ADUI WA MWANAMKE NI MWANAMKE MWENZIE.....!
Nimekumbuka msemo wa Mama yangu,kuhusu Wanawake wasivyopendana na kukosa umoja hata katika maswala muhimu yanayosumbua wao kama ukatili,udhalilishaji,ubakaji dhidi ya Wanawake.
Kwamba 100% Wanawake wanaoenda maofisini iwe ofisi za umma au serikali wanapokuta mtoa huduma ni mwanamke mwenzao uwezekano wa kuhudumiwa vizuri bila shida unashuka hadi 5% au 0% kabisaa.
Asilimia 90% ya wanawake hawapendi kuhudumiwa na Wanawake wenzao mahala popote.
Hivyo hivyo katika biashara,Mwanamke anapokuta biashara anafanya na Mwanamke mwezie basi asilimia za kufanyika hiyo biashara zinashuka hadi 5% hadi 0%.
Kanuni hizi nimezikumbuka wakati huu moyo ukiwa na maumivu na majeraha makubwa ya kuona Mwanamke (mtoto wa Kike) anafanyiwa ukatili huku wenye jukumu la Kumlinda na Kumtetea ni Wanawake wenzie.
Pata picha nchi yetu Rais ni Mwanamke,Waziri wa Ulinzi ni Mwanamke,Waziri wa Jinsia ni Mwanamke, Spika wa Bunge ni Mwanamke,Kamanda wa Polisi mahala alipobakwa Binti JM ni Mwanamke pia.
Lakini uwezi amini kuwa pamoja na Kushika madaraka makubwa na kwa wingi wao ,hawana msaada wowote kwa binti JM aliye bakwa na Kulawitiwa kisha video zake zikasambazwa mitandaoni nchi nzima,
Wala hawana msaada wa mkakati wa kukomesha ubakaji na ukatili dhidi ya Wanawake wenzao kwa ujumla.
Inawezekanaje Kamanda Polisi Dodoma ambaye ni Mama na Mwanamke mwenzao anakosa uchungu wa kumsaidia binti wa Kike.
Badala yake anashiriki kuhujumu na kuharibu kesi ya Mwanamke mwenzake kwa kusema maneno mabaya na ya uongo hadharani ili binti akose msaada na kupoteza haki yake kwa tamaa ya fedha au madaraka.
1.Binti JM hakuwa anajiuza kama anavyo sema Kamanda wa Polisi bali ni binti anaye fahamika rekodi yake vizuri ,mwenendo wake vizuri, na ni binti mwenye wazazi Baba na Mama wote wa Kazi wa Dar es Salaam
2.Binti JM kwa sasa anamiaka 17 na mwaka huu angekuwa anahitimu kidato cha nne kama siyo kukatisha masomo yake akiwa kidato cha pili baada ya kushindwa kuelewa masomo darasani.
3.Binti JM akiwa na umri wa chini ya miaka 18 ,aliajiriwa na Askari wa Jeshi la Polisi ASP FATUMA KIGONDO maarufu kama "AFANDE" ambaye pia ni Mwanamke na Mama pia.
alifanya Binti JM kuwa mfanyakazi wa Bar yake inayojulikana kama THE MARION PUB,Dodoma kati ya mwezi April hadi May alipofikwa na tukio la Kubakwa.
4.Binti JM hakuwahi Kuishi Buza au Jirani na shule ya Msingi Dovya kama ambavyo kwenye Video anayobakwa anawatajia wabakaji wake sehemu anayotoka Dar es saalam huenda ilikuwa ni njia ya Kujilinda wasimsumbue zaidi.
Binti JM amewahi Kuishi na Bibi yake Mabibo Luhanga,kisha baadae kuhamia kwa mjomba wake Kiluvya Madukani Viwanja vya NSSF ,Karibu na tanki la maji la NSSF.
5.Mabinti ambao ni Wahudumu THE MARION PUB ya "Afande ASP" Fatuma Kigondo ndiyo walio mtambua Binti JM Kama mfanyakazi mwenzao ambao walikuwa wamekodiwa chumba kimoja cha kulala pale MRESHENI LODGE na Wanajua tukio lote la Binti kubakwa na kurudi Dar es Salaam lakini wakinyamaza sababu ya Vitisho.
kama kweli JM na wenzie walikuwa wanajiuza basi walikuwa wanauzwa na Afande Fatuma Kigondo.
7.kwa Mujibu wa wazazi wa Binti JM ,wanaseme Binti JM aliondoka Dar es saalam akiongozana na rafiki yake aitwaye SHADYA kwenye kutafuta kazi ya Hotel kama alivyokuwa anauza moja ya mgahawa wa chakula pale Kariakoo.
Walipoenda Dodoma hakukuta tena kazi ya Hotel bali walilazimika kuanza kufanya kazi kwa Afande Fatuma Kigondo yeye na SHADYA kutoka Mwezi April 2024 hadi mwezi May 2024 aliporudi Kiluvya,Dar es Salaam baada ya Kuugua baada ya Kubakwa na kulawitiwa.
