Xi Jinping wa China anaenda Korea Kaskazini kumtembelea Kim Jong Un kwa siku 2. Mara ya mwisho Xi kwenda Korea Kaskazini ilikuwa 2019, miaka 7 iliyopita. China na Korea Kaskazini zimepakana, tena zina makubaliano yenye miaka 65, kwamba mmoja wao akishambuliwa mwingine anaingilia
Hanan Jawad and Bakhita Al Mheiri wameweka historia ya kuwa wanawake wa kwanza wa Kiemirati kuwa marubani wa shirika la ndege la Emirates. Shirika hilo lenye miaka 40 lilikuwa halijawahi kuajiri rubani mwanamke ambaye ni raia wa UAE. Wote watarusha ndege aina ya Boeing 777
MNAMKUMBUKA DADA YETU
Dada Eliet (Neema) Rwechungura (22) wa Bukoba? Wazazi wake walifariki na kumuacha na umri wa miaka mitatu tu, ikabidi apelekwe Ifakara kulelewa na baba mdogo. Mwaka 2022 akiwa na miaka 18 mlezi wake alifariki, hivyo akalazimika kurudi Bukoba kwa bibi.
Akiwa Bukoba akapata kijana mmoja ambaye walianzisha mahusiano na wakahamia Shinyanga kuishi pamoja. Wakiwa Shinyanga Eliet alipata uvimbe mkubwa sana kwenye shavu ukaathiri hadi sehemu ya shingo. Yule kijana aliyekuwa akiishi naye akamkimbia.
Eliet akahangaika peke yake lakini hakuwa na fedha za kujitibia. Siku moja akiwa amejilaza chini, amekata tamaa pale hospitali ya mkoa Shinyanga, muuguzi mmoja akamuona na kumsikiliza. Akamsaidia fedha za kufanya vipimo.
Vipimo vikaonesha ana “Ameloblastoma” yaani uvimbe unaotokana na seli za “ameloblasts” kukua na kuharibu mfupa wa taya na kusababisha sura ya uso kubadilika.
Muuguzi huyo akamchukua Eliet na kuishi naye, maana baada ya kukimbiwa na mwanaume alikosa makazi. Hakuweza hata kulipa kodi ya pango. Daktari mmoja kwa kushirikiana na muuguzi huyo wakamsaidia kuratibu matibabu yake.
Akapewa rufaa kwenda Bugando lakini hakuwa na fedha. Na hapa ndipo @_ghfoundation iliposhirikiana na Watanzania kumchangia fedha za matibabu. Kwa umoja wetu tulimuwezesha kwenda Bugando na kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe na sehemu ya taya iliyoathirika (Wide local excision).
Kwa sasa anaendelea vizuri na kliniki. Taasisi ya @_ghfoundation imemkatia bima ili kumsaidia kwenye kliniki zake mpaka atakapopona kabisa.
Picha ya kwanza ni jinsi alivyo sasa hivi.
Shukrani kwa madaktari, wauguzi na watoa huduma wote wa hospitali ya @bugandomedical kwa kufanikisha upasuaji huu mkubwa na kuokoa maisha ya binti huyu.
Shukrani pia kwa madaktari, wauguzi na watoa huduma wa hospitali ya mkoa Shinyanga kwa kujitolea kubeba jambo hili kibinadamu. Wangeweza kumuacha tu akafa maana hakuwa na fedha za matibabu, lakini waliamua kulibeba kibinadamu nje ya misingi yao ya kitaaluma.
Shukrani pia kwa Watanzania wote ambao kupitia @_ghfoundation mlichangia matibabu ya binti huyu na kuokoa maisha yake. Sifa na Utukufu ni kwa Mungu 🙏🏽
Kila Asubuhi mpya ni ushahidi kwamba Mungu bado hajamalizana na wewe. Shukuru kwa uhai, ombea nguvu, na tembea kwa imani.
Neema ya Mungu ikutangulie leo 🙏🏼
BEIA YA MAFUTA IMESHUKA katika soko la Dunia sasa wakati wa Kupanda inapanda ghaflayaani ikipanda asubuhi mchana lazima huku tupewe kipenyo lakini cha ajabu sasa Imeshuka wameanza longo longo eti wanaangalizia kushuka zaidi yaani imeshuka kwa Asilimia 20?! halafu bei zisibadilike? Hii ni maajabu
Ni kweli wengine hatukusoma hesabu na ukokotoaji wa hesabu nisuala la kitaaluma tulikimbilia somo la Siasa but the number is not adding hapa tunapigwa.
Hivi hata hili Wabunge pale Dodoma nalo mnashindwa kuwalinda wananchi?
BAK MWABUKUSI.
Kuna wazee wenzetu huwa wanataka kutajirikia kwa mabinti zao wanataja mahari za kikenge sana. Yaani mahari ukijumlisha kila kitu inakuja milioni 9 yaani 9 kabisa? Nimemwambia dogo atafute mwanamke mwingine twende ila huko siendi 🚮🚮🚮
Maombi ya Kesi ya Mapitio ya DPP v. Tundu Antiphas Lissu yatasikilizwa mnamo tarehe 11 Juni 2026 na Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufaa (Mwarija, Muruke & Khamis) jijini Dar es Salaam.
The Revision Application by the DPP v. Tundu Antiphas Lissu at the Court of Appeal of Tanzania,arising out of the treason case against him at the High Court of Tanzania, will be heard on the 11th of June 2026 by a panel of three justices of appeal(Mwarija, Muruke, &Khamis) in Dar es Salaam.
Mnalazimisha mambo yawe magumu wakati ni marahisi sana.
Andaa thread moja fupi yenye details za kutosha marisiti na maushahidi kama yote, then fungua space watu watakuja, uwe tayari kujibu lolote. Atakaeshindwa kujibu kwa maandishi au kwa kusikika kwa maneno nae ni mhusika 😂
Taarifa: Ili kumuunga mkono Mwenyekiti wetu Lissu na struggles zake gerezani, nimeamua kumuiga style yake mpya ya nywele…Sitachana wala kunyoa nywele zangu mpaka atoke jela akiwa HURU✌🏾✌🏾
#LiMwenyekiti#KatibaMpya#FREELISSU
Hatimae nimerejea uraiani baada ya miezi 6 katika kuta za Gereza R/Bunda.
Mateso yote niliyopitia tangu 01/11/2025 - 22, Mei 2026 yamenipa nguvu ya mapambano zaidi.
Sasa basi ili kuiondoa CCM Madarakani lazima tuwe na Vijana Watundu, Vijana Wakorofi na Vijana wenye Hasira.
Katika siku hii tukufu ya Arafa, Ya Allah nakuinua jina la Danny kwako. Popote alipo, mzungushe na ulinzi wako, nuru yako, na rehema zako. Mlinde na kila aina ya madhara, mrahisishie mambo yake, na umrudishe salama nyumbani.
Ya Rab, tuunganishe naye tena kwa namna iliyo nzuri zaidi, tulize nyoyo zetu, na ubadilishe maumivu haya kuwa faraja na habari njema. Tuimarishe katika imani tunaposubiri, na ufanye siku hii iwe mwanzo wa kurejea kwake salama. Ameen