Kasekwa alikanusha kwenda kuwaongoza Polisi wale waliomkamata, kwenda maeneo kadhaa Mji wa Moshi na Arusha. Alikanusha pia kupelekwa Central Dar es Salaam bali Kituo cha polisi Tazara.
Jaji: KINGAI NA MAHITA wote wanakubali kuwa walisafiri kuja Dar es Salaam, Na wakakabidhiwa kwa Msemwa. Kingai anasema baada ya kufahamishwa haki zake kisheria alihojiwa siku hiyo hiyo. Kwa Upande wa utetezi, Mshtakiwa anayetajwa Moses Lijenje..