@millardayo Yule WA Kagera amefanywa nini? Wanaotekwa ni Nani mtekaji na mmefanya nini? Ni mara ngapi CCM wametembea na mapanga? Give us a break Nchimbi umwagaji damu umeanzishwa na chama chako na unahamasishwa kisirisiri makambi bado yapo?
Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye amesema mchakato wa Tanzania kuwa na satelaiti yake yenyewe unaendelea vizuri na kusema endapo mchakato utakamilika satelaiti hiyo itasaidia kuboresha huduma za mawasiliano Nchini hadi vijijini.
Akiongea Ikulu Dar es salaam leo June 06,2024, Nape amesema ““Wenzetu wamepiga hatua kubwa kwenye miundombinu ya mawasiliano, hapa kwetu tunaendelea na uwekezaji, uwekezaji huo ni gharama, kingine wenzetu wanazalisha smart device kwa maana ya simu janja n.k, sisi kwetu tuna changamoto ya kusambaa kwa vifaa hivyo kwasababu ni ghali, moja ya eneo ambalo tumezungumza kwa kina ni kuona namna ambavyo tunaweza kushirikiana nao tukazalisha hapa kwetu kwa maana ya kuviunganisha vifaa ambavyo vitakuwa kwa bei nafuu ili Watanzania waweze kuvimudu”
“Najua swali kubwa hapa ni kwamba miundombinu vijijini ikoje, mtakumbuka bajeti yetu iliyopita tumetangaza mchakato wa kuwa na satelaiti yetu kama Nchi, mchakato huo unaendelea vizuri, zipo Timu zimeenda Duniani, Katibu Mkuu na Timu yake walikuwa China, wengine wataenda Marekani na kwingine , baada ya pale pamoja na miundombinu mingine ambayo tunaendelea lakini hili la kuwa na satelaiti yetu kama Nchi linaendelea vizuri na changamoto hizi zitapungua”
“Lazima tujenge utamaduni aa kufanya kazi huu utamaduni wa Watu wanashinda mtandaoni masaa 24 halafu baada ya pale mfukoni hamna kitu huu utamaduni lazima tuupige vita vinginevyo hatuwezi kutoka, na ni kupitia kazi, Watu wasifikiri kuna Mjomba atakuja mahali akuletee maendeleo ya maisha yako”
#MillardAyoUPDATES
@millardayo Seriously!? Waziri ambaye ana history ya kuzima TV licence tu wananchi wasifuatilie mijadala ya wawakilishi wap eti waziri WA mawasiliano fyiuuu! Only in tz