Liwalo na liwe!!
Naandaa kitabu cha nyimbo kabisa na sehemu ya kusoma neno! Maana i dont want to be caught off guard on this special and historic moment
Niliuliza kuhusu aliko rais Jumamosi. Halijajibiwa. Naongeza maswali mengine. Mlimpeleka Hospitalini (Mzena) kufanya nini? Kwanini mmemtoa leo jioni kwa siri, kwa magari yenye namba za kiraia? Na hali ya Bashiru ikoje? Hali ya mlinzi wa rais ikoje? Tunajua. Sasa mpangieni TUKIO.
Afya ya Rais ni suala la umma. Kikwete alipotibiwa tezi dume Marekani tuliambiwa. Mkapa alipotibiwa nyonga Uswisi tulijulishwa. Baba wa Taifa alipougua saratani ya damu London hatukufichwa. Kwa nini kuna kigugumizi juu ya afya ya Rais Magufuli? Au ndio kila zama na kitabu chake?