#HABARI Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Kigoma imemhukumu Ally Athumani maarufu ‘Kabala’ (56), kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Aidan Omary (30), kufuatia ushahidi uliotolewa katika kesi hiyo.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Agustino Rwizile baada ya mahakama kukamilisha usikilizwaji wa shauri hilo, ambapo ilieleza kuwa mauaji hayo yalihusishwa na mgogoro uliotokana na deni la Shilingi 18,000 ambalo Aidan alikuwa akidaiwa na mshitakiwa.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za mahakama, tukio hilo lilitokea Julai 20, 2024, na mshitakiwa alifikishwa mahakamani Agosti 9, 2024 kwa ajili ya kujibu shtaka la mauaji.
Katika hukumu hiyo, mahakama ilisema upande wa mashtaka uliweza kuthibitisha shtaka dhidi ya mshitakiwa bila kuacha shaka yoyote, hivyo kumtia hatiani kwa kosa la mauaji kinyume cha sheria.
Kutokana na ushahidi huo, Mahakama Kuu imempa Ally Athumani adhabu ya kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kumuua Aidan Omary.
#EastAfricaRadio #TogetherTunawakilisha