Watekaji, wahurumie wazazi wetu.
Namshukuru Mungu hadi sasa nimebarikiwa kuwa na watoto watatu. ELON, LIAM na FREEMAN. 24/04/2026 nikapoteza mtoto mmoja wa kiume, mama yake akiwa anajifungua. Nilipata uchungu siyo wa kawaida.
Nikakumbuka 2019 mama yangu alivyopoteza mtoto wake, Frank, akiwa na miaka 30. Aliugua malaria tu siku mbili nyingi, akafariki. Mama yangu alikuwa analia kila kilio juu ya jeneza la mtoto wake. Niliumia sana.
Nimetazama kilio cha mama yake James Temba akiaga mwili wa mwanae pale KKKT Usharika wa Tabata. Nimejisikia vibaya san. Mama anamuaga mwanae, kiwiliwili tu. Kichwa hakipo. Unaelewa maumivu yake?
Sisi ambao ni wazazi, tunaelewa maumivu ya kupoteza mtoto kwa kifo cha kawaida. Fikiria sasa kifo cha mtoto wako kutekwa, kupotezwa na kupatikana akiwa ameuwawa kikatili, amekatwa kichwa na hakionekani.
Kuna nyakati nikitulia pekee yangu, nikianza kusali na kuabudu sifa na utukufu wa jina lako, ninajiuliza. Mwenyezi Mungu kwanini umeyaruhusu yatokee?
Mzee Ali Mohammed Kibao awaache watoto wake na wajukuu wake, Godwin Mlay aiache familia yake? Deusdedith Soka bibi ataishije bila mjukuu wake?
Fredrick Chaula aliyetekwa na kupotezwa huko mkoani Mbeya, baba yake ataishije bila kumuona kijana wake mashuhuri kwa sanaa ya uchoraji? Ataacha kulia?
Dioniz Kipanya aliyetekwa na kupotezwa huko Sumbawanga, akiitwa kutoka nje na kuacha kikao cha familia kikiendelea, ndugu zangu watamsahau?
Familia ya Frank Mbise wanacheka na nani? Kijana mdogo, hakuwa mwanasiasa au mwanaharakati. Frank Mbise alikombwa pamoja na Deusdedith Soka.
Mdude wamemvamia nyumbani usiku akiwa amelala. Wamevunja mlango na geti. Wakaingia ndani na kumshambulia kwa nyundo. Damu zimemwagika.
Haikutosha, wamemvuta kutoka ndani hadi barabarani usiku huo. Damu imemwagika umbali mrefu. Wameondoka na mwili wa MDUDE kusikojulikana.
Tundu Lissu akiwa na makovu mengi ya risasi katika mwili wake, anakamatwa Mbinga (Ruvuma) na kusafirishwa hadi DSM kupewa kesi ya uhaini.
Wananchi wanaojitolea kufika katika kesi, wanakamatwa, wanapelekwa porini, wanapigwa, wanateswa, wanavunjwa viungo vya mwili.
Wanatupwa porini na msituni bila msaada. Waliowatendea hayo, wanakanusha na kusema hawahusiki kuwakamata kwa namna yoyote.
Nikajiuliza ni Mungu wa namna gani anaweza kuruhusu mambo haya mazito yatokee kwa watu wake? Kwanini anaruhusu watu wake watekwe na kupotezwa?
Mwenyezi Mungu utaendelea kuruhusu yatokee hadi siku gani? Haiwezekani kuwalinda watu wako dhidi ya ukatili wa watawala? Wasitekwe na kupotezwa?
Lakini baadae katikati ya tafakuri na maombi yangu nikiwa nalia sana, nakumbuka kwamba Mungu ametukumbusha tusinung'unike. Tusihuzunike.
Yahweh! Maamuzi yako hayahojiwi. Tunakuabudu na kukutukuza na katika mapambano ya haki tunafuta machozi yasiyokauka, tunasimama na kusonga.
Wafausi wa CHADEMA, wanasiasa, wanaharakati, wanahabari, watumishi, wafanyabiashara, wavuvi, wakulima, wajasiriamali, wazee kwa vijana.
Wanaume kwa wanawake, Wametekwa na Kuteswa. Wamefilisiwa,Wamefukuzwa vyuo, wamefukuzwa kazi, wamekosa ajira, wamekosa ndoa na kadhalika.
Wengine wapo mahabusu na hata gerezani hadi leo pasipo na haki. Wengine wanashinda korido za Mahakama kwa mashtaka ya uongo na uzushi.
Kutokana na Maandiko yako Mungu, kuna nyakati nimetamani kuinua upanga kama yule mwanafunzi wa Yesu aliyemkata sikio Askari wa Wayahudi.
