Omba kwa imani, shukuru kwa ulichonacho, fanya kazi kwa bidii na uwe tayari kufuata mwongozo wa Mungu. Maombi si njia ya kumlazimisha Mungu kutimiza kila matamanio yetu, bali ni njia ya kumkaribia, kutafuta hekima yake na kumkabidhi maisha yetu.
Ameen 🙏🏼
Kutoka DM
Habari madam, samahani naomba unipostie hili kwa watu X nipate msaada. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27 Nina pambana changamoto ya colon cancer nilifanyiwa operation wa mwezi kumi mwaka Jana na nikabadilishiwa njia ya haja kubwa now natumia mifuko pembeni ya tumbo inaitwa Colostomy bag, naomba mni support niweze kumudu gharama za matibabu pamoja na hiyo mifuko kwa sababu hali imekuwa ngumu kwa sasa nashindwa kumudu gharama hizo.
Kwa sasa nahitaji sana msaada Naomba kuwezeshwa niweze kumudu gharama za matibabu, mpaka sasa nimefanya mizunguko mitano ya chemotherapy na sijahudhuria clinic miezi minne sasa kutokana na changamoto ya kifedha. Hospital wamenambia itabidi nianze mizunguko upya kutokana nilipitisha mda mrefu bila Dawa. Naombeni support yenu chochote mtakachojaaliwa niweze ku pambania afya yangu.
Na pia naomba msamaha kama nitaleta taharuki yoyote maana nimewatumia ujumbe huu watu kadhaa Dm wanisaidie kupost hivyo na wewe ni miongoni mwao dada samahani kama nitasababisha taharuki ni matatizo tu ndy maana nimewatumia watu tofauti tofauti naona kimya ndy maana natapatapa.
Namba yangu: 0786 594 753 kwa mawasiliano zaidi ili iweze kuifahamu vizuri hali yangu na Kuni support ahsante.
Usichoke kuwa mtu mwema.
Usikate tamaa kufanya yaliyo sahihi.
Na usisahau kwamba hata wewe unastahili kupokea upendo, msaada na furaha ambayo umekuwa ukiwapa wengine.
Kijana Mwenzangu Amka kumekucha.
Amka Ujaribu Tena leo ni siku yako,
Amka utengeneze Connection nyengine,
Amka utengeneze Networks nyengine
Wewe ni Bora sana ndio maana umepewa nafasi nyengine.
Uwe na Siku bora kuliko jana.