Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Steven Kimondo, ametoa onyo kali kwa watawala akisisitiza kuwa serikali isijidanganye kwamba inaweza kujenga au kulinda amani ya nchi kwa kutumia amri za kisheria zinazowanyang'anya wananchi haki zao za kikatiba.
Mchungaji Kimondo ameyasema hayo jana julai 5 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya, ambapo amefafanua kuwa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini halina nia njema, bali limekusudiwa kukikandamiza na kukifuta kabisa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kiongozi huyo wa kiroho ameeleza kuwa kisingizio cha "tishio la kiusalama" kinachotumiwa na serikali kupiga marufuku siasa kinafichua ubaguzi mkubwa, kwani mikusanyiko mingine ya maelfu ya watu kama ile ya mashabiki wa timu ya Wanyanga wakisherehekea ushindi wa ligi ya taifa inaruhusiwa na kulindwa kikamilifu na Jeshi la Polisi.
"Tusijidanganye kwamba amani itatokea wakati watu wanazidi kunyang'anywa haki zao... Kwa jinsi wanasheria wanavyosema, hana mamlaka ya yeye kuzuia. Leo nilikuwa naangalia TV tuna mkusanyiko wa Wananyanga wanasherehekea ushindi wao kwa ligi ya taifa, watu wamekusanyika wengi polisi wako pale wanalinda. Kuna ubaya gani kama vyama vya siasa watafanya mikutano yao halafu polisi walinde? Kuna shida gani?" amehoji Mchungaji Kimondo.
Mchungaji Kimondo pia ameshangazwa na mkanganyiko wa wazi ambapo wakati tangazo la kuzuia mikutano hiyo likitolewa kwa nchi nzima, viongozi wa ngazi za juu wa serikali, akiwemo Waziri Mkuu, wameonekana wakiendelea kufanya mikutano ya hadhara mikoani na kuhutubia wananchi, akitolea mfano wa ziara zilizokuwa zikiendelea kupitia waziri mkuu Mwigulu Nchemba.
Ametamatisha kwa kutoa wito kwamba Tanzania ni nchi ya wananchi wote, na kuwaonya viongozi kuacha kutengeneza mifumo ya kiutendaji inayoliletea taifa madhara huko mbeleni. Amesisitiza kuwa amani ya kweli na ya kudumu itapatikana na kudumishwa iwapo tu haki itatendeka kwa kila mmoja bila ubaguzi wa kiitikadi.
Leo, tarehe 26 Aprili, 2026 ikiwa ni Siku ya #Muungano, tujikumbushe mwaka 2014 ambapo Mhe. @TunduALissu aliwasilisha maoni kuhusu #Muungano katika Bunge Maalum la Katiba.
Watanzania ICHANGIENI CHADEMA ifanye kazi zake.
Mimi nimekuwa ktk siasa za upinzani tangu 1990.
Nawashuhudia Chadema ndio chama pekee kinachojali masilahi yetu.
Kama mtadharau ushuhuda huu mtalia na kusaga meno.
Ndugu wanachama wa CHADEMA na Wapenzi wa Demokrasia Nchini.
Chama chetu kimefunguliwa rasmi kufanya shughuli za siasa. Hii ni fursa muhimu katika kuendelea na mapambano ya haki, uhuru na uwajibikaji katika Taifa letu.
Lakini ukweli usioepukika ni huu
hatuna ruzuku hata ya SENTI MOJA.
Hii ina maana kwamba uhai, nguvu na uendelevu wa CHADEMA uko mikononi mwetu sisi wenyewe.
Hatuna budi kuchukua jukumu.
Hatuna budi kusimama.
Hatuna budi kuchangia.
Kila Mwanachama na kila mpenda Demokrasia ana wajibu wa moja kwa moja, kuchangia CHADEMA.
Usione mchango wako ni mdogo.
Usisubiri mwingine achukue nafasi yako. Kila senti unayotoa ni nguzo ya kusimama kwa chama hiki.
Tujenge utamaduni wa kuchangia bila kusukumwa. Tujenge tabia ya kusaidia chama kila wakati. Hapo ndipo tutakapopata uhuru wa kweli wa kisiasa na kiutendaji.
Mimi nipo, na nimeanza.
Na wewe pia ni wakati wako sasa.
Chukua hatua.
Anza kuchangia.
Simama na CHADEMA.
Kwa pamoja, tutakijenga chama imara na Yaifa lenye HAKI.
Tuchange tu kwa namba maalumu za CHAMA na Akaunti za Benki ili kujenga uadilifu wa Taasisi Imara.
Mikakati zaidi inakuja baada ya vikao kuanza.
Asanteni.
Kama Lissu alipigwa Risasi 17 na hakufa basi Mungu anampango maalumu na Tundu lissu kwa ajiri ya Taifa hili
Na lissu hata kufa mpaka mpango wa Mungu utimie
“Mchungaji”
Repost 210
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Steven Kimondo, ametoa ujumbe mzito wa kiroho kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu, akimtaka kuwa hodari na mwenye moyo wa ushujaa katika kipindi hiki anachopitia.