Lakini Yesu akamueleza arudishe upanga wake katika ala yake kisha akaliponya sikio la bwana yule. Nahofia kuchukua hatua halafu ukaponya sikio la watu hao.
Uendelee kutujaza ujasiri wapenda haki wengine wote hapa nchini kwetu, utujaze ujasiri kama ulivyomjaza ujasiri Daudi na kulinda jina lako kwa kombeo.
Kombeo letu liwe silaha inayodhihirisha ukuu wako mbele ya wanadamu kama ulivodhihirisha kwa Wafilisti wale wasiotaahiriwa. Wakashindwa na jeshi la Daudi.
Sote tutakuwa tayari kulipa gharama za kuwa wapinzani wa Serikali katili ya CCM. Tunaelewa, lazima yatakuwepo madhara na hizo ndiyo gharama za kulipa.
Kitabu cha Kutoka 20:5 ulituonya kuwa wewe ni Mungu Mwenye wivu juu ya mamlaka na ukuu wako katika kiti cha Enzi na umetukanya kutovisujudia viti vingine.
Waliotekwa na kupotezwa, waliouawa, walioteswa, waliopoteza kazi na ajira kwa sababu ya harakati, waliokosa ndoa na uchumba kuvunjika, biashara n.k
Tutasimama na kusema kama Ayoub na tutasubiria majibu yako Mungu wa haki utakapotuongoza katika mapambano haya magumu huko mbeleni.
Tunapambana na simba na dubu wanaojitapa kutojaribiwa. Tutashinda. Yesu Kristu, mitume na manabii walijaribiwa. Wao hawataki kujaribiwa.
Utawashusha na utawavua ukuu wao hapa Duniani. Wewe ni Mungu mwenye wivu. Unawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Mi naamini washkaji wengi humu wana Idea ya Biz tukipeana Push tutanyenyuka wengi sana. Mi huwa najitahidi hata ku support kwa njia ya biashara kuungishana inasaidia.
Wengine sisi tumelelewa kwa kusaidia japo hatukuwa yatima ila wenye uwezo walitu push.
Sativa alinipanga kuhusu Sarah nikaona sio Issue Sarah nilimuungisha Shuka nikamwambia ntakupostia ila sikufanya hivo nikamwambia tutaku support kwa njia nyingine.
Mimi nilikuwaga na wazo la kufungua foundation ila ni hela ndefu sana nikaamua na mwanangu @Sativa255 tuwe tuna push tu washkaji wenye uhitaji maisha yanaendelea tumeshafanya hivi kwa wengi sana hasa washkaji ingawa haikuwa hela kubwa kidogo kama hii ila naamini iliwa save kwa kiasi flani.
Kupitia gang ya Sativa 17 na Betting Brain hii tutaifanya mara kwa mara haitaishia hapa na sio lazima sisi hata wengine tusaidiane kupushiana ukimsaidia mmoja umesaidia chain kubwa.
@Finah_Business nakutakia kila la kheri kwenye biz yako hiyo hela ni jasho letu hatujaiba hivo naamini ina baraka zote kabisa.
TAARIFA KWA UMMA.🚨
SATIVA17 tumefanikisha tulichokiahidi kwa @Finah_Business .
Tumempa MTAJI wa 4M CASH leo 5.5.2025.
SATIVA17 ni TAASISI ambayo inajihusisha na KAMARI kwasasa. Wafuatao wameshiriki kikamilifu kwenye mtaji huu aliopewa FINAH.
1. @Sativa255
2. @Thereal_taivina
3. @kingwakitaa01
4. @prolific_88
5. @Champione_Tips
6. @Chabuluma1xbet
7. @is_Dickson_9
8. #Ozil
Mwaka 2025 ni mwaka ambao tutasaidia watu mbali mbali hasa vijana kulingana na malengo tuliyojiwekea. Tunafanya hivi kwa AWAMU ambapo tutafanya kitu kwa mtu / watu kila baada ya miezi minne. Inamaanisha kwa huu tutafanya hivi mara 4.
Na tukijaaliwa UHAI Disemba tutakuwa na jambo kubwa kama TAASISI kwa jamii yetu.
Sisi ni vijana tunaoishi kwa KAMARI, tumejikusanya kuifanya “Betting business” lengo ni kufika wote. Tunarudisha kwa jamii kama sehemu ya kukumbuka na vijana wenzetu ambao wanapambana kwenye angle tofauti.
Leo tumemgusa FINAH ila naamini baada ya Muda nae ataenda kumgusa mwingine na mwisho jamii inaenda kuinuka. Tunatambua HATUWEZI KUMALIZA MATATIZO YA VIJANA WOTE, ila tunaweza kuleta NAFUU KWA BAADHI yetu.
