Anaandika Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, @Dr_DGwajima
Mabinti nisikilizeni:
Iwapo hujajiandaa binafsi kukabiliana na maisha ya dunia hii ya kizazi cha leo halafu unajiamulia mwenyewe kuwa bize kujiandaa kusaka mwanaume mmoja hivi ushirikiane naye kuijaza na kuiongeza dunia hii ya leo hebu amua kunipa masikio yako kwamba;
Kupitia uzoefu wangu wa kupokea taarifa za migogoro ya mahusiano ya kike na kiume, sehemu kubwa zaidi ya 90% ni taarifa za vilio vya wanawake vyenye hoja za kanitelekeza na watoto, haleti matumizi, analeta hela kidogo hadi umfuatilie sana, aliniachisha shule kaniharibia maisha nk
Binafsi huwa naanza kujiuliza, je sisi walalamikaji kwani inakuwa sisi tulijiaandaaje kwenda kukutana na yaliyomo kwenye ajenda tunayoikubali? Na kwa nini tuliacha shule jamani? Hivi tunakuwa tulipatana na mpenzi kwa mapenzi au tulipatana na money downloading machine?
Hivyo, kwa wema tu tukumbushane kuwa, ama tujiandae kwanza na maisha au tujiandae vema kulia machozi mengi tusipate wa kuyafuta kwa ninavyokiona hiki kizazi cha dunia ya leo.
Haya, msinipopoe mawe mimi nawashauri tu.
Rais wa Singapore, Tharman Shanmugaratnam anatarajiwa kufanya ziara ya kitaifa ya siku tatu Tanzania kuanzia Juni 8 hadi 10, 2026 kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan.
Rais Shanmugaratnam anakuwa Rais wa kwanza wa Singapore kutembelea nchini tangu kuanzishwa ushirikiano wa kidiplomasia mwaka 1980.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mfanyabiashara kutoka nchini Nigeria ambaye pia ni Mwanzilishi na Mmiliki wa Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote pamoja na Ujumbe wake, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Mei, 2026
Martin maranja masese @IAMartin_ ni mtetezi wa haki za binadamu na mchambuzi wa siasa mwenye ushawishi mkubwa katika mijadala ya kijamii hasa kupitia mitandao ya kijamii
Alianza maisha yake ya kazi kama mwalimu kisha akaamua kuacha ajira ya serikali na kujikita katika shughuli huru za kijamii na kitaaluma akilenga zaidi kuelimisha jamii kuhusu haki za binadamu, uwajibikaji na utawala bora
Umaarufu wake umejengwa juu ya uwezo wake wa kipekee wa:
1:kuchambua masuala ya kisiasa kwa kina na kwa mantiki
2:kuunganisha sheria, historia na uhalisia wa kijamii katika hoja zake
3:kuelimisha vijana kuhusu haki zao na wajibu wao katika jamii
4:kuhimiza uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi
Kupitia mitandao ya kijamii hasa X/Twitter amekuwa chanzo cha mijadala yenye manufaa kwa jamii akisaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu demokrasia, haki za binadamu na masuala ya utawala
Katika safari yake amekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo shinikizo la kijamii na kuitwa na vyombo vya dola kutokana na msimamo wake wa wazi lakini hali hiyo haijamzuia kuendelea kusimamia anachoamini
Mpaka sasa anaendelea kutambulika kama mmoja wa sauti muhimu zinazochangia uelewa wa haki za binadamu, uwajibikaji wa viongozi na maendeleo ya fikra za kisiasa miongoni mwa vijana Tanzania
Gen Z si adui; Ni wateja wa siasa na uchumi wa kesho.
Making Africa Work: A Handbook (waandishi ni Greg Mills, Jeffrey Herbst, Olusegun Obasanjo, na Dickie Davis). Kitabu kinasisitiza kuwa Afrika inapitia ongezeko kubwa la watu kuliko bara lingine lolote.
Mmoja wa waandishi, Olusegun Obasanjo (Rais wa zamani wa Nigeria), ameandika kwamba “Making Africa Work” kunahitaji uongozi wenye maono ya mbali sana, siyo uongozi wa kuzima moto wa maandamano.
Idadi ya watu itaongezeka mara mbili hadi kufikia bilioni 2 ifikapo mwaka 2045. Zaidi ya nusu ya Waafrika wataishi mijini. Kundi hili litakuwa na vijana ambao wanaunganishwa kupitia simu na mitandao ya kijamii.
