Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Jijini Lusaka nchini Zambia leo Novemba 19, 2025.
Makamu wa Rais anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Ukarabati Mkubwa wa Reli ya TAZARA, itakayofanyika tarehe 20 Novemba 2025 Jijini Lusaka.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Makamu wa Rais amepokelewa na Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Dkt. Elijah Muchima, Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, Maafisa waandamizi wa Jamhuri ya Zambia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoandaliwa kwa heshima yake.
Pamoja na viongozi wengine, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Nchimbi ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Masanja pamoja Mkurugenzi Mkuu TASAC Bw. Mohamed Salum.
Hotuba yangu mapema leo Ikulu, Dodoma nilipozindua Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.
Nina imani na uwezo na weledi wa tume hii. Taarifa yao juu ya kiini cha tatizo itatuongoza kujielekeza kwenye hatua sahihi za kiutendaji na mazungumzo ya kuleta maelewano, kuimarisha usalama, amani na umoja wetu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu awasimamie na kuwaongoza.
DKT. MWIGULU AKUTANA NA KATIBU MKUU WA TEC
Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Novemba 20, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.