#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 6
Amemaliza Wakili wa Serikali Mrema
Naona Majaji wanajadili jambo kidogo hapa
Jaji Nduguru anasema kila upande una wajibu wa kuiambia mahakama sio useme navumilia.
Kama kuna jambo lilionekana mapema kuna lina shida ulipaswa kusema na sio kusema nilikuwa navumilia.
Naomba tuwe guided na sheria maana sheria iko hapo.
Wote tunajua kuwa tunabanwa na pleadings na pleading ni ile PO yenyewe.
Msemaji unakuwa kwenye jicho la unasema mambo mengi ambayo yako on face of records.
Anaendelea Mhe. Lissu sasa.
Waheshimiwa majaji nimezungumza sana kuhusu records.
Sasa naomba nirudi kwenye sheria ya ukabidhi.
S. 262 of CPA Nilisema pia kuhsuu kesi ya Dodoli Kapufi kuwa lazima mwenendo wa committal lazima ufuate sheria.
Maombi yaliyopelekwa kwa Jaji mtembwa inasema yaliambatana na viapo viwili.
S. 266[3] ya CPA ndio hoja yangu.
Inazungumzia nini kinapaswa kuwepo kwenye record of proceedings.
Sheria inasema kila records inayopelekwa kwa mshitakiwa inapaswa kujumuisha nyaraka zote ikiwemo zilizotumika kwenye jambo lolote mahakama kuu au mahakama zingine. Hawajaniambatanishia hayo manyaraka yote.
Waheshimiwa majaji hizo nyaraka kupewa mtuhumiwa iko sababu.
Sababu yenyewe iko kanuni ya 5(1) na 5(2) ya kanuni za ulinzi wa mashahidi.
Zinasema mahakama itatoa amri endapo itaridhika kuwa mtu ambae amelindwa kuna hatari atakuwa kwenye tishio la usalama.
S. 263(4) of CPA (CRIMINAL PROCEDURE ACT yaani sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai)
Inamtaka mahakama kumuelezea mtuhumiwa atakapotoa taarifa yake asiwe na hofu na wala asitegemee upendeleo wowote.
Whatsoever he says may be given in evidence at the trial. Lolote atakalosema chochote alachosema kinaweza kutumika kama ushahidi katika trial yaani kesi ya msingi huko mahakama kuu.
S. 265(5) inasema yote ambayo mtuhumiwa atakachosema kirekodiwe na asomewe.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niwapeleke kwenye records kuhusu chochote nilichosema je kiliruhusiwa? Je kilirekodiwa? Je nilisomewa? Twende sasa.
Kwenye rekodi ya Ukonga, kuna maneno ukurasa wa 5 kuna maneno ambayo yamesemwa na mahakama.
Ukisoma sheria hayo maneno yanapswa kuonekana kwneye rekodi na hayapo.
.sheria inasema aambiwe na asome.
Rekodi haioneshi kama aliambiwa. S. 263(5) of CPA nilipaswa kurekodiwa kwenye kila nitakachosema.
Sasa kwneye rekodi hii hakuna mahali kokote mtuhumiwa aliambiwa maelezo yako ni haya na ulichosema ni hiki unachochote cha kuongeza? Sijawahi ambiwa hivyo na hayapo kwenye records.
Na wala sijawahi kuulizwa una chochote cha kuongeza. Mimi sio vyakuongeza hata vyakwangu sikumaliza.
Sasa tuje rekodi ya mahakama hii kuanzia ukurasa wa 93 niliyosema yalipaswa kuwepo hayapo pia hata hayo.
Sijawahi kuambiwa kwamba haya ni maelezo yako. Nakusomea na kuulizwa una nyongeza sijawahi kuulizwa.
Maelezo haya ni ushahidi sio urembo kabisa.
S. 263(6) of CPA maelezo ya mtuhumiwa ni lazima mtuhumiwa aseme ni kweli au sio kweli? Ni maelezo yake na anayakubali.
Hakimu wa ukabidhi ni lazima athibitishe hiyo rekodi. Ukurasa wa 13 wa rekodi ya Ukonga. Pia Ukurasa wa 98 wa rekodi ya mahakama hii angalieni.
Ni lazima nyaraka hizo ziwe certified. Hakimu anasema maelezo hapo juu nathibitisha kuwa ni ya mtuhumiwa na amekiri ni yakwake. Kifungu ameweka 263(3) wakati kiuhalisia kifungu halisi ni 263(6). Anapothibitisha kuwa nilisema mimi na kukiri kuwa ni yangu. Ni wapi nilisema hayo?