Hadi kufikia 2050, robo ya idadi ya watu duniani itakuwa Afrika. Ongezeko linaweza kuwa baraka ikiwa vijana watapata kazi na elimu, au likawa janga ikiwa serikali zitashindwa kuweka mifumo ya kiuchumi
Kitabu kinaeleza; Ikiwa (Gen Z) watapewa fursa za kiuchumi, watakuwa nguvu ya mabadiliko na ukuaji (demographic dividend). Lakini ikiwa hakuna ajira, uchumi na fursa, itakuwa janga la kisiasa na kijamii.
Waandishi wa “Making Africa Work” wanaeleza kuwa (Gen Z) wanaishi mijini zaidi na wameunganishwa na mtandao (digital connectivity). Tofauti na vizazi vilivyopita ambavyo vilikuwa vijijini na vilitawanyika
Gen Z siyo Taasisi iliyosajiliwa, ni wazo (Idea). Tofauti na vyama vya siasa ambavyo vina ofisi, viongozi wa kukamatwa, ruzuku za kuzuia, Gen Z ni kizazi chenye itikadi inayozungumza haki, ukweli, na teknolojia.
Gen Z Hawana “central command”. Wao wanakutana ‘online’ tu. Ukimkamata mmoja, wengine elfu kumi wanazaliwa mtandaoni. Huwezi kuua wazo lao ambalo halina ofisi wala msemaji mkuu mmoja. Never.
Gen Z hawana kiongozi mmoja (leaderless movement), hivyo hakuna mtu mmoja wa kumnyamazisha ili harakati zao zifariki. Decentralization haitawezekana kamwe katika Ulimwengu huu wa sasa wa kidijitali.
Habari inasafiri kwa sekunde. Ukijaribu kufunika ukweli mmoja, video 100 zinatokea TikTok au X (Twitter) au Instagram au Facebook. Information speed ni kubwa sana. Huwezi kutengeneza uongo na kuutea uongo.
Usiwaone Gen Z kama adui, waone kama mtaji katika uwekezaji wa baadaye; Wanaishi katika ulimwengu tofauti na vizazi vilivyotangulia. Wao wanafikiria digital, wanataka uwazi, haki, na fursa za kiuchumi.
Huwezi kufungia “spirit” ya watu wanaozungumza lugha moja kupitia mitandao. Washauri wa watawala wanatumia mbinu za karne ya 20 (mabavu, propaganda, na vitisho) kukabiliana na matatizo ya karne ya 21.
Mtawala anayewaona vijana kama maadui anajitenga na uhalisia. Badala ya kutumia nguvu (force), alipaswa kutumia ushawishi (influence). Vijana hawataki kupindua nchi; wanataka nchi ifanye kazi kwa ajili yao.
Kitabu hiki kimeweka msisitizo mkubwa kwamba, Viongozi wanaotaka kuendelea kubaki madarakani lazima waendelee na ukuaji wa kiuchumi wa kweli na kuunda ajira — si kupambana na raia wao wenyewe.
Fanyeni tafiti (research) halisi, si hizi tafiti zenu za uongo za kufurahisha genge; Washauri wa watawala huwaeleza watawala lugha ambayo wanadhani wanayotakiwa kusikia. Hawaelezi ukweli na uhalisia.
Mnatakiwa kutumia data halisi, surveys zisizopendelea upande, na mazungumzo ya moja kwa moja na vijana (bila kuwakamata au kuwatisha). Kuujificha nyuma ya “wanasiasa wana wachochea” ni kukimbia ukweli.
Kitabu kinakataa mifumo ya kufadhiliwa na rushwa (patronage) na kuendesha mambo tu bila mpango (muddling through). Kinasisitiza kuwa ongezeko hili la watu linafanya mifumo ya zamani isifanye kazi tena.
Kitabu hiki kimeandika kwamba, ulinzi wa kweli hautokani na silaha, bali unatokana na raia walioridhika. Kupambana na “Gen Z” ni sawa na kupambana na injini ya gari lako mwenyewe ukiwa barabarani.
Unapochagua mabavu dhidi ya raia wako, unajenga Deep-seated Resentment. Hiki ndicho kizazi chenye nguvu kazi, wabunifu, na walaji wa kesho. Ukiwavunja moyo, unaharibu uchumi wa nchi muda mrefu.
Ukiziba njia zote za kidemokrasia na mazungumzo, unawalazimisha kutafuta njia mbadala ambazo mara nyingi huwa ni za machafuko zaidi. Hapa ndipo inaibuka dhana ya ‘Radicalization’ ili wapate kupumua vizuri.
