Uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023 sasa ni tarehe 01, Februari 2025.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu mabadiliko ya tarehe ya hafla ya uzinduzi wa Sera mpya ya Elimu.
Kwaheri, Jenerali.
Ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Makamanda, wapiganaji wastaafu, wapiganaji walio katika utumishi, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa kuondokewa na shujaa wetu, mpendwa wetu, mwalimu, mshauri na kiongozi wetu, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Musuguri.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha yake ya miaka 104, ambapo miaka 46 kati ya hiyo ameitumikia nchi yetu kwa weledi, umahiri, kujituma, ushujaa, nidhamu na kwa mafanikio ya hali ya juu, akiishi kiapo chake cha kuwa tayari kuutoa uhai wake ajili ya ulinzi wa Taifa letu. Ametuachia mfano bora wa utumishi wa umma utakaoendelea kuwa mwanga ndani na nje ya Majeshi yetu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Amina.
Nawatakia kila la kheri wanafunzi 1,230,780 wa Darasa la Saba mlioanza Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi leo. Mnatoka hatua moja ya elimu na malezi kwenda nyingine katika safari yenu ya kujiandaa kutoa mchango wenu wa maendeleo kwa Taifa letu. Serikali imeandaa mazingira sahihi ili muweze kufikia lengo hili.
Ahadi yangu kwenu katika safari yenu ya elimu na maisha ambayo tayari inatekelezwa ni; nafasi katika shule kwa kila atakayefaulu kuingia Kidato cha Kwanza 2025, miaka minne ya sekondari ya awali bila ada, miaka miwili ya Kidato cha Tano na Sita bila ada, Chuo cha Ufundi katika kila Wilaya kwa mtakaochagua njia hii na mikopo ya Elimu ya Juu kwa mtakaofaulu kwenda Vyuo Vikuu.
Kazi hii inakwenda sambamba na kuendelea kuboresha sera za uchumi wetu ili uweze kuzalisha fursa zaidi kwa kila mmoja wenu kadiri mnavyoendelea kukua na kuingia katika nguvu kazi.
Mwenyezi Mungu awaongoze.
Ngasere High Class tunatoa shukrani za dhati kwa wanafamilia wetu wote waliowezesha ushindi wa tuzo hii muhimu, kwa kutupigia kura na kuhakikisha tuzo hii inabaki nyumbani. Hakika huu ni ushindi mihimu kwetu na tuna ahidi kuboresha huduma zetu na kuwa za viwango vya juu zaidi.
Mojawapo ya njia nzuri zaidi kwa taifa letu kuwalinda watoto na kujihakikishia kesho njema ya nchi yetu ni kuwapa fursa ya kupata elimu na malezi kimaadili na kiakili toka ngazi ya chini kabisa. Hili ni jukumu la Serikali na kila Mtanzania; kushiriki katika elimu na malezi ya watoto wa taifa letu. Tunajivunia maendeleo makubwa kwenye eneo hili tukiwa moja ya nchi vinara kwa Bara letu la Afrika, ambapo pamoja na mambo mengine tumejenga shule za awali karibu katika kila Shule ya Msingi nchini.
Mapema leo nikiwa na baadhi ya watoto wa Shehia ya Tasani, Makunduchi, Kusini Unguja, Zanzibar baada ya Ufunguzi wa Skuli ya Maandalizi Tasani. Ufunguzi huu ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi linalogusa uchumi, utamaduni, mafunzo ya ujasiriamali hasa kwa vijana pamoja na shughuli za kijamii.
Je wajua
Ujugu wa Ujugu Arena hakuwahi kufikiria kabisa kama ubao wake wa mechi unaweza ukawa na wadhamini wa makampuni mbalimbali ya biashara alikua anajiandikia kuvutia biashara yake
Na lengo la kupost mitandaon ilikua kupata wateja wa mbali zaidi sio wa palepale mtaani kwake
Hadi alipo pigiwa cm na kampuni ya ASAS kwa mara ya kwanza
Na mkataba wake na ASAS ni wa milele Amina 😂
#ElimikaWikiendi UjuguHapa
Nimefurahi kukutana na mmoja wa waliokuwa waalimu wangu nikiwa mwanafunzi wa IDM Mzumbe (sasa Chuo Kikuu Mzumbe) kuanzia mwaka 1983 hadi 1986 Mama Sabina Gellejah, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Majengo ya Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu Mzumbe.
Imekuwa siku njema ya kazi katika Wilaya za Gairo na Kilosa mkoani Mogorogoro ambapo pamoja na mambo mengine nimezindua rasmi matumizi ya Hospitali ya Wilaya ya Gairo, Daraja la Berega [kuunganisha Kilosa, Gairo, Kiteto na Kilindi] na kuzungumza na wananchi.
Faraja kubwa kuona namna miradi ya maendeleo wilayani inavyosaidia kubadili maisha ya wananchi wetu.
Katika kazi mkoani Rukwa mapema leo, baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Shule ya Sayansi ya Wasichana Mkoa wa Rukwa.
Tunajenga shule hizi maalumu kwa mabinti zetu wanasayansi wajao wa nchi yetu katika mikoa 26 ya Tanzania Bara, na kila moja itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000. Wito wangu kwa mabinti zetu kila kona ya nchi yetu ni kutumia fursa hizi kujijenga kwa ajili ya maisha yao na nchi yetu siku zijazo.