Haya yaliyopo yaliandikwa wapi na lipi na lini na nani aliandika?
Sheria iansema mtuhumiwa anapaswa kusign or attest baada ya yale niliyoyasema.
Sahihi yangu wala dole gumba halipo wakati sheria inasema iwe hivyo.
Part 7 itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
Ndugu Watanzania,
Kwa heshima na taadhima, ninawaandikia barua hii nikiwa mwenye uchungu wa kweli juu ya hatima ya nchi yetu. Sauti yangu ni sauti ya mamilioni ya Watanzania waliokata tamaa. Ni kilio cha taifa lililonyimwa haki, likakandamizwa kisiasa, na sasa likielea bila dira.Leo tunashuhudia kilele cha udanganyifu wa kitaifa unaoitwa uchaguzi. Kinachoendelea mbele ya macho yetu si uchaguzi, bali ni maonyesho ya kisiasa yaliyotengenezwa na CCM kwa ajili ya kudumisha utawala wake wa mabavu. Mfumo wetu wa uchaguzi umepoteza uhalali. Tume ya uchaguzi haijitegemei. Sheria zimejaa upendeleo. Na uhuru wa wapinzani unadhibitiwa kwa vitisho, vifungo, na masharti ya hovyo.
Katika hali hii ya giza, chama kikuu cha upinzani CHADEMA tumechukua msimamo wa kishujaa na wa kizalendo: “No Reforms, No Elections.”
Hakuna mageuzi, hakuna uchaguzi.
Hakuna tume huru, hakuna ushiriki.
Hakuna sheria ya haki, hakuna maana ya kura.Msimamo huu wa CHADEMA si wa ukaidi. Ni msimamo wa kulinda heshima ya wananchi, wa kupigania demokrasia ya kweli, na wa kusema ukweli kwa ujasiri wakati ambapo wengine wanaogopa.
Lakini kinachouma zaidi ni hiki: wakati CHADEMA wanasimama imara kwa ajili ya taifa, wimbi kubwa la watu — hasa vijana — linakimbilia kuchukua fomu za kugombea. Wengi wao hawana sera, hawana maadili, wala hawana dira ya taifa. Wanaona kutokuwepo kwa CHADEMA kama fursa ya kupenya bila ushindani. Wanadhani kuwa uchaguzi bila chama kikuu cha upinzani ni “mteremko wa kisiasa.” Hawajui kwamba wanashiriki katika kufunika kaburi la demokrasia. Na kilicho cha aibu zaidi ni kuwepo kwa baadhi ya vyama vinavyojiita vya upinzani vinavyoshiriki uchaguzi huu huku wakijua fika kuwa hakuna usawa, hakuna haki, na hakuna matumaini. Hawa si wapinzani — ni wasindikizaji wa watawala. Wamesahau wajibu wao wa kupigania haki ya wananchi. Wameamua kuuza heshima ya siasa kwa tiketi ya kugombea.
Sisi ndio tulipaswa kuwa mstari wa mbele kulinda msingi wa “No Reforms, No Elections.” Sisi ndio tungepaswa kulia na kudai tume huru. Tungepaswa kuandika, kuandamana, kuhamasisha na kushinikiza mageuzi ya kweli ya kisiasa. Lakini badala yake, tumekuwa mashabiki wa mfumo huu wa hovyo. Tumeingia kwenye siasa bila kusoma historia ya taifa letu. Tumejitosa kwenye uchaguzi wa aibu tukidhani kuwa siasa ni jukwaa la sifa na Fedha badala ya uwanja wa majukumu.
Nawauliza leo:
Je, ni ujasiri au ni ujinga kugombea uchaguzi ambao tayari umepangwa?
Ni uadilifu au ni tamaa kugombea pasipo haki wala sheria ya haki?
Na ni uzalendo au ni usaliti kushiriki uchaguzi ambao unawadhulumu mamilioni ya Watanzania kwa kimya?
Wito wa “No Reforms, No Elections” si wimbo wa CHADEMA peke yake. Ni wito wa kila Mtanzania anayejua tofauti kati ya haki na hila, kati ya uongozi na ulaji, kati ya siasa safi na siasa ya hovyo.
Watanzania wenzangu, huu si wakati wa vigeugeu. Si wakati wa kusubiri kufaidika kwenye mfumo uliopinda. Ni wakati wa kusema ukweli, hata kama ni kwa uchache.
Wito wangu, tuunge mkono kauli ya “No Reforms, No Elections” kwa vitendo, si maneno.
