Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 Nchini Ujerumani amekamatwa na Polisi baada ya kuiba basi na kuendesha umbali wa kilomita 130 akimpeleka Mpenzi wake Shuleni.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Vyombo vya Habari vya Ujerumani, DPA na SWR, tukio hilo limeripotiwa baada ya Kampuni ya Usafiri ya eneo la Wiesbaden, Jimbo la Hesse, kubaini kuwa basi lao la abiria limeibiwa mapema siku iliyotangulia kutoka kwenye Karakana yao.
Inaelezwa kuwa Kijana huyo alivunja Karakana hiyo kisha kutumia Ufunguo Maalum (master key), kufungua basi, na kuondoka nalo hadi Mji wa Karlsruhe, umbali wa takriban Kilomita 130, ambako alimchukua Mpenzi wake mwenye umri wa miaka 14 na kumpeleka Shuleni.
Kampuni ya Usafiri iligundua kutoweka kwa basi hilo majira ya saa 12 asubuhi, lakini awali walidhani huenda limechukuliwa na Mfanyakazi mwenzao, hivyo walitoa taarifa Polisi majira ya saa sita mchana.
Baada ya kupokea taarifa hiyo, Polisi walifanikiwa kulipata basi hilo mjini Karlsruhe na kumkamata Kijana huyo, hivyo anakabiliwa na Mashtaka ikiwemo wizi na kuendesha gari bila Leseni.
#MillardAyoUPDATES
*KITONGA MNOO HII IPHONE* *IPHONE 11 PRO* โข โ Storage 64GB โข Face IDโ *BEI* ๐๐ป๐ฐ490,000/= *TOP UP & EXCHANGE โ * *MIKOANI TUNATUMA๐* ๐Kariakoo Mtaa wa aggrey ๐*0683774969* *Link ya kujiunga group share๐๐๐ผ*https://t.co/qJIqEH9xvG