Ni Binti aitwae Maimuna Yusufu Lukanga (Lulanga) Mkazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Maimuna, amehitimu masomo yake ya Kidato cha Sita na kuibuka na matokeo mazuri ya Division One ya 6 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtwara (Mtwara Girls) Na kuchaguliwa kujiunga na Chuo cha Mzumbe kilichopo Morogoro kwenda kusomea Sheria.
Ila Maimuna, anaziona dalili za kukatishwa kwa ndoto yake ya kuwa Mwanasheri kutokana na hali ngumu ya maisha ya Familia yake na hivyo kushindwa kumkamilishia mahitaji muhimu ya Chuo Ikiwa ni pamoja na Ada.
Baba Mzazi wa Maimuna ni mlemavu wa viungo, anayeilisha Familia yake kupitia kazi yake ya kushona Viatu
MAHITAJI YA MAIMUNA:
Ada ni TSH. 1300,000/= kwa mwaka.
Hostel TSH. 600,000/= kwa Mwaka
Na mahitaji Madogo Madogo
Namba ya Simu ya Baba - 0784 569 693
Jina - Abed Lukanga
Watu wa Mbagala mnasiri sana kumbe mnatume mpya huko na anafufu watu mmekaa kimya tu.
Tafadhali mtag rafiki yako wa Mbagala atupe habari za Mtume mpya. #Trending#TrendingNow
Tanzania inauza mahindi tani 650,000 nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kufuatia mazungumzo kati ya Rais Samia Suluhu na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema Aprili 26 mwaka huu na kufuatiwa na mazungumzo kati ya wizara za kisekta na balozi za nchi hizi.
VIDEO: Kampuni ya Watanzania ya Imperial Innovations imetengeneza mita za maji za kisasa za prepaid ziitwazo ‘moran’ zitakazowawezesha Watumiaji kununua maji kabla kama ilivyo kwa umeme wa LUKU.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Murtaza Ebrahim kwenye mahojiano haya sehemu ya kwanza ameiambia @AyoTV_ kwamba mita hizo zinakuja kuwa suluhisho bora kwa mara ya kwanza Tanzania kwenye sekta ya maji ———> “haya ndio mapinduzi makubwa, maji utayonunua ndio utayoyapata kama unavyonunua LUKU vile”
“Wazo hili lilianzia mwaka 2020 wakati sisi wenyewe tulipata changamoto unakuta Mtu amekuja kusoma bili lakini sisi ule muda wa kufuatilia kwamba kasoma bei gani au unit ngapi hatuna, hapo ndio wazo la kutengeneza hizi mita likanijia, tumezitengeneza wenyewe na imetuchukua miaka minne kuzitengeneza na kujiridhisha kwamba ziko tayari kwenda sokoni” - Murtaza.
Mita hizi zinatumia betri maalum ambazo zinaweza kukaa miaka sita hadi nane bila kuchajiwa na baada ya hapo betri itabadilishwa, pia Mtumiaji anaweza kusimamia matumizi ya mita yake kwa njia ya simu ikiwemo kuifunga au kuifungua popote alipo duniani.
“Sifa nyingine ni kwamba ukiwa na hii mita unaweza kukopa maji hata kwa jirani mfano nakupigia simu maji yameisha naomba nikopeshe lita kadhaa unatoa kwako unanipa naendelea kupata maji papohapo, vilevile Mtumiaji atakua akipata notification kadri maji yake yanapokaribia kuisha tofauti na mfumo kama wa umeme wa LUKU ambao haukupi notification” - Murtaza.
Murtaza amekiri kuwa Wataalamu nyuma ya ubunifu huu ni Watanzania aliowachukua kutoka Vyuo mbalimbali ambapo wengi wao ni Vijana kutoka Mbeya University ( MUST).
Je Murtaza ameonesha ubunifu huu kwa Serikali au Mamlaka za Maji ? ataziuza vipi ? maswali hayo na mengine mengi yatajibiwa wiki ijayo kwenye sehemu ya pili ya mahojiano haya. #MillardAyoUPDATES
RATIBA YA WANASIMBA LEO
Saa 1:00 Kanisani
Saa 2:00 Kufanya usafi wa nyumbani
Saa 3:00 Kufua nguo za kazini na Uniform za watoto
Saa 4:00 Chai ya nguvu
Saa 5:00 Kwenda Sokoni/ Car Wash
Saa 6:00 Kutulia nyumbani na kuhakiki Simba App yako imelipiwa
Saa 6:50 Kuingia Simba App kusubiri taarifa
Saa 7:00 Kusoma Jina la mchezaji wetu mpya
Saa 7:03 Kutabasamu kwa furaha