Nimetumiwa huu ujumbe usiku huu na mtu ambae katoka Central anasema kwamba amemwacha Frida Mikoroti lock up.
Najiuliza kwanini mpaka sasa Ofisi ya ZCO Mafwele inaendelea kusema kwamba hawajamkata wala hawamshikilii Frida lengo lao ni nini?
#FreeFridaMikoroti
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 6
Amemaliza Wakili wa Serikali Mrema
Naona Majaji wanajadili jambo kidogo hapa
Jaji Nduguru anasema kila upande una wajibu wa kuiambia mahakama sio useme navumilia.
Kama kuna jambo lilionekana mapema kuna lina shida ulipaswa kusema na sio kusema nilikuwa navumilia.
Naomba tuwe guided na sheria maana sheria iko hapo.
Wote tunajua kuwa tunabanwa na pleadings na pleading ni ile PO yenyewe.
Msemaji unakuwa kwenye jicho la unasema mambo mengi ambayo yako on face of records.
Anaendelea Mhe. Lissu sasa.
Waheshimiwa majaji nimezungumza sana kuhusu records.
Sasa naomba nirudi kwenye sheria ya ukabidhi.
S. 262 of CPA Nilisema pia kuhsuu kesi ya Dodoli Kapufi kuwa lazima mwenendo wa committal lazima ufuate sheria.
Maombi yaliyopelekwa kwa Jaji mtembwa inasema yaliambatana na viapo viwili.
S. 266[3] ya CPA ndio hoja yangu.
Inazungumzia nini kinapaswa kuwepo kwenye record of proceedings.
Sheria inasema kila records inayopelekwa kwa mshitakiwa inapaswa kujumuisha nyaraka zote ikiwemo zilizotumika kwenye jambo lolote mahakama kuu au mahakama zingine. Hawajaniambatanishia hayo manyaraka yote.
Waheshimiwa majaji hizo nyaraka kupewa mtuhumiwa iko sababu.
Sababu yenyewe iko kanuni ya 5(1) na 5(2) ya kanuni za ulinzi wa mashahidi.
Zinasema mahakama itatoa amri endapo itaridhika kuwa mtu ambae amelindwa kuna hatari atakuwa kwenye tishio la usalama.
S. 263(4) of CPA (CRIMINAL PROCEDURE ACT yaani sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai)
Inamtaka mahakama kumuelezea mtuhumiwa atakapotoa taarifa yake asiwe na hofu na wala asitegemee upendeleo wowote.
Whatsoever he says may be given in evidence at the trial. Lolote atakalosema chochote alachosema kinaweza kutumika kama ushahidi katika trial yaani kesi ya msingi huko mahakama kuu.
S. 265(5) inasema yote ambayo mtuhumiwa atakachosema kirekodiwe na asomewe.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niwapeleke kwenye records kuhusu chochote nilichosema je kiliruhusiwa? Je kilirekodiwa? Je nilisomewa? Twende sasa.
Kwenye rekodi ya Ukonga, kuna maneno ukurasa wa 5 kuna maneno ambayo yamesemwa na mahakama.
Ukisoma sheria hayo maneno yanapswa kuonekana kwneye rekodi na hayapo.
.sheria inasema aambiwe na asome.
Rekodi haioneshi kama aliambiwa. S. 263(5) of CPA nilipaswa kurekodiwa kwenye kila nitakachosema.
Sasa kwneye rekodi hii hakuna mahali kokote mtuhumiwa aliambiwa maelezo yako ni haya na ulichosema ni hiki unachochote cha kuongeza? Sijawahi ambiwa hivyo na hayapo kwenye records.
Na wala sijawahi kuulizwa una chochote cha kuongeza. Mimi sio vyakuongeza hata vyakwangu sikumaliza.
Sasa tuje rekodi ya mahakama hii kuanzia ukurasa wa 93 niliyosema yalipaswa kuwepo hayapo pia hata hayo.
Sijawahi kuambiwa kwamba haya ni maelezo yako. Nakusomea na kuulizwa una nyongeza sijawahi kuulizwa.
Maelezo haya ni ushahidi sio urembo kabisa.
S. 263(6) of CPA maelezo ya mtuhumiwa ni lazima mtuhumiwa aseme ni kweli au sio kweli? Ni maelezo yake na anayakubali.
Hakimu wa ukabidhi ni lazima athibitishe hiyo rekodi. Ukurasa wa 13 wa rekodi ya Ukonga. Pia Ukurasa wa 98 wa rekodi ya mahakama hii angalieni.
Ni lazima nyaraka hizo ziwe certified. Hakimu anasema maelezo hapo juu nathibitisha kuwa ni ya mtuhumiwa na amekiri ni yakwake. Kifungu ameweka 263(3) wakati kiuhalisia kifungu halisi ni 263(6). Anapothibitisha kuwa nilisema mimi na kukiri kuwa ni yangu. Ni wapi nilisema hayo?
Haya yaliyopo yaliandikwa wapi na lipi na lini na nani aliandika?
Sheria iansema mtuhumiwa anapaswa kusign or attest baada ya yale niliyoyasema.
Sahihi yangu wala dole gumba halipo wakati sheria inasema iwe hivyo.
Part 7 itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
🚨IDU is alarmed by reports of poisoning attempts on opposition leader @TunduLissu in custody. We urge Tanzanian authorities to protect his life, health and rights. Any harm lies with the Government of Tanzania. The world is watching! #FreeTunduLissu@SuluhuSamia (Image: Ericky Boniphase/DW)
@zittokabwe Umesha poteza mvuto kaka sababu ya kukosa msimamo ulio kufanyanya ung'ale sana pele mwanzo kifupi umesha pitwa nawakati zama zinabadilika. Wewe bado upo na siasa za kina mzee CHEYO JOHN MOMOSE. yeye amesha soma alama za nyakati aka pack. Oct tuna tiki reforms zikifanyika🙌🏻