Akizungumza katika mahojiano maalum hivi karibuni, Mchungaji Kimondo amemnukuu Lissu kupitia kitabu cha Yoshua 1:18, akimtaka asitetereke wala kulegea kwa kuwa Mungu yuko pamoja naye, huku akimfariji zaidi kwa neno kutoka kitabu cha Yeremia 1:8 linalosema: "Usiogope kwa sababu ya hao, maana mimi niko pamoja nawe nikuokoe."
Mchungaji Kimondo amesisitiza kuwa Lissu asijione yuko peke yake huko aliko, kwani anaamini kuwa harakati na utetezi wa haki alioufanya akiwa nje ni mpango maalum ambao Mungu alimtuma auyafanye kama mjumbe wake kwa ajili ya taifa. Amebainisha kuwa muujiza wa Lissu kuishi mpaka leo, licha ya kushambuliwa kwa idadi kubwa ya risasi mnamo mwaka 2017, ni thibitisho tosha kuwa kiongozi huyo ana ulinzi wa kiungu, akilinganisha na matukio ambapo watu wengine hufariki kwa risasi moja tu, na kusisitiza kwa ujasiri kuwa: "Lissu hatakufa mpaka atimize kusudi la Mungu katika taifa hili."
Aidha, kiongozi huyo wa dini ametoa mwito kwa Watanzania wote kuungana na watu wanaotetea haki pamoja na wale wanaopigania upatikanaji wa Katiba Mpya kwa ajili ya mustakabali wa Tanzania. Amesema kuwa harakati za kudai Katiba Mpya na haki zisichukuliwe kama faida ya vyama au makundi kadhaa ya kisiasa, bali ni hitaji muhimu kwa ajili ya ustawi wa taifa zima kwa ujumla ili kuleta usawa na maendeleo ya kweli kwa kila raia bila kujali itikadi yake.
Mchungaji Kimondo amehitimisha kwa kusema kuwa taifa linapita katika wakati ambao unahitaji ujasiri na unyoofu wa moyo, akiamini kuwa kusudi la Mungu kwa Tanzania litatimia kupitia watu walioandaliwa kusimamia ukweli. Amewataka waumini na wananchi kuendelea kuliombea taifa ili liweze kuvuka changamoto za sasa kwa amani, huku haki ikitendeka kwa kila mmoja kama msingi mkuu wa utulivu na umoja wa kitaifa.
Mchungaji Steven Kimondo wa kanisana KKKT amesema amekuwa akifuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi inayomkabili Tundu Lissu, akieleza kusikitishwa na kile alichokiita ucheleweshaji wa mchakato wa haki, hususan katika hatua za rufaa.
Akizungumza katika mahojiano maalum, Kimondo alibainisha kuwa hatua ya mwisho iliyosikika wazi ilikuwa mwishoni mwa mwezi wa pili, ambapo rufaa inayohusiana na shauri hilo ilikatwa. Hata hivyo, tangu wakati huo, amesema kumekuwa na ukimya mkubwa bila taarifa za maendeleo ya kesi hiyo.
“Kinachonisikitisha ni kwamba tangu rufaa ilipokatwa, kumekuwa kimya kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa,” alisema Kimondo.
Aidha, alisisitiza kuwa licha ya kutokuwa mtaalamu wa sheria, anaamini kuwa haki ya msingi ya mtuhumiwa ni kusikilizwa kwa kesi yake kwa haraka, akisisitiza kuwa kisheria mtu hubaki hana hatia hadi pale mahakama itakapothibitisha vinginevyo.
“Tundu Lissu bado hajahukumiwa, hivyo anastahili haki ya kusikilizwa kwa wakati. Ukimya huu ni kama kumuumiza mtu ambaye bado hajapatikana na hatia,” amesema
Kimondo pia alieleza kuwa anaelewa kuwa mahakama zinaongozwa na taratibu na mipaka ya kisheria, lakini alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati ili kulinda haki za msingi za wahusika.
Wachambuzi wa masuala ya sheria wanaeleza kuwa ucheleweshaji wa kesi unaweza kuathiri haki ya mtuhumiwa na kuibua maswali kuhusu ufanisi wa mfumo wa utoaji haki nchini
Hata kama humpendi au unakichukia Chama chake. Ukweli utaendelea kubaki huyu ni wa pekee? Anapendwa na Mungu na anamlinda. IQ yake ni kubwa.
Chuki inawafanya watawala kumtesa baadala ya kumtumia ktk ujenzi wa taifa.
Bila shaka watalipa mbele za Mungu sasa na baadae siku ya kiama.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 95
Kaaya: Naomba Mahakama ilinde taarifa zangu binafsi naomba tulizingatie hilo.
