Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha kwa muda wa siku 30 leseni za huduma za maudhui mtandaoni za kampuni ya Mwananchi Communications Limited (The Citizen, Mwananchi Digital, Mwananchi na MwanaSpoti) kutoa huduma za maudhui mtandaoni nchini.
TCRA imesema kampuni hiyo ilichapisha maudhui yaliyokiuka kanuni ambayo yameleta tafsiri hasi kwa taifa.
Hii inatia sana moyo kuona jamii inakubali kazi kubwa unaiyofanya Maranje, Keep it up Kaka, siku moja utalipwa kwa kazi yako. @IAMartin_
BRIGEDIA MARTIN MARANJE MASESE.
‼️MAKATIBU BINAFSI WA RAIS NI AKINA NANI?‼️
Katibu (binafsi au faragha) wa marais huwa si watu wanaojulikana wakiwa kazini! Ni low key people ambao wanamsaidia Rais aliye madarakani au mstaafu katika kumsaidia majukumu yake kikazi!
Wangapi mlimjua Adam Issara au kumkuta anajiposti? Wengi tumemjua walipotangaza kifo chake 🙏��� RIP
Mzee Butiku hakujulikana sana hadi baada ya kifo cha Mwl Nyerere ingawa aliendelea kuwa Katibu wa Rais hata chini ya Mwinyi!
Hii ni nafasi nyeti maana unaweza kuja kujua mambo ya ndani sana ya mkuu wako ila unahitaji kuwa na kifua
Una nafasi POWERFUL maana hadi ratiba ya Mkuu wa Nchi unapanga wewe!
Rais anachagua na kuteua Katibu wake ila LAZIMA APITISHWE KWENYE VETTING
Sasa @SuluhuSamia alikataliwa uteuzi wa Waziri Rajab Salum akamtimua aliyempa ushauri wa kitaalum kwa nini Waziri hawezi kuwa Katibu wake
Amelazimisha mtu asiye na vigezo kukaa hapo - sasa haya ndo matokeo yake - ufisadi, ubabe - the most unprofessional OBR! Sijawahi kuona au kusikia!
Samia Suluhu the buck stops with you kwa madudu ya Waziri Rajab Salum! Ushauri uliopewa umeupuuza the chickens are coming home to roost!
#TutaelewanaTu lakini
Jina: Faustine Jackson Mafwele
Umri: miaka 47
Kabila : Mkerewe
Dini: Mkristo
Makazi : Mikocheni
Kazi: Afisa mwandamizi wa polisi
Cheo: Kamishina Msaidizi wa Polisi
Madaraka: Zonal Crime Officer
Tuhuma: Kuendesha genge la uhalifu dhidi ya binadamu.
Mawasiliano: +255 755 855 743
+255 787 922 913
1. ACP Faustine Mafwele kwa mara ya kwanza amethibitishwa hadharani na kutambuliwa na Edger Edson Mwakabela (Sativa) kama afisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania ambaye alitoa amri ya kubebwa kwake kisha kusafirishwa kwenda Arusha na katavi kupigwa risasi ya kichwa kabla ya kunusurika kuuawa.
2. ACP Faustine Mafwele amewahi kuwa OC-CID mwaka 2011-2015 wa kituo cha Polisi Arusha na baadae akawa RCO wa Mkoa wa Arusha
Wakati wa mauaji ya wanachama wa CHADEMA maandamano ya Arusha ya 04 January 2011 alikuwa OC-CID.
Wakati huo Faustine Mafwele akiwa na cheo cha ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi
Tarehe 05 January 2012 akiwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi Faustine Mafwele alipigwa risasi na Jambazi Jijini Arusha kati ya majibizano ya risasi baina yake na Jeshi la Polisi,hata hivyo askari mmoja wa Jeshi la Polisi aliuawa kwa risasi na Mafwele aliendelea kutibiwa hospitali ya Seriani.
3.Amewahi kuwa Zonal Crime Officer (ZCO) wa Kanda maalum ya MKIRU yani Mkuranga, Kibiti, Rufiji.
4.katika kesi za watu wanaolalamika kwangu ndugu zao kutekwa, kupotea au kukutwa wameuwawa asilimia 90 wanamtuhumu ACP Faustine Mafwele kama mtu ambaye ndiyo mtekelezaji wa shughuli hizi mbaya.
5.ACP Faustine Mafwele amekuwa ni Afisa wa Jeshi la Polisi ambaye hana madaraka makubwa sana ila anaogopwa hadi na viongozi wake wa Jeshi la Polisi kuanzia Kanda Maalum ya Dar es saalam hadi Makao Makuu ya Polisi,Dodoma
6.Kuna hisia ambazo hazijathibitishwa kuwa ni Penetrating Officer (PE) wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye anafanya kazi mbili kwa pamoja kiasi cha Viongozi wa Jeshi la Polisi kumuogopa wakiamini ni Mtu ambaye kazi zake zina baraka ya Idara ya Usalama wa Taifa.
7.Baada ya Kazi Maalum ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti Rufiji) kumalizika akiwa kama Crime zonal Officer (ZCO) alihamishiwa kwenda Kuwa RCO wa Mkoa wa Mwanza
Huko Dunia ilianza kufahamu ukatili wa ACP Faustine Mafwele baada ya 2021 Mzee William Sije kulalamika kuwa RCO Mafwele wa Mkoa wa Mwanza amemuua Mtoto wake James William Sije.
