Watu huwekeza kwa watu wanaowaamini.
Uaminifu ndio msingi wa mahusiano imara, ushirikiano wa kudumu na fursa kubwa. Jenga tabia ya kuwa mwaminifu katika maneno na matendo yako, kwa sababu watu wengi huwekeza kwanza kwenye tabia yako kabla ya kuwekeza kwenye wazo.
Usihangaike kuthibitisha uwezo wako kwa kila mtu. Endelea kufanya kazi kwa bidii, jifunze, boresha maisha yako, na acha matokeo yazungumze kwa niaba yako.
Kimya chako kiwe sehemu ya mkakati wako, na mafanikio yako yawe jibu lako.
Muda wako utafika. Usipaniki.
Ukiona wengine wanafanikiwa, wanaoa au wanaolewa, usikate tamaa. Furahia mafanikio yao huku ukiendelea kujitengeneza kwa ajili ya wakati wako.
Kila maisha yana ratiba yake. Kinachochelewa si lazima kipotee.
Maisha ya utafutaji si mbio za mita 100, ni mbio za marathoni. Wanaoshinda si wale wanaokimbia kwa kasi zaidi, bali wale wanaodumu bila kukata tamaa. Endelea kupambana, siku moja matokeo yatazungumza kwa niaba yako.
Gen Z wengi si wanachama wa CHADEMA wala hawana kadi ya chama. Hata hivyo, wapo wengi wanaokiunga mkono kwa sababu wanaamini kinazungumza kuhusu changamoto za wananchi na kutetea maslahi yao.
Urithi si kuacha mali pekee, bali pia kuacha maarifa ya namna ya kuitunza, kuiendeleza, na kuifanya izae zaidi. Elimu ya fedha na usimamizi wa mali ni urithi wenye thamani kuliko mali yenyewe.
Familia nyingi za Kiafrika hufilisika baada ya mwanaume kufariki, si kwa sababu mali hazikuwepo, bali kwa sababu hakukuwa na elimu ya kuzisimamia na kuziendeleza.
Nje ya elimu ya darasani, tafuta ujuzi utakaokuongezea thamani. Mjini, ujuzi ni mtaji unaokufungulia milango ya fursa.
Mtu mwenye ujuzi si rahisi kulala njaa—kwa sababu ana uwezo wa kutengeneza thamani popote alipo. 💼📚
Usikope kwa sababu tu ni rahisi kupata mkopo. Kopa pale tu unapokuwa na sababu ya msingi na mpango wa kuurejesha.
Kumbuka, baada ya kukopa kuna wajibu wa kurejesha. Uamuzi wa kukopa bila kufikiria matokeo unaweza kukuweka kwenye mzigo wa madeni usio wa lazima.
Usipoteze muda kuwashawishi watu waelewe stori yako.
Wengi hawajali ulianzia wapi; wanataka kuona umefika wapi.
Pambana kimya kimya.
Mafanikio yako ndiyo yatakayozungumza kwa niaba yako.