Kitabu kinaeleza huwezi kuwadhibiti watu ambao wanajua haki zao na wanaona maendeleo ya nchi zingine kwa kutumia mabavu. Gen Z hawawezi kufungwa macho kirahisi. Ulimwengu upo kiganjani.
Badala ya kupambana nao, waweke katika meza ya mazungumzo. Washirikishe katika maamuzi badala ya kuwafanyia maamuzi. Wana maoni makali kwa sababu wanaona matatizo moja kwa moja kupitia mitandao.
Kiongozi unatakiwa kujenga uaminifu mkubwa kupitia vitendo, si maneno; Punguza gharama za maisha kwa vitendo. Pambana na ufisadi bila kuchagua. Toa fursa za kiuchumi kwa vijana (ajira, mikopo, elimu bora).
Tumia mitandao kuwajibu moja kwa moja, si kuwazima ili sauti zao zisikike tena. Msiifungue hiyo mitandao. Msiifanye kama ni majukwaa haramu kuyatumia. Tumia lugha yao kupitia mitandao, memes, na uwazi.
Usiwaone Gen Z kama watu kutoka nje — ndiyo wapiga kura wengi wa baadaye. Miaka mitano ijayo, hawa walio na umri wa miaka 15 had 18 watakuwa na miaka 20 hadi 23 na ndiyo watakuwa wapiga kura wenu wengi.
Watawala mnatakiwa kuanza kufanya town halls za kidijitali na za kimwili (physical) bila kuwakamata. Wajenge uwezo — elimu bora, stadi za tech, na nafasi katika uongozi (youth quotas bunge na serikali).
Tumia Youth Councils na hizi Youth Development Forum ili kupata malalamiko ya vijana. Tumieni data halisi (si kutegemea taarifa za intelligence tu) kuelewa malalamiko halisi ya gharama ya maisha na ajira.
Kitabu kinatoa takwimu Afrika inahitaji kutengeneza mamilioni ya ajira kila mwaka ili kukidhi hitaji la vijana wanaoingia sokoni. Serikali lazima zifanye mageuzi makubwa sana ya kiuchumi (economic reforms).
Toeni mikopo ya vijana (kama SIDO au TIB) bila siasa, anzisheni digital hubs katika mikoa. Tengenezeni National Youth Dialogue Forum na hakikisheni isifanywe kuwa jukwaa la kisiasa la vijana wa mbogamboga.
Vijana si kikwazo, ni kipimo cha uongozi wako; Kiongozi mkubwa si yule anayeshindana na vijana, bali yule anayewaelewa na kuwaongoza kuelekea mustakabali bora. Gen Z wataendelea kukua na kuwa wengi zaidi.
Usipambane na kizazi chako. Kipambane na matatizo yanayowatesa. Kama utawaelewa na kuwahudumia, watakufanya uwe na urithi mkubwa. Kama utawapuuza au kuwapiga, watakuandika kama sehemu ya tatizo.
Kitabu kinathibitisha suluhisho la Afrika siyo bunduki, bali ni sera sahihi, utawala bora, na kutoa nafasi kwa Gen Z kuongoza mabadiliko ya kiuchumi. Mtawala anayewazuia, anazuia maendeleo ya nchi yake.
Watawala someni kitabu, mtaelewa Afrika iko njiapanda. Upande mmoja ni mafanikio makubwa kupitia nguvu ya vijana, na upande mwingine ni machafuko ya kudumu ikiwa mahitaji ya vijana ya kudumu yatapuuzwa.
Huwezi kushinda vita dhidi ya wakati. New generation (hawa ambao tunawaita Generation Z) ni wakati unaokuja, na kamwe, huwezi kuuzuia jua lisioneke kwa kutumia kiganja cha mkono. Msiwachukie Gen Z.
Mimi nimeshauri tu kama mwananchi wa kawaida, mkitaka chukueni ushauri, msipotaka acheni.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
“Much love, my friend—I miss you deeply. You are still one of the finest brains this country has. I’m keeping you in my prayers—may God give you the courage, strength, and resilience to rise above every challenge before you.”
Kama utaitafsiri Ndoa (Familia) kama source ya starehe basi hilo sio eneo sahihi kwako..
Kama utatafuta Mwanamke kwa ajili ya kuongeza burudani kwenye maisha yako basi hauna miezi 6 kabla ya kujajutia maamuzi yako ya kuoa...
