Nimeshiriki sherehe za Muungano wa Shirikisho la Ujerumani , ikiwa ni kumbukumbu ya Muungano wa Iliyokuwa Jamhuri ya Ujerumani au Maarufu Ujerumani ya Mashariki na Ujerumani Magharibi.
Nikiwa Mgeni Rasmi wa sherehe hizo nimepata muda mzuri kueleza tulipotoka na mashirikiano baina ya nchi zetu yalivyoendelea kuwa Imara na yanavyokuwa huku nikikumbusha kuwa mahusiano haya yasiwe kwenye sherehe tu bali yaende hadi kwenye nyanja mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo Utalii, Teknolojia, nk
Nimeungana na Viongozi wenzangu na Wananchi, kuhani msiba wa Baba yetu na Mwenza wa Rais wetu, Mzee wetu Hafidh Ameir Hassan, Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja. Pia nimepata nafasi ya kumuhani Dr. Samia Suluhu Hassan kwa msiba mkubwa uliomkuta. Tunaendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe nguvu, subira, na imani kushinda huu mtihani wa kumpoteza Mwenza wake. #InnallillahWainnaillahRajoun
Salamu nyingi za pongezi na Dua njema toka kwangu Binafsi na Menejiment nzima ya Ofisi ya Rais , Utumishi na Utawala Bora kuja kwako Mh. Deo Ndejembi, Makamu wa Rais wa JMT katika siku hii muhimu Unapoapa kuanza kazi kubwa ya kuisaidia Nchi yako na kumsaidia Mh. Rais kutimiza ahadi zake za Ilani kwa Watanzania. Ahadi yetu ni ushirikiano mkubwa na kuchapa Kazi kwa kiwango kikubwa sana. #KaziNaUtu #KaziIendelee
Nimefanya ziara Kata ya Mandera, Halmashauri ya Chalinze kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na Wananchi. Katika ziara hii tumekubaliana kuendelea kumalizia miradi ambayo haijamalizwa na kuhakikisha ubora. Serikali imetenga kisi cha shilingi Milioni 760 kumalizia miradi katika sekta ya Elimu, Afya, utawala na maendeleo ya jamii. #ZiaraJimboni #Chalinze
Ninawatakia Waislamu na wananchi wote kheri ya Sikukuu ya Maulid. Kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) iwe sehemu ya tafakari na mafundisho katika maisha yetu juu ya; kuishi katika ukweli, kusimamia haki, upendo na moyo wa kujitoa kwa wenzetu.
Tusherehekee kwa furaha na upendo, tukimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aendelee kulibariki Taifa letu lidumu katika amani, umoja na ustawi, na kutufanikisha kutimiza yote tuliyojipangia kwa maendeleo ya nchi yetu.
Mawlid Al Nabi Mubarak.
Asante sana, Dr. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wetu wa Chama na Wajumbe wa Vikao kwa Imani Kubwa. Imani ulipwa kwa Imani, Sintowaangusha. Tutanadi na Kuelimisha Umma kuhusu Ilani kwa Uzuri na Njia Bora Zaidi.
Mapema leo katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi, Dodoma, nilipoambatana na Mgombea Mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kuchukua Fomu ya Kugombea Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ahsante kwa wanachama wote wa Chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakazi wa Dodoma, wanakijiji wenzangu wa Chamwino na wananchi wote kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu kwa salamu za kheri.
Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.
Heri ya Sikukuu ya Nanenane kwetu sote.
Leo tunapoadhimisha Sikukuu ya Nanenane, tuna kila sababu ya kujipongeza kwa hatua kubwa ambazo tumepiga kwenye sekta za kilimo, mifugo na uvuvi. Kwa upekee, mwaka huu tumeweka rekodi nyingine ambapo nimezindua Maabara Kuu ya Kilimo, Dodoma, ambayo itatuhakikishia usalama wa chakula tunachokula na tunachouza nje, hivyo kuvutia wanunuzi zaidi.
Serikali yenu imechukua hatua mbalimbali kukuza sekta hizi ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa mitaji, masoko, ruzuku, na kukuza matumizi ya mbolea na mbegu bora. Tumefanya haya tukitambua tija kwenye sekta hizi, ndiyo tija kwa Taifa.
Ninawasihi wananchi kutumia maarifa, hasa ya matumizi ya teknolojia na mbinu bora za uzalishaji waliyoyapata katika Maonesho ya Nanenane kuongeza tija kwenye shughuli zenu. Pia, kama kaulimbiu ya maonesho haya inavyosisitiza, tujiandae kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya sekta hizi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Maabara Kuu ya Kisasa ya Kilimo iliyopo Mtumba, Jijini Dodoma, tarehe 08 Agosti, 2025.
Tulipohamisha Stendi ya Mabasi Ubungo kuipeleka Mbezi Luis, Dar es Salaam kulikuwa na hofu kwa wananchi kuwa watapoteza fursa za kiuchumi. Ninafarijika kuwa leo nimezindua Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) katika eneo ilipokuwepo stendi hiyo, kituo ambacho kinatoa fursa nyingi zaidi, hasa ajira, kuliko zilizokuwepo awali.
Mradi huu wa kimkakati utaimarisha na kukuza biashara na nchi jirani kwa kuwaunganisha wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa bidhaa kutoka ndani na nje ya nchi. Pia, utapunguza gharama za usafirishaji, utaongeza mapato ya serikali na akiba ya fedha za kigeni, utatoa ajira kwa wananchi na ni sehemu ya jitihada za kufanikisha ndoto ya soko la pamoja Afrika.
Nimeona wananchi wamejitokeza kwa wingi kukodi maduka kwenye eneo hili. Hongereni sana. Hata hivyo, nimewatoe hofu kuwa, kituo hiki siyo mshindani wa Soko la Kariakoo, bali ni sehemu ya wafanyabiashara kujifunza, hasa matumizi ya teknolojia katika kuongeza thamani ya bidhaa na kufanya biashara.
#KumbukiziMuhimu Mwaka 1992 Umojq wa Vijana wa CCM waliita Harambee kwa ajili ya Kuchangia Usafiri wa Wanafunzi Mkoa wa Dsm. Nashukuru kwa kupewa nafasi ya kuchangia Usafiri Vijana wetu. Yaliyofuata ni sehemu ya Historia. Hii ni Kumbukumbu nzuri katika safari ya Maisha. #DindiliMizega #Chipukizi
Nimeshiriki uzinduzi wa mradi wa Maji wilayani yaMonduli wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge Wilayani hapo.
Katika salamu sana nimewapongeza na kuwatakia kheri Wakimbiza Mwenge wa Uhuru , Uongozi wa Wilaya ya Monduli na Halmashauri ya Wilaya ikiongozwa na Mbunge wa jimbo la Monduli Ndg. Fred Lowasa.
Leo imekuwa siku ya baraka ambapo nimeungana na waumini na wananchi katika ufunguzi wa Kanisa la Arise and Shine, Dar es Salaam. Ujenzi wa nyumba za ibada ni maelekezo ya Mwenyezi Mungu kama yalivyoandikwa katika Kitabu cha Hagai 1:8.
Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote za kidini kwani tunatambua na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya taifa letu, pamoja na kujenga jamii yenye maadili na hofu ya Mungu. Nimewasihi viongozi wa dini kuendelea kutoa mahubiri yenye kudumisha amani, umoja na utulivu, hasa tunapoendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu.