BBT Chinangali in matatizo makubwa, Wizara ya Kilimo chini ya Waziri wake lazima iwajibishwe, hii haimsaidii Rais Samia Suluhu. Kambi haina maji, vijana hawajalipwa posho muda sasa, kilimo kimekufa na vijana wengi wameondoka kambini kukimbilia mtaani kufanya kazi nyengine.
Nikionaga mtu anasema Wairaki na Wamburu ndio makabila yenye mabinti warembo zaidi🇹🇿... Hapo najua kbs huyo mtu hajawahi kufika Muleba, Karagwe na Ngara
Huko kuna Wabanyamulenge, Wahangaza na Watutsi. Hao watu wana pua za Kiitaliano, nyama nyama za Kibantu, na maji ni mengi sn🌊
AyoTV imepokea barua kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ) ikitaka Chombo hiki cha habari kuondoa maudhui yaliyochapishwa May 24 2025 yakihusisha nukuu ya maelezo aliyoyatoa Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima kuhusu matukio ya utekaji Nchini Tanzania.
Barua hiyo ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dr. Jabiri Bakari, imeeleza kuwa maudhui hayo hayakufuata sheria na kanuni za Uandishi kwasababu yalikosa mizania inayotakiwa kutokana na kubeba taarifa za upande mmoja pekee japokuwa mwishoni mwa taarifa hiyo kulikua na maelezo ya AyoTV yaliyoeleza kuwa inaendelea kuzitafuta Mamlaka za Serikali ili kusikia upande wao juu ya yaliyosemwa na Mbunge huyo.
TCRA imeielekeza AyoTV iondoe maudhui hayo hadi pale itakapoupata upande wa pili ( Mamlaka za Serikali) ili kuweka mzania wa habari husika kwa kuwapa nafasi upande wa Serikali au Mamlaka husika kutolea ufafanuzi kauli hizo za Askofu Gwajima na kusisitiza kuwa endapo AyoTV itapuuzia au kukaidi kutekeleza maagizo hayo ya TCRA, Mamlaka haitosita kuchukua hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti dhidi ya AyoTV.
Kutokana na agizo hili la TCRA na masharti ya leseni yetu kutoka kwa Mamlaka hiyo, tunawafahamisha Wasomaji wetu kuwa endapo hawatoendelea kuyaona maudhui hayo katika mitandao yetu kuanzia leo May 31 2025, waelewe kuwa ni kutokana na kutii agizo hili la TCRA ambapo tunalazimika kuyaondoa hadi pale juhudi zetu tulizozianza tangu May 24,2025 za kuzitafuta Mamlaka za Serikali zitakapofanikiwa.
#MillardAyoUPDATES
Mtu anapotea, Jeshi la Polisi linakanusha kuhusika kupotea kwake. Ajabu ni kwamba, matukio haya ni mengi mno, na kila tukio polisi hawahusiki. Ajabu zaidi, Polisi hawatoi ripoti ya uchunguzi ya mtu aliyepotea, wala haihaingaiki kutafuta watu wanaotumia jina lao kuwachafua.