Familia kwa Mwanaume ni Jukumu ambalo kama utalitekeleza kwa usahihi basi matokeo yake ni amani ya moyo..
Familia ni ndio kundi pekee ambalo kila kitu kikienda mrana unaweza kuwaambia niombeeni na moyo wako ukapata amani.
Ukipata nafasi ya kuoa kama una akili timamu fanya maamuzi hayo haraka sana. Familia ni tunu, Familia ni faraja na ni baraka sana... 🧎🏽♂️🙏🏽
Naomba Retweet Yako mkali.🙏
Hizi ni 2x3 Grade 1 zimenyooka kama Rulaaa...Zina Urefu wa Average Futi 16.
-Hizi zinatoka Kwa 6,500(inapungua)
📍 Rombo Tarakea.
Call/WhatsApp +255756946965
Zaburi 23:6 🙏
VIDEO:
Ni siku moja tangu Jambo TV ilipochapisha habari kuhusu hali ya maisha ya Bibi Janeth Yohana (56), mkazi wa mtaa wa Ngo’ngona Jijini Dodoma, ambaye amebeba jukumu zito la malezi ya wajukuu wake wawili baada ya kumpoteza mtoto wake wa kike aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kujifungua kutokana na changamoto za mshono.
Mara baada ya kuchapishwa kwa habari hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Doroth Gwajima, alitoa maelekezo kwa maafisa kutoka wizara hiyo kufika nyumbani kwa bibi huyo kwa lengo la kumpatia msaada wa haraka.
Akizungumza na Jambo TV leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Bibi Janeth amewashukuru Watanzania pamoja na Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa kufanikisha matibabu ya mjukuu wake na kuonesha mshikamano katika kipindi kigumu anachopitia.
Aidha, baadhi ya wananchi wa mtaa wa Ngo’ngona wamefanikisha kumnunulia bibi huyo kiwanja kwa ajili ya kupata makazi ya kudumu yeye pamoja na wajukuu wake. Hata hivyo, Bibi Janeth amewaomba tena Watanzania pamoja na Serikali kumsaidia ujenzi ili aweze kupata angalau chumba kimoja cha kuishi katika kiwanja hicho.
Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa mtaa wa Ngo'ngo'na, Venance Moses amesema licha ya baadhi ya watu kujitoa katika kununua kiwanja hicho, bibi huyo bado hana uwezo wa kifedha katika kujenga makazi yake ya kudumu hivyo amewaomba wadau mbalimbali kujitoa tena walau bibi huyo apate chumba kimoja kwa ajili ya kuishi.
Aidha, kwa yeyote anayeguswa kuendelea kumsaidia bibi huyo anaweza kutuma mchango wako kupitia namba ya simu 0650 938 253.
Humphrey Polepole, Mzaliwa wa Tabora aliye kulia na kusoma Dar es Salaam, na Arusha.
Mtoto wa fundi magari na mama wa nyumbani. Watekaji wameamua kukuteka. Muachieni Polepole!
Watengeneza Content wa YouTube Uingereza wamechangia Tsh Trilioni 7.3 kwenye Uchumi wa Uingereza 2024 na wamewezesha ajira 45,000. Tena sasa hivi wanazidi kuwasiliana na bunge lao ili waboreshewe sera wazidi kufanya biashara. Dunia ya sasa sio ya kufunga mitandao ya jamii
OXFORD, here I come🥳😭🎓
I’m thrilled to share that I’ve been admitted to my dream @UniofOxford , to pursue a Master of Science in Nature, Society and Environmental Governance, fully funded through the prestigious WHT scholarship in Oxford📚
Dear girl child, it can be done!🥳
Rwanda wana sera ya taifa ya Artificial Intelligence tangu 2023, Kenya wana Mpango wa taifa wa AI na vyuo vyao tayari vinatoa degree za AI. Nchi nyingi za Afrika zinakimbizana na mabadiliko makubwa ya Teknolojia yanayoendelea duniani na hazitaki kuachwa nyuma hata kidogo
Tundu Antipas Mugway Lissu siyo wakili tuu anayejua kuongea na kupanga hoja.
Kwasanaa ya sheria watu wa namna hii huwa tunawaita "Legal Maneac" ni watu wenye ueledi wa kina na ubobevu ambao huwezi kuupata Darasani... NI CHUO KIKUU CHA HIYARI CHA TAFAKURI ZA KISHERIA.
BAK Mwabukusi.