MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
Mapokezi ya kihistoria na yenye hamasa kubwa yaliyotokea Leo tarehe 29 Mei 2026 Mkoa wa Kilimanjaro kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Kenani Laban Kihongosi, aliyewasili rasmi kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Wanachama wa CCM, viongozi wa chama na serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro wamejitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo, jambo lililoonesha mshikamano, uhai wa chama na imani kubwa ya wananchi kwa CCM na uongozi wake.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha utekelezaji wa Ilani ya CCM, kukagua shughuli za chama, kuzungumza na wanachama pamoja na kuendelea kuhamasisha uwajibikaji, uzalendo na maendeleo kwa wananchi.
CCM inaendelea kusonga mbele kwa nguvu, umoja na mshikamano chini ya viongozi wake madhubuti.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#ZiaraYaKazi
#mtumishiwawote
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
Sanya Stand leo imefurika nguvu ya wananchi wa Wilaya ya Siha na Mkoa mzima wa Kilimanjaro wakionesha imani kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi. Wananchi wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi akizungumza kuhusu maendeleo, mshikamano na mustakabali wa Taifa letu.
CCM ni sauti ya wananchi, nguzo ya maendeleo na tumaini la Tanzania imara. Kazi iendelee, maendeleo yaendelee.
#KaziNaUtuTunasongambele #Sihayamaendeleo #mtumishiwawote
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Shinyanga mjini katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, mkoani Shinyanga tarehe11 Oktoba, 2025.
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi Ilani ya Uchaguzi baadhi ya wagombea Ubunge wa Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Maganzo tarehe 11 Oktoba, 2025.
Shamra shamra za mapokezi ya Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili Kahama mkoani Shinyanga tarehe 11 Oktoba, 2025.
Nimefurahi kufika tena Kahama leo na kuona namna mji huu unavyoendelea kukua kwa kasi huku ukileta neema kwa idadi kubwa ya wananchi wanaofika hapa kutafuta riziki, toka maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Kwa pamoja tumezungumza na kukubaliana na wananchi wa Kahama kwamba watawachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Oktoba 29, ili chama kiendelee na kazi ya kuwaletea maendeleo, kama ambavyo kimefanya wakati wote, huku tukibaki kuwa Taifa moja lenye amani na mshikamano. Ahsanteni sana. Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Shinyanga Mjini, ninawashukuru sana. Wingi na hamasa yenu ni uthibitisho kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni imara, kinaifanya vyema kazi ya kuitumikia nchi yetu, kina ushawishi, kinaaminiwa na ndicho chenye nia na uwezo wa kuendelea kulitumikia Taifa letu huku tukibaki wamoja, wenye maendeleo, imara, wenye amani na utulivu.
Ahsanteni sana kwa hakika ya Tiki zenu Oktoba 29. Mwenyezi Mungu awabariki.
Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Same mkoani Kilimanjaro tarehe 30 Septemba, 2025.
Sehemu ya wananchi wa Same waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro tarehe 30 Septemba, 2025.