Kutunza rekodi za miamala ni funguo ya kufanikiwa. Kama mfanyabiashara na mjasiliamali kutunza rekodi sahihi yasaidia katika kufanya maamuzi sahihi, kufuatilia maendeleo yako kiuchumi na kutambua nafasi za kukua. Ni msingi wa biashara yenye mafanikio.
#Entrepreneurs#Biashara
Tafsiri; “Hatua moja kwa wakati, haina sababu ya kuwahi."
Katika kila jambo ufanyalo, punguza papara ya kutaka kuwahi, fanya kwa hatua, kiumakini hatakama utamaliza wa mwisho. Ni bora kuchelewa kuliko kuharakisha alafu uharibu kazi.
#StepbyStep#Hatua#JordinSparks#MaarifaPrime
Tafsiri; " Elimu ni silaha yenye nguvu sana katika kubadilisha Dunia"
Kuelimika ndani na nje ya darasa, ni ufunguo tosha katika uelewa wa mtu. Husaidia kuboresha namna ya kutatua changamoto na kuboresha namna ya kuishi.
#education#powerful#weapons#NelsonMandela
Hakuna kazi pasipo mawasiliano, kuwa na uelewa mzuri wa kuzungumza na kuandika kwa lugha zaidi ya moja ni jambo bora na laweza mpa mtu nafasi ambazo hata hakutegemea katika sekta mbalimbali kimataifa. Endapo unapata nafasi ya kujifunza, itumie kwa busara, kwani inamsaada sana.
Tafsiri; Nakua Mtulivu, wakati wa Presha/Changamoto.
Kuwa mtulivu wakati wa Presha kunaletea faida nyingi. Inakuruhusu kufikiri kwa uwazi, kufanya maamuzi bora, na kuendelea kuwa thabiti katika hali ngumu.
Jali umuhimu wa kuwa Mtulivu na uone jinsi inavyokufanya Kua Mtu imara.
Tafsiri; Ningetamani kuwa na ujasiri wa kuishi maisha yanayolingana na nafsi yangu, siyo maisha yanayotarajiwa na wengine.
Ni vyema kutambua kua maisha ni mafupi na yakupita. Maranyingi tunataka kufanana na wengine na kuwafurahisha, tukisahau tunavyovitaka na hisia zetu.