Tuwakemee vijana wanaogeuza siasa kuwa jukwaa la kutafuta umaarufu badala ya majukumu
Tuwalaani wapinzani bandia wanaosaidia CCM kudumisha mfumo huu wa mabavu.
Pasipo mageuzi, uchaguzi ni mzaha.
Pasipo uchaguzi huru, hatuna uhuru.
Pasipo ujasiri wa vijana, hatuna kesho.
Pia Mheshimiwa rais utakuwa umeona watu wameanza kutumia mifumo ya Camera majumbani mwao, maofisini na kwenda maeneo ya mifumo hiyo.
Wengine wameanza kujihami kwa kuyashambulia magari yanayofanana na yatumiwayo sana na "wakamataji kwa nguvu"
Hii inaleta ujumbe gani kwako rais?
CCM wamechagua mwisho mbaya..!
Jana usiku nimempigia Mzee mmoja mstaafu wa serikali aliyewahi kuhudumu kama msaidizi wa mambo ya ulinzi na usalama wakati wa Rais Julius Kambarage Nyerere.
Nimemlalamikia namna serikali ya CCM,CCM yenyewe na vyombo vya dola jinsi vilivyochezea uchaguzi wa serikali za mitaa tangu zoezi la uandikishaji,uteuzi na hata kuelekea kupiga kura na kutangaza washindi.
1.Mzee amesema kila kitu kinatokea kwa sababu,moja ya sababu ya CCM kuharibu uchaguzi ni Wananchi kukosa Imani na wa CCM kiasi cha kukosa ushawishi na kutochagulika tena .
2.Kama kuna kosa CCM watakuja Kulijutia ni Kutengeneza Mazingira ya lazima kwa Wananchi Kukosa Imani na Uchaguzi; kwa sababu Wananchi Wataiondoa CCM bila ya Kusubiri tena au Kutumia Uchaguzi
3.CCM ikiondolewa bila uchaguzi madarakani hali itakuwa mbaya sana,kwakuwa wataondolewa kwa njia ya machafuko.
4.CCM ikiondolewa kwa machafuko hawatopata nafasi ya kuendelea Kubakia na mali zao,uhuru wao na huenda hata uhai wa baadhi ya Viongozi wao au makada wao.
5.Ubaya wa Kuondolewa madarakani kwa machafuko hakutegemei muda kiasi gani kama ilivyo muda wa uchaguzi ,Mtawala anaweza Kujitangazia ushindi wa Kishindo October alafu umma ukamuondoa kwa nguvu mwezi December ili mradi Wananchi wawe wamekuchoka.
5.Kazi ya Usalama wa Taifa ilikuwa ni kama Kamisaa wa mchezo awapo uwanjani,ilikuwa ni kuangalia na Kuzuia CCM wasivuke mipaka yao katika kutawala na kubashiri hatari inayokuja mbele ili wasije kufanya Wananchi watafute njia mbadala ya Kuwaondoa madarakani nje ya uchaguzi.
Swali langu kwa Mzee likuwa Je Watanzania hawa Bongolala ndiyo wanaweza Kuiondoa CCM madarakani kwa nguvu..?
Mzee amenijibu kuwa hakuna mtu mbaya Duniani kama mtu mpole na unayefikiri ni mjinga. kwa sababu siku akichukua hatua inakuwa ni "SURPRISE"
Kuna nchi zilikuwa na Wananchi wajinga kuliko hawa wa Tanzania lakini siku waliyo badilishia watawala Kibao,hakuna Jeshi lilitosha kuzuia umma wa Wananchi hao kuingia barabarani.
MAzee anaiona hali hiyo inakuja Tanzania, na wala haiko mbali sana,anafikiri pamoja na Uzee wake,lakini anaweza Kushuhudia hali hiyo kabla Mwenyezi Mungu ajachukua uhai wake.
Mzee anamalizia kwa kusema furaha ya CCM juu ya uovu huu unaoendela katika chaguzi ni ya muda mfupi sana,laiti wangejua kinachokuja mbele yao wasinge jaribu Kulivua chupi Taifa na Kulibaka hadharani kiasi hiki.
Taifa litakosa uvumilivu na kuamua kujitetea,ghazabu ya Wananchi itakuwa Juu ya CCM
Anasikitika kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kuchagua hatima yao mbaya.
. @naythetrueboy ft. Raydiance - Nitasema
Verse mbili hazitoshi kabisa Emmanuel, tungepata hata verse nane hivi kwenye hii hotuba kwa Taifa. Anyways, mpo wachache sana wasanii wenye uwezo wa kusema mambo yanayoigusa jamii bila woga. Kuna gharama za kulipa lakini wewe ni MSHINDI