@Sativa255 Mwenyekiti Aandai Mikutano Hiyo NI Kazi Ya Secretariat Ya Chama Sasa Je Makamu Mwenyekiti Ajui Km Kuna Uchaguzi Nikichogundua Adi Saa Hizi Kwa Hoja Wameshindwa #chaster
@ExMayorUbungo Haya Mnatuambia Ni Chama cha Demokrasia Ilihali Amtaki Kuiishi Hiyo Demokrasia Nachomwambia Tundu Lisu Akaze Apo Apo Mpk Kieleweke #chaster
08
— Baada ya kuwa chini ya uangalizi maalumu ili atimize miaka miwili na ahukumiwe.
— Hatimaye, 2018, April, tarehe 20, Gamble alisomewa mashtaka yake na kupatiwa adhabu ya miaka miwili.
— Adhabu hiyo haikuwa kali sana kwani alionekana kuonesha tabia njema kwa kipindi chote hicho cha miaka miwili alipokuwa ameshikiliwa.
— Kwa sasa kijana huyo ni mtu huru. Yupo uraiani na amebadilika.
Swali: Je ni kweli amebadilika au bado hajakinukisha?
SIJUI!😁
07
— Kane aliendeleza harakati zake za kuuanika uovu mitandaoni. Hakuishia CIA, alisogea mpaka FBI na kuigusa pia National Security.
— Lengo lake lilikuwa ni kuwakosesha usingizi WAMAREKANI. Na alifanikiwa.
— Lakini, mwaka 2016 ukawa ndiyo mwisho wa harakati zake.
— Walimdaka akiwa nyumbani kwao. Nchini Uingereza. Japokuwa haikuwa ni kazi nyepesi. Kijana alijua kujificha.
06
— Miongoni mwa watu ambao walikuwa ni wanufaika wa taarifa hizo ni Julian Assange. Mmiliki wa WikiLeaks. Akazichapa katika tovuti hiyo.
— Huyu bwana walimkamata 2019.
— Na mwaka huu, juzi tu hapo, iliripuka habari yake ya kuachiwa mitandaoni.
— Ana visanga vyake vingi huyu. Tutamzungumza siku nyingine.
05
— Mwaka 2015 kazi ikaanza. Shabaha ya kwanza ikawa ni John Brennan. Huyu alikuwa ni Director wa CIA kwa wakati huo.
— Mchongo ulianza June. Mwaka huohuo 2015. Mpaka kufikia October kila kitu kumuhusu Director wa CIA kikawa mikononi mwao.
— Yeye pamoja na wenzake, waliingia kwenye mawasiliano ya bwana huyu. Wakatazama ujumbe aliokuwa akiutuma. Amri alizokuwa akitoa na mipango mingi ambayo ilihusu Iran na nchi nyingine za mashariki ya kati.
04
— Alianzisha timu ya wadukuzi wa mtandaoni. Akaiita CRACKAS WITH ATTITUDE. Yeye akiwa ni kiongozi wao.
— Walikusanya kidogo kidogo taarifa kutoka kwa wahusika wa CIA. Taarifa walizoamini zingekuja kuwasaida.
— Na kwakuwa walidhamiria kumuua nyoka, wakaamua kupiga kichwani!
— Walianza kwa kuwalenga maafisa wakubwa wa idara hiyo. Viongozi.
03
— Yeye ni Muingereza ambaye alikuwa akizichukia harakati za kijeshi za serikali ya Marekani huko mashariki ya kati.
— Akatamani kufanya jambo.
— Na wazo hilo, lilikuja baada ya kujaribu kudukua mifumo mingi ya kwenye kompyuta kisha akafanikiwa.
"Kwanini nisiidukue serikali ya Marekani?"
— Pengine aliwaza kwa kujiuliza hivyo. Na hatua ya kwanza ikawa ni kutafuta timu ambayo ingemsaidia.
02
— Kuchezea mifumo ya kiteknolojia ni kipaji chake cha asili. Akiwa na miaka kumi, alinunuliwa kompyuta yake ya kwanza.
— Alipofikisha miaka 13, akaweza kudukua mifumo ya games mbalimbali kwenye kompyuta hiyo.
— Huo nd'o ukawa mwanzo wa kunogewa na tabia hiyo ambayo kijana huyu aliifurahia.
— Huyu hapa, kijana ambaye aliitetemesha dunia kwa kuivua nguo mifumo ya CIA, akiwa na miaka 15 tu!
— Nyaraka zote ambazo wao waliamini ni za siri na hakuna wa kuweza kuzifikia, kijana alizifunua na kuzigeuza atakavyo.
— Jina lake ni KANE GAMBLE (Tamka: Ken Gembo)...
Na huu ni UZI maalumu kuhusu kisanga hiki...
Wakati unaanza kutiririka, usiwe mchoyo, fanya uungwana mdogo tu, angusha REPOST hapo chini ili maarifa haya yawafikie wengi zaidi....
Twen'zetu!👇🏽