Utawala dhalimu wa damu, mmeua maelfu ya watu kujitangaza bila ridhaa ya umma..
Mmeteka na Mnateka watu ili kuwajaza watu hofu..
Mnawategea wengine sumu ili kuwaua na kumaliza kila anaewakosoa..
Ushirika wa kidhalimu huwa haudumu, hakuna mwenye unafuu miongoni mwenu…
Wote mmekalia viti vya damu na vyeo vya uongo…
Damu ya Watanzania itaendelea kuwanenea kila baya nyie na familia zenu.
Ni muhimu mmeanza kumalizana, kama boss anaweza kutuma mtu kuita msaidizi wake majina (YUDA)
Watanzania tutashinda vita hii, hakuna mwenye nafuu ccm wote ni walewale.
Mwigulu unasemaje sasa kuhusu hili? Anaehujumu serikali ni nani?
Serikali dhalimu hii iliyojaaa damu, inatesa mamilioni ya Watanzania kuanzia Mtwara mpaka Tarime toka Tarime mpaka Kigoma kutoka Kigoma mpaka Songea, Tunduma mpka Dar..
Kila kona ya Nchi hii watu wanalia kama sio kubambikiziwa kesi na polisi, ndugu zao wametekwa au wameuwawa na vyombo vya dola .
Huyu mama anahitaji kulipwa nini ili aandamane kudai haki ya mtoto wake kutekwa.
Watoto wa huyo kijana au wa Soka, Mdude au polepole, watoto wa Chonchoryo au Sinda, watoto wa Tall au Kipanya wakikua wataacha watoto wenu waishi kwa Amani?
Mnajenga sumu ya hatari mno kwenye mioyo ya Watanzania, bahati mbaya nashindwa kuona tatizo hili na kulitatua bado mnatumia ubabe na kiburi…
Fikiria huyo angekua mama yako!
Utaratibu wa polisi kukamata watu upo kisheria. Kwanini polisi wanateka Watanzania?
Kila mtu ambae mtoto wake au ndugu yake amechukuliwa story zinafanana kwamba watekaji walijitambulisha kwamba wao ni polisi.
Jambo kubwa kama hili, Watuhumiwa ni polisi alafu unasema polisi ndio wafuatilie!hivi mnawaonaje Watanzania?
Watanzania hawatakubali kuishi kwa hofu kwasababu ya kagenge kadogo ka wauaji na wanyonya damu.
Rais wa Marekani, Donald Trump, amemkosoa na kumshambulia kwa maneno makali Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV akisema ni Papa dhaifu kwenye kushughulikia masuala ya uhalifu na ambaye hayupo vizuri kwenye kushughulikia Sera za Kigeni huku akisema anamshangaa kuona Papa Leo anaona ni sawa Iran kuwa na silaha za Nyuklia na amekiri kuwa yeye Trump sio Shabiki wa Papa Leo na haoni kama anafanya kazi nzuri.
Trump ametoa maneno hayo makali kupitia mtandao wa Truth Social ambapo ameandika “Papa Leo ni dhaifu katika suala la kukemea uhalifu na ni mbaya sana katika kushughulikia Sera za Kigeni, anaongelea hofu ya Utawala wa Trump lakini hataji hata kidogo hofu ambayo Kanisa Katoliki na Mashirika mengine yote ya Kikristo yalipata wakati wa COVID wakati walipokuwa wakikamatwa Mapadri, Wahudumu na wengine wote kwa kufanya Ibada za Kanisa hata walipokuwa nje na walipokaa umbali wa futi kumi na hata ishirini.
“Mimi nampenda sana Kaka yake Louis zaidi kuliko yeye kwasababu Louis ni Shabiki wa MAGA (Make America Great Again) kabisa, yeye anaelewa na Leo haelewi, simtaki Papa ambaye anadhani ni sawa kwa Iran kuwa na silaha za Nyuklia, simtaki Papa ambaye anadhani ilikuwa vibaya Marekani kuishambulia Venezuela Nchi ambayo ilikuwa ikisafirisha na kuingiza dawa za kulevya kwa wingi mkubwa Nchini Marekani na mbaya zaidi ikiwatoa wafungwa wake wengi, wakiwemo wauaji, wauza dawa za kulevya, wauaji na kuwaingiza katika Nchi yetu, hatutaki Papa anayesema ni sawa kuwa na uhalifu duniani na hatutaki Papa anayeona ni sawa kuwa na silaha za Nyuklia” Ameandika Trump.
Pamoja na hayo, Papa Leo amekuwa akikosoa vita inayoendelea kati ya Marekani & Israel na Iran mara kadhaa na ameukosoa utawala wa Trump kwenye hatua za kushughulikia vita hiyo.
#MillardAyoUPDATES.
Mwaka jana tarehe 25/7 2025 nilikwenda kumtembelea Mh Bwege hospitalin, Taasisi ya Mifupa Moi.
