TEMPLE MOUNT, JERUSALEM.
Moja ya maajabu pale Yerusalemu ni uwepo wa Kanisa, The Holy Sepulcher na Msikiti, Al-Aqsa karibu kwenye Mlima Hekalu Temple Mount. Hivi vitu vina historia fulani very interesting na yenye fundisho la kiroho. Haya majengo yapo juu ndani ya Hekalu ambalo Sulemani alijenga mwaka 960BC.
Ni sehemu takatifu sana kwa Wayahudi kwa sababu ni mahali pa hekalu la Sulemani. Ni sehemu ambayo inagombaniwa na wakristo na waislamu kuwa sehemu takatifu. Wayahudi nao wanadai ni sehemu yao takakatifu kuliko zote kwa sababu hekalu ya Sulemani lilijengwa hapo.
Kanisa la Holy Sepulcher lilijengwa na kutiwa wakfu katika utawala wa Emperor Constantine mwaka 335 AD. Kabla ya hapo Emperor mwingine alijenga hekalu la mungu, Venus. Waaajemi walipoiteka Yerusalemu wakalibomoa Kanisa mwaka 614AD, na baade vikundi vya kupigania Ukristo, maarufu kama crusaders wakalijenga tena mwaka 1009AD. Unaweza kuona panavyogombaniwa.
Waarabu walipoiteka Yerusalemu kupitia Khalif Kattibu[Umar aibn Al -Kattab] wakajenga msikiti, Al-Aqsa kwa sababu kwamba ni mahali patakatifu kwao, ni mahali Mtume Muhammad aliwahi kusali baada ya kunyakuliwa usiku mmoja kutoka Arabia kimiujiza na kuja Yerusalemu na kurudi. Pili mahali khalif alisali, pakahesabiwa kuwa mahali patakatifu na msikiti ukajengwa mpaka leo ni mahali panagombiwa.
Kuna vitu unaviangalia kimaandiko unaanza kuelewa kidogo kidogo, kwanini panagombaniwa namna hiyo? Soma historia ya Greeks Empire, mahali hapo palitokea ugomvi mkubwa sana na Wayahudi. Inaonekana kila Dola iliyotawala Yerusalemu ilileta mgogoro wa eneo hilo. Roman Empire ndo usiseme wamebomoa hekalu na kujaribu kulijenga na kusababisha vita kubwa kati yao na Wayahudi
Tuangalie kwa picha ya maandiko, kuna nini??
Hii sehemu ni mlima Moria, ambapo Ibrahimu alijaribiwa kumchinja Isaka. Mahali Sulemani alijenga hekalu. Mahali Daudi alitoa sadaka ya kuzuia ugonjwa wa tauni. Ni mji wa Daudi[Daudi aliwashinda Wayebusi].
Mwanzo 22:2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
2 Mambo ya Nyakati 3:1 Ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, juu ya mlima Moria, pale Bwana alipomtokea Daudi babaye alipotengeza mahali pale alipoagiza Daudi, katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.
Jicho la unabii:
Ni sehemu ambayo itabaki kugombaniwa hata baadae,
Mathayo 24:15-17
15 Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
16 ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;
17 naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake;
Biblia inautaja Yerusalemu kuwa mji wa Mfalme Mkuu. Biblia kwa lugha ya Agano la kale ni mji Mtakatifu. Lakini pia mahali pa hekalu/madhabahu. Mahali patakatifu[kwa lugha ya Agano la kale].
Ukiitazama kwa jicho hili utaona madhabahu zingine kama zinataka kutawala mahali hapo. Yaani kujenga madhabahu juu ya madhabahu nyingine.
Disclaimer: [Si madhabahu kwa Kanisa]. Ni mahali patakatifu na madhabahu kwa Wayahudi.
Nadhani mnaofatilia historia mnatambua kwamba Wayahudi wanasema kila siku wana mpango wa kujenga hekalu lingine. Hii siyo hadithi hakika litajengwa.
Sasa mie nilitaka uone kwamba mara kadhaa chukizo la uharibifu lilipotokea Yerusalemu kila dola ilikimbia kudai hekalu la Sulemani ni mahali pao patakatifu. Ni kweli Yesu alisema ile sentensi kuashiria Roman empire itakavyobomoa Yerusalemu, Hekalu na kuchafua madhabahu yake, Mwaka 70 AD. Lakini kuna matukio madogo madogo yanafanania chukizo la uharibu kusimama mahali patakatifu.
Wakatoliki huhesabu kuwa Kanisa la Holy Sepulcher ni mahali patakatifu, mahali ambapo kuna kaburi la Yesu na mahali ambapo tukio la Ufufuo la Yesu lilifanyikia. Hivyo basi kuwa mahali patakatifu sana. [Kwa Wapentekoste ni sehemu ya kumbukumbu tu si Patakatifu].
