Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Katibu wa Tume ya Watumishi wa Umma, Jacob Kipanda kutoa maamuzi kwa misingi ya haki, akisema bado kuna Watumishi wanaohukumiwa kwa chuki na kupewa adhabu zisizoendana na makosa yao.
Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 1, 2026, Ikulu jijini Dar es salaam, wakati akimuapisha Kipanda pamoja na viongozi wengine wawili. Amesema Tume ya Watumishi wa Umma ina jukumu kubwa la kushughulikia mashauri ya Watumishi, yakiwemo malalamiko na migogoro, hivyo ni muhimu kuhakikisha haki inatendeka wakati wote.
“Huku kuna kazi kidogo kuna malalamiko, migogoro, uadilifu na hakikisha tume yako inasimamia haki, simamia tume iondoshe malalamiko kwa watumishi”
“Pia migogoro ndani ya taasisi zetu kuna mambo mengi, Mtumishi anaweza akahukumiwa kwa chuki tu, kwa tatizo dogo lakini akapewa hukumu kubwa,” amesema Rais Samia.
#MillardAyoUPDATES
"Nimeona kwenye mitandao ya kijamii wanachama na mashabiki wa Young Africans wakituomba na kutushauri viongozi tutengeneze mkeka wa kuchangia matibabu ya Pacome Zouzoua. Ni jambo zuri, lakini nichukue fursa hii kuwaambia [...] matibabu ya Pacome Zouzoua yamegharamiwa na uongozi wa klabu." - Ally Kamwe, Afisa Habari Yanga SC
Ninaungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuipongeza Klabu ya Yanga kwa ushindi wa leo na kutwaa Ubingwa wa Kombe la Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo. Ninawapongeza Wachezaji, Benchi la Ufundi la Klabu ya Yanga na kwa timu zote zilizoshiriki mashindano haya.
Hongera pia kwa timu za Simba SC , Azam FC na Singida BS SC zitakazoungana na Yanga SC katika kuiwakilisha nchi kimataifa msimu ujao wa mashindano.
Michezo ni furaha na amani.
*Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi*
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
DODOMA: Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju ameyasema hayo Juni 30, 2026 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Madalali wa Mahakama.
Zaidi tembelea https://t.co/nW0OJZTzB3
#JamiiForums#Utawala#Uwajibikaji
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Hamza kutoka Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Mtandao, leo Julai 1, 2026, ametoa elimu kwa watoto waliotembelea banda la Jeshi la Polisi Tanzania
https://t.co/rzMFAdNNDV
#VIDEO: Msemaji wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema timu hiyo haina cha kujilaumu baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu, akieleza kuwa maandalizi yao yalikuwa mazuri licha ya mwanzo wa msimu kusuasua.
Akizungumza baada ya Simba kuifunga KMC FC bao 1-0, Ahmed alisema timu ilirekebisha mwenendo wake baadaye, lakini matokeo ya mwisho hayakuwa upande wao na hakuna wa kulaumiwa ndani ya kikosi.
#MzawaUPDSTES
Ni Imani yetu maelezo haya ya Dkt. Murete Sanare Lukumay, Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi na Mganga Mkuu wa Ekenywa Specialised Hospital aliyoyazungumza kupitia BONGO FM yatakusaidia kujua madhara ya 'UTI' kwa Mama wajawazito.
Beki wa kati wa JKT Tanzania 🇹🇿 Hassan Wahabi akiongozana na uongozi wake wamemtembelea hospitali kiungo wa Young Africans 🇹🇿 Pacöme Zouzoua 🇨🇮 aliyepata majeraha hapo jana.
Wahabi ameomba msamaha kwa Pacome, Young Africans, mamlaka za soka na wana michezo kwa ujumla.
Mchezaji wa JKT Tanzania, Hassan Wahabi, amemtembelea hospitalini kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua, aliyepata jeraha baada ya kugongana naye katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu.
Wahabi ameambatana na baadhi ya viongozi wa JKT Tanzania.
Shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu (FIFA) limemfungia mechi tano kiungo wa Qatar, Assim Madibo, kufuatia rafu iliyosababisha kiungo wa Canada, Ismaël Koné, kuvunjika mguu katika mechi ya Kundi B ya Kombe la Dunia.
Madibo alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea rafu kutoka nyuma Koné katika kipindi cha pili cha mchezo ambao Canada ilishinda Qatar mabao 6-0 mjini Vancouver.
Kamati ya Nidhamu ya FIFA ilisema adhabu hiyo imetolewa kutokana na kosa la uchezaji hatari, huku ikieleza kuwa uamuzi huo bado unaweza kukatiwa rufaa.
Mchezaji huyo alivunjika mifupa ya tibia na fibula katika mguu wake wa kushoto na alifanyiwa upasuaji baada ya kuondolewa uwanjani kwa machela.
Mifupa ya Tibia na fibula ni mifupa miwili mikubwa ya sehemu ya chini ya mguu kati ya goti na kifundo cha mguu.
Tukio hilo liliwashtua wachezaji na mashabiki, na kusababisha mchezo kusimamishwa kwa muda huku wahudumu wa afya wakimhudumia Koné.
Baada ya tukio hilo, Madibo alionekana kusikitishwa na kilichotokea na baadaye alimtembelea Koné hospitalini akiwa ameambatana na Waziri wa Michezo wa Qatar, katika ishara ya uungwana na mshikamano wa kimichezo.
#KitengeSports
Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania Himid Mao Mkami amesaini nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia klabu ya Azam FC mpaka mwaka 2027.
Azam FC imethibitisha kumsainisha kiungo huyo nyongeza wa mkataba mpya baada ya kuonesha kiwango bora tangu arejee klabuni hapo akitokea Ghazl El Mahalla mnamo Julai 2025.
#KitengeSports
@mkainerugaba#HABARI Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakari Zubeir Ally, amemuomba Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili mapumziko ya Mwaka Mpya wa Kiislamu yawe yanatambuliwa nchini kote badala ya Zanzibar pekee.
Mufti Zubeir alitoa ombi hilo leo Juni 15, 2026, wakati wa mwendelezo wa Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu visiwani Zanzibar.
Alisema kuwa Tanzania ni nchi moja, hivyo ni vyema mapumziko hayo yakatolewa kwa wananchi wote ili kuwawezesha Waislamu kuadhimisha siku hiyo muhimu ya kidini.
Ombi hilo limekuja baada ya Rais Dkt. Mwinyi kutangaza kuwa Juni 17, 2026 itakuwa siku ya mapumziko rasmi Zanzibar kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1448 Hijria.
Mufti alimpongeza Rais Mwinyi kwa hatua hiyo na kueleza matumaini yake kuwa utaratibu huo unaweza kupanuliwa hadi Tanzania Bara.
#EastAfricaTV
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa imesema katika kipindi cha Julai, 2025 hadi Machi 2026, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ilihudumia jumla ya tani milioni 29.66 za shehena, ikilinganishwa na tani milioni 23.18 katika kipindi kama hicho mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 27.96.
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Filbert Philimon (23), mwanachuo wa Chuo Kikuu cha St. John's kwa tuhuma za kuchoma chumba moto na kusababisha vifo vya watu wawili, Rebecca James na Felister Peter katika Mtaa wa Kikuyu, Juni 7, 2026.
Polisi wamesema mtuhumiwa alikamatwa katika Stendi ya Mabasi ya Magufuli, Dar es Salaam akiwa katika harakati za kutoroka, na baada ya mahojiano alikiri kutenda kosa hilo baada ya kuachwa na mpenzi wake, Felister.