Civil engineer👷 available for professional building construction consultancy,founder of @+Y_generation,guitarist,motivational,arsenal fans for life, love God
Kila siku unapoanza siku mpya ifikirishe akili yako ikupe majibu namna ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na namna unavoweza kujiongezea kipato,Fanya hivo kwa mwezi mmoja tu utafurahia mabadiliko chanya ya Hali yako ya kipesa
Kuna dhambi ukizifanya lazima zikuumbue. Ukijitia kiburi, ushupaze shingo, uonekane huna hatia ndio unaharibu kabisa. Dhambi za hivi zikishajua una kiburi huwa zina tabia ya kukufuata mguu kwa mguu mpaka ule matunda ya kiburi chako kwa ukamilifu.
Dawa ya dhambi hizi huwa ni kumeza kiburi, uache kujitetea kizembe, ukubali aibu, udharaulike, ufedheheke, unyenyekezwe kisha uukusanye ujasiri wa kuufungua ukurasa mpya wa maisha kama mwenye dhambi anayejutua dhambi zake.
Mfalme Daudi alipotumia madaraka yake kuzini na Bethsheba—mke wa raia mnyonge Uria—kiburi cha dhambi kilimchochea kukimbilia kuficha dhambi kuliko kushughulikia matokeo ya hatia yake. Dhambi huja na ‘busara’ zake. Busara hizo zikamwelekeza Mfalme Daudi kuja na mpango wa amani wa kumpa Uria Mhiti ‘ofa ya kurudi nyumbani kwa mapumziko mafupi.’ Daudi alitaka Uria alale na mkewe wakati wa vita. Daudi alitaka maridhiano na uhalifu wake. Daudi alitumia amani na Uria kama mkakati wa siri wa kufunika dhambi.
Uria, kwa upande mwingine, hakujua kinachoendelea nyuma ya ofa ya Mfalme. Dhambi ilikuwa imetendeka gizani wakati yeye akifanya kazi ya kizalendo kulipigania taifa lake vitani dhidi ya Waamori. Kwake, Uria, kulala na mke wake wakati nchi iko vitani ilikuwa usaliti mkubwa kwa wapiganaji wenzake. Uria alikuwa anawawaza wanyonge wenzake wanaopambana na Waamori wakati Mfalme Daudi anawaza namna ya kufunika dhambi yake na kulinda heshima ambayo hata yeye mwenyewe anajua hakuwa nayo.
Uria aliukataa mpango huo wa amani hewa wakati akijua wazalendo wenzake wanapambana na Muamori. Kukataliwa kwa mkakati huo wa kufunika dhambi kulichochea vibaya mno kiburi cha Mfalme Daudi na kumwingiza kwenye uhalifu mbaya zaidi. Daudi aliagiza Uria awekwe kwenye vikosi vya mbele ili ale jeuri ya uzalendo wake. Kweli mnyonge Uria aliuawa na mfalme akaamini amepoteza ushahidi na angeishi kwa amani na mke wa Uria.
Hapo ndipo Nathan, kiongozi wa dini, alipojitokeza na kusimama kwenye nafasi yake kumkemea vikali Mfalme Daudi. Nathan alinyoosha maneno kuwa, “Mungu anaenda kukuvua nguo.” Kilichomuokoa Daudi ni ule moyo wake wakukubali ametenda dhambi, kujuta na kutubu. Daudi hakuendelea na propaganda za kuzimisha sauti ya kiongozi wa dini anayepigania haki ya mnyonge asiye na yeyote wa kumtetea.
Tunachojifunza hapa ni kwamba Mungu siku zote huwa upande wa mnyonge. Dhambi dhidi ya mnyonge huwa haiachani na wewe mpaka ukubali aibu ya kuikiri na kuijutia. Mungu akikupenda anakupa nafasi yake pili kwa kukuletea mpaka Nathan akuonye. Ukishupaza shingo ukakwepa aibu ya kukiri dhambi lazima ule matokeo ya dhambi. Kilio cha mnyonge hakiendi bure.
[kwa simulizi kamili rejea 2 Samweli 11:1-27; 12:1-23]
Kuna kilio na kijembe kimezoeleka masikioni: Kinahusu watu walio nje kuwa ni wachochezi. Kina kasoro nyingi, nashauri kiachwe.
1.Watu si wajinga kushawishiwa wasichopenda. Kama huamini, nawe washawishi wakufuate wewe.
2.Siyo sifa njema kuwa na wakimbizi nje. Tuifanye nyumba yetu kuwa ya wote - wema na wakorofi.
3.Kubaki ndani si kigezo cha uzalendo. Kuna mijizi, mifisadi, michokoraa, miuza siri za nchi na mirafi imejaa humu ndani.
Haya anaandika PhD BAGONZA.
REPOST 500
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
@CivilEngDis is this page run by a real civil engineer,the reinforcements of this staircase is completely wrong yet published for the public education?
The older you get, the more you realize peace isn’t quiet, it’s the absence of pretending. No forced smiles. No fake bonds. Just truth, even if it’s lonely but peaceful.
@pallnandi we men are goals orinted,adding a year in our lives is not an achievement rather a reminder that time flies so fast while we are getting old,we celebrate something we achieved from our efforts, in our dictionary birthday is a grace not a goal
Kujipendekeza sio ‘networking.’ Watu hufuata thamani. Ikiwa huna ufumbuzi fulani unaorahisisha kazi za watu, unaweza kufahamiana na watu wengi na isikusaidie.
Tumia muda mwingi kujifunza, kujitafuta na kujenga umahiri hata kama itakubidi kuwa mkiwa kwa muda. Thamani yako ikianza kuonekana, ‘network’ zitakuja zenyewe wala hutotumia nguvu.