Maisha yetu ni FUMBO, hatuzijui kesho zetu, ndiomaana tunapopata kibali kumsaidia mtu atoke sehemu moja kwenda nyingine tunafanya bila kusita tukijua hata sisi hatuijui kesho yetu na nani atatupa MSAADA.
Naomba kuwasilisha na nimtakie @Finah_Business kila lakheri kwenye hii SAFARI yake ikawe ya mafanikio.
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Naitwa Edger E Mwakabela maarufu kama SATIVA17. Kwa siku mbili tarehe 9 na 10 mwezi wa 4 mwaka 2025 nimekuwa na Lugha YA MATUSI dhidi ya Jeshi la polisi @tanpol
Siandiki huu waraka kwaajili ya KUOMBA MSAMAHA, nataka niwape taarifa ambao wamenijua JUZI. Kwahiyo kama unahisi huu uzi kwaajili ya kuomba msamaha ishia hapa.
Mimi ni mmoja kati ya wachache ya watanzania ambao nimefanikiwa kuponea kwenye UTEKAJI unaofanywa na SERIKALI chini ya JESHI LA POLISI. Kwa muda mrefu tumekuwa tukiambiwa SERIKALI ndiyo inateka watu na kuwapoteza, sasa hilo mimi lilinitokea na nikaishi.
Nilipigwa RISASI YA KICHWA na kuenda kutupwa PEMBEZONI mwa mto wenye MAMBA NA VIBOKO WAKALI, nikipona hapo basi niliwe na wanyama wakali waliopo MBUGANI kama FISI, simba na wengine waliopo ndani ya MBUGA YA KATAVI.
Yote hayo MUNGU ALINIEPUSHA NIKAISHI. Tangu siku hiyo mpaka leo licha ya kumtaja muhusika wa UTEKAJI WANGU ila HAKUNA hatua amechukuliwa zaidi ya kupandishwa vyeo JESHINI (MAFWELE). Na kibaya ni kwamba tangu mwaka jana mwezi wa 9 amekuwa akinitafuta kimya kimya aniue.
Nimeishi maisha ya kukimbizana na jeshi la polisi kwa muda wa zaidi ya miezi 8 sasa. Hakuna hatua kama serikali wala nchi imechukua kwenye tukio langu la UTEKWAJI. Gharama ninazotumia kujitibia majeraha ya RISASI YA KICHWA MPAKA SASA ni zaidi ya MILIONI 55.
Ndugu zangu jana wamenipigia sana simu, lengo sio kunilaumu ninavyotukana, lengo nikujaribu kunipooza HASIRA ZANGU kwa jeshi la polisi. Wanajua ninayo haki ya kufanya vile nafanya ila ndio TANZANIA.
Nikiona mtu kafanyiwa UNYAMAA na jeshi la polisi MOYO WANGU hautulii kabisa, maumivu ya kichwa yanaanza UPYA. Bora nitukane NIPONE na naona inasaidia maana naona nao MATUSI YANAWAUMA.
Hii ndio njia nimeichagua kupunguza hasira zangu maana HAKI SIWEZI KUIPATA KWENYE HILI TAIFA. Kwahiyo PUNGUZA USHAURI ULIENIJUA JUZI ACHA SHOBO.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Siku 15 zimepita tangu kupotea kwa mpendwa wetu, Daniel Chonchorio. Ni kipindi kigumu, si kwa familia pekee, bali kwa jamii nzima inayomfahamu, kumpenda na kumjali. Katika hali hii ya sintofahamu, tunawakumbusha wote kuwa mshikamano wetu kama jamii ndiyo nguvu kuu ya matumaini, Tunawaomba tuendelee kuombea, kutafuta, na kushirikiana kwa njia yoyote ile Kila mchango una maana, na kila moyo unaojali ni sehemu ya tumaini la kurejea kwa salama kwa Daniel. Jamii yetu imesimama pamoja mara nyingi na leo tena tunasimama pamoja, tukiwa wamoja katika imani na upendo. Daniel hatujakuacha. Popote ulipo, jamii yako iko nyuma yako, mbele yako, na pembeni yako kwa maombi, kwa matumaini, na kwa upendo usioisha. MRUDISHENI DANIEL URAINI ANA KILA HAKI YA KUA HURU.
#BringDanielHome
#PrayersForDaniel
#FaithOverFear
#NeverStopPraying
#BringBackdanielChonchorio
#WherelsChox
#FreeChox
#FreeChonchorio
#FreeDanielChonchorio
#BringBackdanielChonchorio
#JusticeForChonchorio
Wakuu tulikubaliana haya maparody ni kwa ajili ya kujichotea Followers na sio kujichotea vitita vya Fedha..... huyu jamaa anazingua Kuma La bibi yake.🖕🖕🖕