8.May 2024,Baada ya Kukutwa na mkasa wa Kubakwa ,aliwapigia simu wazazi wake kuwajulisha kuwa anaumwa lakini hakuwaambia wazazi wake anaumwa nini.
Baada ya Wazazi kuona anaumwa muda mrefu bila kupata nafuu walimtumia Binti JM nauli aweze kurejea Dar es saalam kwa matibabu.
ambapo Binti JM alifikia kwa mjomba wake alipoluwa anaishi Kiluvya Madukani Viwanja vya NSSF jirani na tanki la NSSF ambapo alijiuguza na kupata nafuu.
Wazazi na ndugu walimuhisi kuwa ametoa mimba kwa jinsi alivyougua muda mrefu akilalamikia maumivu hasa sehemu za tumbo na sehemu zake za siri.
Wazazi na ndugu walikuja kuoanisha tukio la kuugua kwake na Kubakwa baada na wao kuona video za binti yao akibakwa na Kulawitiwa mitandaoni.
9.Katika hali ya kushangaza ni baada ya Mama na Baba wa JM kumpeleka rasmi Central Police,Dar es saalam kufungua malalamiko siku 2 baada ya kuona video zile zilizunguka mitandaoni.
1.Polisi walimbakisha JM kituoni na Kuwataka wazazi waondoke wamuache binti yao
watawasiliana watakapo hitajika,ambapo walikaa siku 3 bila kumuona wala kusikia habari za binti yao.
2.Jeshi la Polisi kwa mara ya kwanza likamtafutia makazi binti aliyebakwa na kuficha sehemu waliyompeleka ni ipi kwa maelezo ya usalama wa binti
au taasisi gani kwa maelezo kuwa ameenda kupatiwa msaada wa matibabu ya kisaikolojia.
3.Jeshi la Polisi likaipiga mkwara familia ya JM isiwasiliane na mtu yeyote kuhusu kubakwa kwa binti yao huku wakitaja Jina langu "Boniface Jacob" ambaye hapaswi kusogelea amilia ya JM.
Baadae Jeshi la Polisi likapiga marufuku ya mtu kuhoji na kuitafuta familia ya JM kwa maelezo kuwa tutaiumiza familia.
Hii inaweza Kutafsirika kama nia ovu ya kujaribu kuzuia Wanahabari,Wanaharakati na taasisi ziziso za kiserikali zinazopigania haki za binadamu na utawala bora.
Cha ajabu leo wao ndiyo wanaiumiza familia kuliko sisi wasamaria wema kwa Afisa wa ngazi ya Juu ya Jeshi la polisi kumbatiza JM jina la Malaya,changudoa ,muuza uchi binti wa miaka 17 aliyebakwa.
10.Jeshi la Polisi likatangaza kutafuta wahalifu wawili katika jalada hilo la Upelelezi wao na kuwaomba raia tuwasaidie Polisi kuwatafuta watuhumiwa hao wawili bila ya..
1.Kutaja majina ya watu wanaowatafuta ilituwasaidie kuwatafuta.
2.Kuweka Picha ya wahalifu wanaotafutwa hadharani.
Hii pia inaweza kutafsirika kama nia ovu ya Jeshi la Polisi kutaka kuwaficha wahalifu na kudanganya Jamii ione kuna watu hao wawili bado wanasakwa.
11.Kitendo cha Kamanda wa Jeshi la Polisi kusema binti alitebakwa alikuwa anafanya biashara ya Kujiuza mwili wake,nina kitafsiri kama nia ovu ya Jeshi la Polisi katika kupoteza haki za Binti JM
Kwa kutumia mbinu ya "Ukitaka kumuua Mbwa basi mpe Jina baya."
Nimitarajia kuona Kesi hii Wanawake wote Tanzania wanaungana Kumtetea Binti JM na kujakikisha haki inatendeka kama sehemu ya Kulinda wanawake wengine dhidi ya ubakaji na udhalilishaji.
Boniface Jacob
Ex-Mayor
The voice of the silenced Majority.
HABARI MBAYA KUTOKA MTWARA
Mwandishi wa Habari wa Mtwara Digital Mohamed Mwaya ( @+255 717 505 047 ) amekamatwa na kuchukuliwa na watu wasiojulikana Mchana huu July 24,2024 maeneo ya Bima Mtwara.
Mashuhuda wanasema watu hao walikuwa wanne na waliondoka naye kwenye gari ndogo kuelekea barabara ya Maktaba ya Mkoa.
Tunaomba taarifa hii isambae na kama kuna kosa la kisheria linalomkabili basi apelekwe kwenye vyombo husika kwa ajili ya taratibu za kisheria.
Ahsante
Nimesikia IGP? Nikamsikiliza tena? Kwa kauli yake yeye ndiye anayewatuma polisi kuwaua Watanzania? Ni hatari sana? Usalama wa wetu Watanzania uko rehani?
Tafakari? Mtafakari IGP? Tafakari kauli yake inaondoa tumaini la watu kuishi?