Kila mahali ambapo uamsho wa Injili uliisha maadui walikuja kutawala. Ukisoma historia ya Kanisa, angalia baada ya mitume kuondoka, walikuja watumishi[maaskofu] wakavuruga doctrines na kutengeneza Dini. Dunia ile ilikuwa 20% ya Mashariki yote ya kati ni nchi za[dini] Kikristo hawakua na nguvu tena za kiroho kwa sababu ya dini, miaka ya 600+ baadae upande ule wakachukua nchi zote.
Muda ukaenda zaidi ya miaka 400 Mungu akafanya nafasi tena, Uingereza ikaanza kuchukua Dunia, uamsho ukaingia watu kama akina John Wycliffe, William Tyndale wakaanza kutengeneza njia za uamsho miaka ya 1500. Uingereza ikawa kitovu cha Injili, watumishi wa Mungu miaka ya 1700+ kama John Wesley, Goerge Whitfield wakapiga Injili hadi Marekani. Kikafuata kizazi cha 1800 wiliam Booth na Smith Wigglesworth. Watumishi waombaji walioweza kuchallenge serikali, mifumo na siasa.
Miaka ya 90 injili nyingine ikaaanza, Injili ya kutia moyo tu, kutekenya hisia za watu. Injili za kuchemsha[goshiwa]. Mungu anakupenda hata ukae uchi. Ni neema tu huhitaji kufunga wala kuomba sana. Imeshakuwa ya kwako wee kiri na kupokea bila[BILA MUKTADHA SAHIHI WA MAANDIKO].
Kanisa limepoa dhambi imekua kawaida tu, ushoga umeingia tena, dini zimezidi kuharibu saivi kuna maaskofu mashonga[mtawasikia wengi zaidi katika ile dini kubwa, wanakuja]. Adui ameingia tena Kanisani. Kwa sababu ya kupoza uamsho kwa mafundisho ya ajabu ajabu ya walimu/manabii wanaotia moyo na kulisha hisia za watu tu. Kanisa halina nguvu, haliwezi ku-confront chochote. Watumishi wote mwilini wapo bize na hela na magari.
Nyakati hizi ndipo Mungu huruhusu mapigo tena. Niliandika mwaka juzi [Shetani anakuja]. Injili itazuiliwa tena Duniani kote. Sheria zitatungwa kuharamisha Yesu kutajwa wala Biblia kuonekana. Tutapitishwa kwenye kipepeteo tena. Kanisa litapepetwa na litasafishwa tena, kabla ya uamsho wa kipindi cha jioni cha nyakazi za mwisho. Huu ni mlango wa mwisho wa Mataifa. Uamsho utakuja ambao haukuwahi kuwepo Chini ya jua. Ndipo mlango utafungwa kwa Mataifa. Shetani anakuja.
Mwenye masikio na asikie.
Ukidharau mwanzo mdogo hata ule mkubwa unaoutaka unaweza usiufikie, ilikuwa safari ya siku tatu kusoma na kutafakari kitabu cha Habakuki, leo tunahitimisha safari hii, na kesho tunaanza safari mpya ya kusoma na kutafakari kitabu kingine cha Sefania.
The same thing, instead of saying will surpass the evangelicals to spread the word of salvation, the focus is to become big denomination. Wrong motive. Wrong Biblically..
Moja ya historia potofu ambayo utaisikia Duniani ni kwamba Ukristo ulienea kwa Upanga/nguvu. Sababu zao??
1. Wakoloni walileta ukristo Afrika kwa kutumia nguvu/Upanga ka kadhalika. Ni kupotosha makusudi ili usikosoe dini zinazosambaza mambo yao kwa upanga. Ule sio Ukristo bali walikuwa na mambo yao wakatumia mgongo wa Ukristo.
Mimi nasimamia mafundisho ya Injili yaliyotakana na Uamsho wa movements za Pentecost, tunajua historia yetu, wamishionari wetu. Hakuna mahali waliwahi kutumia nguvu/upanga kueneza Injili tokea walipoipokea kwa Mitume. Misingi wetu wa Injili ni Uamsho unatokana na maombi. Upentecoste ni movement ya Injili sio dini wala taasisi.
Historia ya Pentecost ndiyo tata zaidi sema haijakuwa documented vizuri. Hakuna Taifa hapa Duniani ambalo halijawatesa Wapentekoste. Wamepitia madhira makubwa sana kunyongwa, kuuliwa, kufukuzwa na kukumbizwa, kuhamishwa makazi/nchi zao. Kwenye uhuru wa kuabudu Marekani ndo wamepata neema kidogo. Kwingine huko kuna kipindi kinaitwa kipindi cha giza. Ilikuwa valangati.
Warumi 11:1-2, 7-8, 11-21, 25-32
1 Basi, nauliza, Je! Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benyamini.
2 Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu,
7 Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa uzito.
8 Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo.
11 Basi nasema, Je! Wamejikwaa hata waanguke kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikilia Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu.
12 Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?
13 Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu,
14 nipate kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao.
15 Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?
16 Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika.
17 Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,
18 usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe.
19 Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi.
20 Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.
21 Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.
25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.
28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.
29 Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.
30 Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao;
31 kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema.
32 Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.