Jaji Ndunguru: Shahidi unapaswa kurelax kabisa. Kama kuna swali la kukudhalilisha hatutaruhusu ujibu. Tutaingilia kati. Wewe kama shahidi fanya kazi yako.
Hayo mengine kwamba yanaandikwa mitandaoni achana nayo. Watu wengine wanaweza kucheka kwasababu hawafahamu.
Mahakama tukiona unatwezwa utu wako tutaingilia hayo ya mitandaoni hatuhusiki nayo na hatuwezi kuyazungumzia hapa.
Mhe. Lissu : sasa turudie. Je una Advanced Diploma
Kaaya: Ninayo.
Mhe. Lissu: Ni ya kitu gani na umepatia wapi?
Kaaya: Advanced diploma Refrigilation and air condition na electrical installation. Nilipata chuo cha ufundi Veta na baadae integlobal college iko Nairobi.
Mhe. Lissu: waeleze maana ya NACTE unaifahamu?
Kaaya: Naifahamu.
Mhe. Lissu: Je hicho chuo kinatambulika na NACTE.
Kaaya: ndio kinatambulika.
Mhe. Lissu: Je una shahada ya Chuo Kikuu?
Kaaya: Ninayo.
Mhe. Lissu: Ipi?
Kaaya: Chuo kikuu huria cha Tanzania.
Mhe. Lissu: Umesoma nini na lini?
Kaaya: Nina degree ya LL.B mwaka 2019.
Mhe. Lissu: Kumbe ni Mwanasheria Mwenzangu. 😂
Sasa waeleze majaji kama hayo yote umeyaeleza una shahada ya Sheria.
Kaaya: Sikuandika..
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama ushahidi wako wa week iliyopita na yale maelezo yako ya Polisi kuwa una advanced diploma in refrigilation and air condition?
Kaaya: Sijaeleza kabisa..
Mhe. Lissu: Je ulieleza sababu ya kutokueleza mambo haya matamu na mueleze.
Kaaya: Sikueleza.
Mhe. Lissu: ulisema umesoma chuo cha Unique Academy?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Hiki ni chuo gani hivi?
Kaaya: sio chuo kikuu, sio chuo kinachotoa advanced diploma, hiki chuo tulipelekwa maafisa wa polisi. Huwa tunapelekwa maeneo mbalimbali ikiwemo UDOM tunaendaga. 😂
Mhe. Lissu: ukisema sina uhakika nalo ni jibu. Ukisema sijui nalo ni jibu. Sasa nataka unijibu swali langu hiyo unique academy inatoa diploma ya chochote.
Kaaya: nafikiri inatoa.
Mhe. Lissu: je hicho chuo kinatambulika na mamlaka ya ithibati ya hivyo vyuo vya ufundi?
Kaaya: Sijui kabisa.
Mhe. Lissu: shahidi umesema umesomea chuo cha Polisi Zanzibar umepata cheti cha mahudhurio na chuo cha Polisi Moshi na Dar es salaam na Unique Academy kote umepata vyeti?
Kaaya: Ndio.
Mhe. Lissu: Sasa nikisema wewe Inspector John Kaaya nikisema huna qualification yoyote nitakuwa nakosea?
Kaaya: utakuwa unakosea.
Mhe. Lissu: soma maana ya Professional qualification kwenye PGO.
KAAYA: means advanced diploma and above
Lissu: Je kwa tafsiri hiyo ya PGO ambayo ni advanced diploma au shahada ya Chuo kikuu?
Kaaya: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo huna qualification ila una vyeti vyeti vya hapa na pale? Kweli au sio kweli?
Kaaya: Sikueleza hayo mambo.
Mhe. Lissu: Sasa nataka tuzungumze kuhusu masuala ya mtandaoni. Umesema wewe ni mtaalamu.. hebu tuambie ulisema lazima ufanye usajili kwanza ili uweze kuingia mtandaoni. Je utaratibu huo ni wa aina hiyo hiyo katika mitandao yote?
Kaaya: Utaratibu unatofautiana.
Mhe. Lissu: Je YouTube inamilikiwa na Google?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Mtu yeyote mwenye Google account anaweza kuingia YouTube?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je ni kweli kwamba ili kuwa na Google account unachohitaji kuwa nacho ni username na password peke yake?
Kaaya: ni kweli.
Mhe. Lissu: je ukiwia na Google account unaweza kuingia YouTube?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: je ukiwa na Gmail account huhitaji channel URL ili kupakua video au kuangalia?
Kaaya: waheshimiwa majaji nataka nitoe maelezo kidogo. KWAHIYO SIO KWELI.
Mhe. Lissu: kuna kitu kinaitwa YouTube user account kweli au si kweli?
Kaaya: ni kitu sawa na URL ni kitu kimoja.
Mhe. Lissu: Sasa hiyo channel URL umuhimu wake inakuwezesha ukiwa nayo ku like au ku comment kwenye picha za YouTube mitandaoni?
Kaaya: Ni sahihi ukiwa na email inatosha.
Part 96 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.