8.IGP Simmon Sirro alimuhamishia Mkoa wa Dar es Salaam kuja kuwa Zonal Crime Officer (ZCO) wa Kanda maalum ya Dar es saalam 06 April 2022 kwa kazi maalum dhidi ya Panya road na ujambazi wa kutumia Silaha.
9.Misheni na siri nyingi anazozijua ndiyo chanzo cha Viongozi wa Serikali ya CCM kumuogopa na kumlinda wakiamini anaweza kwenda kusema mambo mabaya zaidi anayoyajua.
Kupitia hoja hiyo, ACP Faustine Mafwele amelalamikiwa mara nyingi sana lakini Viongozi wizarani na serikalini wanamuogopa sana kuchukua hatua.
10. Mafwele pia anatuhumiwa na familia nyingi kama mtu ambaye ameshiriki mauaji kwa moja katika kuwapoteza ndugu wa baadhi ya familia zao
kupotea kwa
1.Mfanyabiashara Musa Mziba
2.Kupotea kwa Deo Mugasa
3.Kupotea kwa Adinani Hussein Mbezi
4.Kupotea kwa Vijana watano wa Aggrey
5.kutekwa na Kupigwa risasi kwa Edger Edson Mwakabela.
6.Faustine Mafwele na genge lake tarehe 22 August 2024 alituhumiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kuhusika kwake ktk Kupotea kwa Kina Godwin Mlay,Deusdedith Soka na Frank Mbise
11.Katika kuonyesha jeuri na kuogopewa na wenzake ACP Faustine Mafwele amejipa ukiranja wa kuwa mwenyekiti wa Ma-RCO wa Jeshi la Polisi Tanzania tofauti na utamaduni wa Jeshi la Polisi ulio zoeleka wa Ma-RCO kuwa chini ya usimamizi wa DCI
12.Nimeona niweke kumbukumbu hizi vizuri na wasifu mfupi wa ACP Faustine Mafwele mjue kazi kubwa iliyopo mbele yetu kuhakikisha Faustine Mafwele anafikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kujibu tuhuma zake
Bila kelele za kutosha hakuna Jambo litakalotokea kwa sababu nilizozitaja hapo juu
Boniface Jacob
Ex-Mayor Kinondoni & Ubungo
0712 239 595
The voice of the silenced Majority
@IAMartin_ Shida kubwa naona hata haipo sana kwa wasanii. SHID KUBWA NI KAMA ULIVYOELEZA, WAFUASI WAJINGA, NA WALIO WENGI NCHINI MWETU HAPA NI WAJINGA KWELI KWELI, WANASUBIRI KUSHIRIKI CHALLENGE TU
Ni uchunguzi HURU wa kimahkama (Independent Judicial Inquiry) tu (tena uwe HURU hasa) ndiyo unaweza kutupa ukweli kuhusu matukio haya ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini. Na wakati tunasubiri hatua hiyo, hawa wawili wanapaswa kuondolewa BILA YA KUCHELEWA kwa kushindwa kazi!
Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.
Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.
Kila hatua DUA. 🙏🏾
Leo mwanetu @ExMayorUbungo amerudisha fomu yake ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani. Huo ni umma wakiwepo wajumbe/wapiga kura waliamua kumsindikiza kurejesha fomu hiyo katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Pwani. #TunarejeaKwaKishindo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi na kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.
“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.
Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”
Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).
“Mteja wetu anaona maneno yote yanayozungumzwa na kunukuliwa hapo juu katika maana yake ya asili, muktadha na misemo kuwa ni kashfa, dharau na kudhuru sio tu sifa yake binafsi bali pia kwa familia yake yote, marafiki, taaluma (Siasa), Jumuiya ya Biashara, Jumuiya ya Kidini, marafiki na rika. Maneno haya si chochote lakini ushahidi dhahiri wa nia mbaya dhidi ya mteja wetu”, imeelezwa na mawakili.
Mbali na hilo, Msigwa alidai kuwa CHADEMA Digital ambayo ni huduma ya usajili wa wanachama, inamilikiwa na kampuni binafsi na kwamba Mbowe anatumia fedha za chama kwa manufaa binafsi.
“Hali hii imeleta hasara kubwa kwa mteja wetu kwani sifa yake ya kiongozi wa kisiasa, mfanyabiashara na mwanafamilia imeathirika sana,” alisema Mwasipu.
Kwa mujibu wa notisi hiyo, Msigwa anatakiwa kuomba radhi kupitia machapisho katika magazeti mawili; moja lenye kuweza kufikia nchi nzima na lingine ambalo linaweza kuwafikia watu walau wa kanda, na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
UTAPELI.
Umeshindwa kuboresha barabara za Kigamboni kwa miaka 14 ukiwa mbunge.
Umeshindwa kuboresha hata mnara mmoja wa simu ukiwa Wizara ya Mawasiliano.
Umeshindwa kuboresha hata zahanati moja ukiwa Wizara ya Afya.
Utaweza kuboresha World Health Organization (WHO)?