@NCHIYANGUT Tanzania ina Mifumo mizuri ya kuhifadhi Nyaraka japo kuna Wananchi ambao sio Wadilifu katika kutekeleza majukum yao naomba Serikali iwachukululie hatua kali za kisheria .
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema mapato yatokanayo na shughuli za utalii yameongezeka nchini kutoka Dola za Marekani bilioni 1.3 mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.9 mwaka 2024 sawa na ongezeko la 200% kwa Watalii wa kimataifa.
Akitoa hotuba Bungeni Jijini Dodoma leo May 19,2025 kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, Balozi Chana amesema “Hatua hii imeifanya Tanzania, kwa mujibu wa UN Tourism, kushika nafasi ya tisa duniani na ya tatu Barani Afrika kwa ongezeko la mapato ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya UVIKO-19”
#MillardAyoUPDATES
#IkuluWIkiHii Tazama muhtasari wa matukio yote muhimu aliyoyafanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika wiki hii.
MIZIGO ILIYOSAFIRISHWA KWA NJIA YA ANGA IMEONGEZEKA
Mizigo iliyosafirishwa kwa kutumia usafiri wa anga imeongezeka ambapo katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, jumla ya tani 33,112.5 za mizigo zilisafirishwa ikilinganishwa na tani 27,532 za mizigo zilizosafirishwa katika kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha 2023/24.
Kati ya mizigo hiyo, tani 30,637.2 zilisafirishwa nje ya nchi na tani 2,475.3 zilisafirishwa ndani ya nchi.
Ongezeko la mizigo inayosafirishwa linatokana na kuendelea kuimarika kwa usafiri wa anga pamoja na ununuzi wa ndege ya mizigo ya ATCL jambo ambalo limechangia kuongeza kwa usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi.
Hayo ni mafanikio ya utekelezaji wa bajeti ya serikali ya mwaka 2024/25 kwa Wizara ya Uchukuzi.
Congratulations to Professor Mohamed Yakub Janabi for being elected the World Health Organization Regional Director for Africa, for the term 2025-2030.
With decades of expertise and experience in the health sector, I have every confidence that you have all that it takes to serve our continent, and steer us all to greater heights.
The United Republic of Tanzania is thankful to every member state that believed in your skills, experience and vision for our continent.
Professor, you have my warmest wishes for a successful tenure.