“Ninakabidhi jezi hizi ili tukaandae michezo kwa lengo la kutuunganisha pamoja na mwisho kuhamisha wanachama wa Jumuiya ya Wazazi kujisajiri”Ndg Dkt KellenRose Rwakatale,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi,Morogoro
#ZIARAWAZAZIMOROGORO
“Nimeridhishwa na miradi ya shule zote nilizotembelea Wilaya ya Gairo mmesimamia vizuri tunapaswa kumpongeza sana Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazofanya za kuleta Maendeleo Nchini” Ndg Dkt KellenRose Rwakatale,Mwenyekiti wa wazazi Morogoro
#ZIARAWAZAZIMOROGAIRO
“Kuna vijana Wengine wanamaliza Masomo darasa la saba na kidato cha nne wanalazimishwa kuolewa ,tulikemee hili ili vijana wetu wapate fusra ya kuendelea na Masomo
” Ndg Dkt KellenRose Rwakatale,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi,Morogoro
#ZIARAWAZAZIMOROGAIRO
“Jumuiya ya Wazazi inajukumu kubwa ya Kusimamia Malezi,tuendelee kusimamia Malezi na Maadili ya Vijana Wetu"Ndg Dkt KellenRose Rwakatale,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi,Morogoro
#ZIARAWAZAZIMOROGAIRO
“Ulipaji wa Ada za Uanachama utasaidia Jumuiya yetu kuwa imara kiuchumi"Ndg Dkt KellenRose Rwakatale,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi,Morogoro
#ZIARAWAZAZIMOROGAIRO
“Ili Chama Cha Mapinduzi kiwe na wanachama wa Kutosha Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro ni lazima tujiandikishe kuwa wanachama wa Jumuiya ya Wazazi na CCM
” Ndg Dkt KellenRose Rwakatale,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi,Morogoro
#ZIARAWAZAZIMOROGAIRO
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Vyeti kwa baadhi ya Wadau waliowezesha kufanikisha Matembezi ya UVCCM katika kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika Kijiji cha Paje, Mkoa wa Kusini Unguja
Matembezi ya UVCCM ya kuadhimisha Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yamefanyika katika viwanja vya Mnara Kisonge, Mjini Unguja Zanzibar 5/1/2023,Mgeni Rasmi,Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Hussein Mwinyi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mvugwe -Kasulu wakati akiwa njian kuelekea Kasulu Mjini kufungua Chuo Cha Ualimu Kabanga .
#CCMImara#KaziIendelee
"Dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia serikali anayoiongoza kuimarisha na kuboresha mazingira ya minada yote ya mifugo nchini kuwa ya kisasa ili ichangie zaidi mapato ya serikali, kipato zaidi kwa wote wanaofanya biashara kupitia uwepo wa minada"Shaka
"Nachukua changamoto ya uhitaji wa jengo la kupumzika wanunuzi na wauzaji na nitaiwasilisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambayo ndio msimamizi wa minada ya mifugo nchini Ili kuitatua changamoto hii hata kwa kutenga sehemu ya fedha wanazokusanya kila mnada unapofanyika"Shaka
"Mnada huu unatoa fursa za ajira na mapato ya serikali kupitia biashara ya mifugo. Pia wapo wananchi wanaotoa huduma za chakula na vinywaji pamoja na mahitaji muhimu kwa wanaofika hapa"Shaka H.Shaka,Katibu wa Itikadi na Uenezi TAIFA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ametembelea na kukagua mnada wa mifugo Igunga ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini baada ya mnada wa Pugu, Dar es Salaam.
"Hospital hii ujenzi wake ulisimama kwa miaka 10 toka 2012-2022 hadi Rais Samia alipoidhinisha fedha kuijenga na kuweka vifaa vya kisasa,Mama Samia halali kuhakikisha anawaletea watanzania maendeleo kwa kuwa ndio kipaumbele chake cha msingi katika kuwatumikia watanzania” Shaka
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Shaka H.Shaka amesema Rais Samia Suluhu Hassan katika suala la maendeleo ya nchi ni kama Kurwa na Doto.Amesema hayo leo katika wilaya ya Kaliua baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya Mwongozo katika kijiji cha Mwongozo ziara Mkoani Tabora.
"awali kulikuwa na malalamiko mengi kuhusiasa na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambapo Chama kililazimka kukaa pamoja na Serikali (Bodi ya Mokopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu) (HESLB) ambapo kwa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa na hali imeimarika"Shaka H.Shaka
“Maboresho makubwa yamefanywa katika sekta ya elimu,nimetembelea mabanda ya taasisi mbalimbali za elimu zinazoshiriki maonyesho haya, nimejionea na kusikia mambo makubwa ya maendeleo na kuona jinsi Rais Samia alivyopania kuleta mageuzi makubwa katika nyanja ya elimu”Shaka H Shaka
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu, unaendelea kutoa matunda mazuri katika sekta hiyo na chama kinaridhishwa sana
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Abdulrahman Kinana amesaini kitabu cha maombolezo tarehe 12 Julai, 2022 katika Ubalozi wa Angola Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Komredi José Eduardo dos Santos, kilichotokea Ijumaa, Julai 8, 2022. nchini Hispania
”CCM kitamkumbuka Bi Chuma kwa mchango wake mkubwa katika kutetea utaifa wetu kwa kudumisha utamaduni, mila, silka na desturi zetu hasa katika kuelimisha, kuhamasisha, kuburudisha na kulea rika zote kupitia semi, tungo na ujumbe maridhiwa katika nyakati tofauti”Ndg.Shaka H.Shaka