#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 68
Anaendelea Mhe. Lissu na maswali kwa Shahidi wa Jamhuri
Mhe. Lissu : Je mtu akisema kukinukisha vibaya sana ni kosa la uhaini?
George: Ndio amefanya kosa la uhaini.
Mhe. Lissu : Sasa kifungu cha 39(2)d ya Penal Code inasema kuhusu kosa la uhaini anamsomea. Je hapo kwenye hicho kifungu wapi kuna KUKINUKISHA SANA SANA?
George: Hayo maneno hayajatajwa kwenye hicho kifungu.
Mhe. Lissu : ulisema nimeitisha serikali?
George: Ni sahihi nilisema hivyo.
Mhe. Lissu : Ulisema uchaguzi mkuu uko Kikatiba?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Sasa waeleze katika kifungu cha 39(2)d kama neno uchaguzi limetajwa?
George: Halijatajwa.
Mhe. Lissu : Uchaguzi Mkuu je?
George: Halijatajwa.
Mhe. Lissu : Kuzuia uchaguzi mkuu halijatajwa?
George: Halijatajwa.
Mhe. Lissu : Wewe hivyo vyeti vyako umenunua sio bure.
Watu : ๐๐๐๐๐๐
Mhe. Lissu : Ulisema Tundu Lissu alitaka kulazimisha serikali kufanya anayoyataka yeye?
George: Ni sawa sawa nilisema.
Mhe. Lissu : Uliandika hivi maelezo yako maneno haya niliona yana nia ya kuitisha serikali.
Sasa nakusomea kifungu cha 55(2) cha Penal Code Pia nitakusomea Media Services Act p. Sec. 52 pia nitamsomea sheria ya TISS (Idara ya Usalama wa Taifa) kifungu cha 3 kinasema tishio kwa usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Lissu : Ni ushahidi wako kuwa mtu anayepinga sheria ni kosa la jinai?
Georg : Inategemea.
Mhe. Lissu : Sasa nianze na Penal Code S. 55(2) kuhusu nia ya Uchochezi inasema kitendo kauli au chapisho hakitakuwa cha uchochezi kama kitakuwa na lengo kuwa serikali imekosea haitakuwa ni uchochezi. Kama unaonyesha makosa au mapungufu katika serikali au katika sheria au utendaji wa haki mahakamani kwa lengo la kubadilisha mambo hayo na anayehamasisha wakazi wa jamhuri ya muungano kubadilisha kwa njia halali sio kosa la jinai.
George: Kwa njia ya halali sio kosa.
Mhe. Lissu: Sasa hujaonyesha sheria toka nianze.
Mhe. Lissu : Sheria ya habari inasema kuionesha serikali imekosea halitakuwa kosa la uchochezi sasa mimi kusema uchaguzi wa hovyo unasimamiwa na serikali ya hovyo ni kosa la jinai?
George : Ndio ni kosa la jinai.
Mhe. Lissu : Twende kwenye Sheria ya usalama wa taifa. Imetaja mengi ikiwemo ujasusi, uhujumu uchumi na matishio ya kutumia serious violence je sheria hii ya usalama wa taifa ni kosa la jinai?
George: Kweli ni Kosa la Jinai.
Mhe. Lissu : Je kusema kutaka mabadiliko ni kosa la uhaini kwa mujibu wa sheria hii?
George: Ukifuata utaratibu sio kosa.
Mhe. Lissu : Huo utaratibu ukoje?
George: Kwenda kuyapeleka Mahakamani.
Mhe. Lissu : Je kuitisha maandamano ya amani ni utaratibu?
George: Ndio utaratibu.
Mhe. Lissu : Ni wapi sisi tulisema hatufuati utaratibu?
George: Sasa kuzuia uchaguzi ni kosa.
Mhe. Lissu : Nani alisema hatafuata sheria?
George: Ni wewe mwenyewe.
Nyie huyu George kuna nati haiko sawa kuna vitu anaongea mpaka unaweza kudhan kakatwa kichwa.๐ eniwei tuendelee
Mhe. Lissu : Jana ulisema kwamba baada ya kuonyeshwa ile video clip uliunda team ya Wapelelezi?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Nimesoma maelezo ya Amin Mahamba. Je ulisoma maelezo ya Amin Mahamba?
George: Mimi sikusoma maelezo ya Mahamba halafuโฆ..
Mhe. Lissu : Acha kiherehere ulisoma maelezo au hukusoma?
George:Sikusoma.
Mhe. Lissu : Mahamba anasema aliunda timu tatu za upelelezi?
George: Ni kweli aliunda.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze Majaji kuwa kama ulionesha Amin Mahamba aliunda timu ya wapelelezi?
George: Sikuandika maana nilishaandika maelezo tar. 08.
Mhe. Lissu : Sasa uliandika maelezo tarehe 10 ya nyongeza pia ulisema kuhusu mahamba kuunda timu ya upelelezi?
George: Sikuandika hilo hata tar. 10.
Mhe. Lissu : Ulisema uliripoti kwa Kamishna Ng'anzi kuhusu kuteua timu ya wapelelezi kama lipo kwenye maelezo yako?
George: Linawezekana kuwa sijaliandika kabisa.
Part 69 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
@Tanfootball@tplboard@NBCTanzania@azamtvtz Mnaangalia biashara na matumbo yenu kuliko mamilioni ya watu,,gharama zimetumika kubwa mno,watu wamejikusanya kutoka kila kona then,,kipuuzi tu,mmeshindwa kuyamaliza mambo usiku huo huo mnalala nayo na bado jua linawaka yanawashinda mnahairisha mechi,,Achieni hizo ofisi mnapwaya
@ZPlanmaster Naomba kujua ilikuaje Suleiman akawa na wanawake wengi na Bado akawa na ushikaji na Sir God ila mimi mwenye mke mmoja nikijaribu kujitwalia kasuria kangu kamoja kanisa linaniona nafaa kukemewa kama pepo