Japo nimekaa na mh Bwege bungeni na kwenye kambi ya upinzani sikuwahi kuwa karibu nae kama kipindi hiki.
Katika kipindi hiki kifupi nilijifunza na kumjua mh Bwege kama.
1. Mtu anaeipenda Nchi yetu na watu wake kwa moyo wote. Katika hali ya ugonjwa aliokuwa nao, watu wengine huacha kabisa hata kufuatilia siasa, kukata tamaa na kuona hata mambo yakiharibika hayamhusu.
2. Mtu mwenye msimamo wa hali ya juu mno, kuna watu walijaribu kumpa msaada wa matibabu lakini kama vile wanaweka masharti, akawambia niko tayari kwa msaada ila siko tayari kuyumbisha msimamo wangu.
3. Mtu aliependa Mageuzi kwa dhati, hata kabla ya kwenda kumuona Hospitalin, alinipigia simu na kuonesha kuwa amefurahishwa sana na uongozi mpya wa Chama chetu chini ya Mwenyekiti wetu Lissu… na akasema ana imani kubwa na Mhe Lissu na atajiunga na chama kama ishara ya kumuunga mkono.
4. Wiki moja iliyopita alianza opareshini ya kusimika Chadema Kusini, katika hali yake ya ugonjwa. Alitoa gari lake bure na mafuta, akawapigia viongozi kule na kuwakabidhi kwa vijana wa Chadema waliokua wanaendesha oparesheni. Kwa wiki moja maelfu ya watu wamehama vyama vingine kule na kujiunga Chadema.
5. Alijua Siasa hasa ground, Spika wa zamani wa bunge la Marekani Thomas P. “Tip” O’Neill Jr, alipata kusema “all politics is local” Siasa ni mahalia, Ndio maana ukienda Tarime utazungumza kuhusu dhahabu na ukienda kusini utazungumza korosho… Bwege alijua sana Siasa mahalia .. ndio maana ni mbunge wa miaka 10 wa upinzani.
6. Aliipenda kusini kwa dhati, aliipigania na alipigania maendeleo ya kusini na kusini ilimpenda sana Bwege.
7. Mfuatiliaji na anaejua watu kwa majina na meneo wanayokaa, wakati wa watu kuhamia Chadema ananipa namba na kuniambia ongea na huyu, yuko Namangaya , ongea na huyu yuko Kivinje, baadae anafuatilia kuuliza kama umeongea nae.
Alijiunga na Chama chetu, tukasubiri mikutano ifunguliwe tumpokee kwa heshima aliyostahili.. Mungu amemchukua kabla ya hiyo azma yake kupokelewa mbele ya maelfu ya watu.
Pumzika kwa amani kaka gwiji wa siasa za kusini.
Mjadala wa GPA? GPA ni kwaajili yako. Sio kwaajili tu ya ajira ya BoT au big entities. Good score will open plenty of doors for you. Kama bado uko shule, tafadhali usicheze, faulu vizuri. Usisubiri upitwe na fursa kwakukosa sifa za kitaaluma. Mengine - bahati na kudra, ni ziada!
Nimeletewa habari sasa hivi ila i have not confirmed it yet so please take it with a grain of salt.
Mleta habari anasema kuwa huyu mtoto hajatekelezwa, anasema mtoto katokea Zanzibar ni mtoto wa ndugu ndani ya familia ya kimama, mama mtu ni binti mdogo wa Kiislam amezaa hajaolewa na walikuwa wanaficha ujauzito wa huyo binti.
CCM wako kwenye full campaign ya kumsafisha kimama kama muuwaji. Wanajaribu ku-soften up image yake.
Kuanzia sasa Watanzania mtarajie movie tupu za kumuonyesha kimama kama binadamu ili msahau aliwaua na kugoma kuwapa miili mzike.
Mwambieni Wastara arudi kitandani haraka, safari hii pesa itatoka kubwa tu maana wauwaji wa CCM wako kwenye kampeni kubwa ya kusafisha image ya kimama.
Vimedia vya BONGO juzi vilikuwa bize kutuonyesha MAFURIKO ya NAIROBI leo vimeingia mitini vinaogopa “ITHIBATI”.
Maisha ya waandishi wa habari wa bongo ni kama “Nyani haoni KUNDU LAKE”.
Mwenye hii BAJAJI nitafutieni niipige full tank kisha aniambie malengo ya week kwa boss ngapi nayo nilipie.
Hiki alichofanya ninzaidi ya ushujaa. Pesa yangu ya ushindi wa treni la odds 83 zinanze kwenda kwa wanangu sasa.
NITAFUTIENI HUYU SHUJAA.
REPOST 200
WANU ana ABDUL sijui kama wangeweza kumshauri hivi mamayao sema mwanetu kawakilisha vema sana mtaa ila ajabu akili kama hizi zinapigwaga RISASI kule IKULU wapo akina BASHITE WANU RIDHIWANI watu wa mfanano kama huo ambao vichwa vyao wanavijua wenyewe����😅