Kuna wafanyakazi wawili.
Wote wanapokea TSh 1,000,000 kwa mwezi.
Wa kwanza anatumia kila kitu.
Wa pili anaishi chini ya uwezo wake.
Anawekeza.
Anajifunza.
Ananunua assets.
Baada ya miaka 10, wote watakuwa wamepata mshahara karibu sawa.
Lakini…
👇🏼
Ukitazama hii video halafu ukaelewa vizuri huwezi kutapeliwa ardhi. Matapeli wengi wa ardhi hawana uelewa wa masuala ya ardhi ni bahati mbaya hata nyie wateja hamna uelewa wa masuala ya ardhi.
UTARATIBU WA MKRISTU MKATOLIKI KANISANI
•Unapoingia Kanisani, chovya maji ya baraka na kusema:
"Unitakase Ee Bwana uovu wangu wote, ili nipate kushiriki ibada takatifu: Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina!
•Kama Kanisani kuna Ekaristi Takatifu iliyohifadhiwa katika Tabernakulo, piga goti huku ukisali: "Bwana wangu na Mungu wangu". Haya ni maneno aliyotamka Tomaso baada ya kumwona Yesu Mfufuka (Yoh 20:28).
•Ukiinuka sali: "Nitakusifu na kukuabudu katika Ekaristi takatifu"
•Nenda mpaka kwenye kiti, piga magoti huku ukitoa nia yako ya kusali Misa siku hiyo, mfano:
"Ee Mungu, ninaungana na jeshi la mbinguni, pamoja na Bikira Maria, nikiwa na nia ya kumwombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, jirani yangu ambaye hatuelewani na pia familia yetu ambayo haina amani. Kwa Sadaka hii ya Misa Takatifu, mponye mama yangu, leta uelewano na jirani yangu, na pia rejesha amani ya familia yetu pamoja na familia zote ambazo hazina amani"
NB: KILA MISA UNAYOSHIRIKI HAKIKISHA UNA NIA YAKO NA UINGANISHE NA SADAKA HIYO YA MSALABA. USISHIRIKI MISA KAMA MTAZAMAJI BILA KUWA NA NIA YAKO MOYONI.
•Endelea na ibada ya Misa na Kushiriki Litrujia kikamilifu.
NB: Hakikisha unashiriki kikamilifu kwa kuimba, kuitika kwa sauti, kusimama, kupiga magoti nk kwa uchangamfu.
Misa huwa tunashiriki wote kwa pamoja lakini MATUNDA YA MISA kila mmoja anapokea tofauti kulingana na jinsi alivyoshiriki.
Kama ni kwa asilimia, basi sio wote huwa tunapata asilimia zinazolingana za neema kwenye Misa. Kuna wanaopata neema nyingi zaidi, wanaopata kidogo nk kulingana na maandalizi ya moyo na ushiriki hai katika kupokea matunda ya adhimisho lenyewe.
Kama ni bomba linalotiririsha maji, basi kila mmoja wetu ni mtekaji akiwa na chombo chake. Wingi wa maji (Neema) utakaoingia ndani ya chombo (Roho/moyo) utategemea:
1. Chombo chako kipoje wakati unateka hayo maji
2. Nafasi (kama ndani ya chombo nafasi ni ndogo, ndivyo na maji yatakavyoingia machache. Kama nafasi ni kubwa, ndivyo na maji yatakavyoingia mengi. Kama moyo umejaa hauna nafasi, ndivyo na Neema hazitaingia kabisa kwasababu hazina sehemu ya kuingia)
3. Umekiwekaje bombani ili maji yaingie ndani (hapa sasa ndio USHIRIKI HAI katika adhimisho.
Hivyo, tuliza akili na moyo wakati wa Misa, na shiriki kikamilifu Liturujia hatua kwa hatua.
Ndiposa kila mmoja anapokea neema za Misa kwa kadiri ya maandalizi aliyofanya na ushiriki anaoonyesha wakati wa adhimisho.
NB: Utofauti wa kupokea matunda ya adhimisho la Misa haupo kwa mtoaji (Yesu) bali kwa mpokeaji (Anayeshiriki). Utofauti wa maji tunapoenda bombani kuteka, haupo kwa bomba linalotoa maji, bali kwa aina ya chombo na utayari wa mhusika kuteka maji hayo.
Tuendelee
•Wakati wa Kupokea Ekaristi (Komunyo) ukikumbuka kuwa una dhambi kubwa (ya mauti), komunika kwa sala ya tamaa. Usithubutu KAMWE kupokea Ekaristi ukiwa na dhambi ya mauti.
"Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. Maana alaye na kunywa, HULA NA KUNYWA HUKUMU YA NAFSI YAKE, KWA KUTOKUUPAMBANUA ULE MWILI. Kwa sababu hiyo wako WENGI KWENU WALIO HAWAWEZI NA DHAIFU, NA WATU KADHA WA KADHA WAMEKUFA." (1 Kor 11:26-30)
Hivyo, usipokee Ekaristi ukiwa na dhambi. Baki upokee kwa tamaa ya moyo. Jisikie wivu Mtakatifu wakati huo, na jitahidi ujitakase kwa kuungama ili adhimisho lingine usikae tena bila kupokea.
•Mwisho, wakati wa kuondoka chovya maji ya baraka na ujibariki. Kwa kuwa baada ya adhimisho huwa tunapaswa kwenda kuishi kile tulichoadhimisha, waweza kusali sala ya binafsi "Unilinde Ee Mwenyezi Mungu, nikapate kuwa mfano katika jamii yangu, na nikushuhudie katika matendo yangu"
Hapo unachovya maji ya baraka na kufanya ishara ya Msalaba "Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina"
Tumsifu Yesu Kristu. Mungu akubariki.
SNAKE BITE in an area with no hospital?
Tie about 3 inches above the bite, apply the LATEX from the stalk of COCOYAM leaves on and over the bitten area and take one tablespoon of charcoal (can be chewed if not in powder form).
Very effective SNAKE poison’s antidote used in the jungle🍀
RATIBA YA KWARESMA 2026 ✝️
• Jumatano ya Majivu – Feb 18: mwanzo wa toba na unyenyekevu
• Dominika za Kwaresma – Feb 22–Machi 22: safari ya sala, kufunga na matendo ya upendo
• Dominika ya Laetare – Machi 15: furaha katikati ya toba
• Dominika ya Matawi – Machi 29: kuingia kwa Yesu Yerusalemu
• Alhamisi Kuu – Aprili 2: Ekaristi na Ukuhani
• Ijumaa Kuu – Aprili 3: mateso na kifo cha Kristo
• Mkesha wa Pasaka – Aprili 4: ushindi wa nuru
• Pasaka – Aprili 5: ufufuko wa Bwana 🙏✝️l
Kuna watu wana historia ngumu na za kustaajabisha mpaka unajiuliza kwanini yeye tu? Mmoja wao ni Mathew Peter Kijiu (40) mkazi wa Yombo-Vituka DSM. Mwaka 2020 akielekea kazini kwenye kiwanda kimoja cha vinywaji maeneo ya Vingunguti alipata ajali akiwa kwenye Bajaj baada ya kugongwa na daladala. Alivunjika mguu, na kwa sababu alikuwa kibarua tu (hana mkataba) hakupata msaada wa matibabu kutoka kwa Mwajiri.
Alijitibia kwa gharama zake hospitali ya Amana. Baada ya miezi mitano alipata nafuu akawa na uwezo wa kutembea japo kwa kuchechemea. Aliporudi kazini aliambiwa nafasi yake imeshapata mtu mwingine, atajulishwa ikiwa kutatokea nafasi za vibarua baadaye.
Akarudi nyumbani, miezi ikapita bila kuitwa kazini. Alipofuatilia akaambiwa bado hakuna nafasi. Akaamua atafute shughuli nyingine ya kufanya ambayo itamsaidia kuendesha familia. Kuna baadhi ya wafugaji wa kuku alikua anafahamiana nao maeneo ya Kitunda, akawaomba wampe mayai kwa mali kuauli. Anachukua mayai, anaenda kuuza, jioni anawalipa, kisha yeye anabaki na faida.
Mwaka 2023 akiwa amepakia mayai kwenye guta, alipata ajali maeneo ya Banana baada ya kugongwa na Suzuki Carry. Mayai yalivunjika na yeye akaumia kichwani. Alikimbizwa Amana lakini ikaonekana kesi yake ni kubwa hivyo akapewa rufaa ya MOI. Alifanyiwa upasuaji na kupona. Hata hivyo alipata changamoto ya kupoteza kumbukumbu mara kwa mara. Alitakiwa kuhudhuria kliniki mara moja kila mwezi kwa uangalizi wa madaktari.
Mwaka 2024 akiwa anashuka kwenye daladala pale nje ya geti la Muhimbili, akielekea MOI kwa ajili ya kliniki, aligongwa na pikipiki na kuumizwa mguu uleule aliovunjika awali. Alikimbizwa MOI na kufanyiwa upasuaji.
Hata hivyo tangu wakati huo bado kidonda ni kibichi na anatembelea magongo. Ameshindwa kurudi hospitalini kutokana na kukosa fedha. Anahofia kidonda hicho kugeuka kansa kwa kuwa kimekaa muda mrefu. Makadirio ya matibabu yake ni TZS 3M.
Ifanye sadaka yako ya kuanza mwaka 2026 iokoe maisha ya Mathew na Mungu aitumie kubariki kazi za mikono yako kwa mwaka huu. M-PESA #0752581983, Tigopesa #0719744954, CRDB #0150633516500, NMB #24110012109 Gifted Hearts Foundation. Rudisha Tabasamu Let Love Lead.