@iamZature The size of rebar (reinforcing bar) to use in building construction depends on several factors
Do you have specific details about your construction project (e.g., type of building or specific element), so I can give a more tailored recommendation?
#VIDEO AyoTV imefika katika Hoteli iliyopo Kiluvya Madukani Wilayani Ubungo, Dar es salaam lilikotokea aribio la utekaji wa Mfanyabiashara Deogratius Tarimo Mkazi wa Kibaha, Mkoani Pwani na kuongea na mmoja wa Wahudumu walioshuhudia tukio lote kuanzia mwanzo mwisho ambapo amesema Tarimo alifika na kuagiza maji huku akisema anamsubiri Mtu ambaye wamepanga kukutana mahali hapo lakini baada ya muda wakaja Watu watatu na kulazimisha kumkamata huku wakijitambulisha kuwa wao ni Askari Polisi kutoka kituo cha Polisi Oysterbay.
Muhudumu huyo ambaye hajataka kuonekana sura wala kutaja jina lake kwasababu za kiusalama amenukuliwa akiiambia @AyoTV_ yafuatayo “Hawa Watu kabla ya Tarimo hajaja walikuja na gari lao likawa linasitasita kuingia wakawa wamesimama, wakashuka wakamwambia sisi ni Polisi kutoka Oysterbay unahitajika kituoni, hawakusema kwa kosa gani na hawakuwa na vielelezo vyovyote”
“Yule Baba (Tarimo) akasema naomba nimpigie Ndugu yoyote wakamkatalia wakaanza kuvutanavutana kwa nguvu wakamvua shati wakataka kumuingiza kwenye gari kwa nguvu sasa yule alikuwa mnene gari ndogo akawa anapiga kelele Majirani nisaidieni, baadaye walipoona wameshindwa kumuingiza wakaondoka wakamwambia ‘tutakupata’ hawakumwambia kosa lake, Tarimo ni Mteja wetu wa muda mrefu ila hawa waliotaka kumteka ni mara ya kwanza kuwaona hawajawahi kuja”
“Walipoondoka, Tarimo akarudi ndani akiwa na pingu mkono mmoja maana walishaanza kumfunga pingu, aliporudi alikuwa kama ana wenge, hata dakika 10 hazikuisha akawasha gari akaondoka, pingu alienda kuitolea Polisi”
@AyoTV_ imefanya pia jitihada za kuongea na Majirani ambao baadhi yao walionekana kwenye video wakiwa wanashangaa wakati Tarimo akitaka kutekwa bila kumsaidia wala kupiga kelele lakini Majirani hao wamekataa kuhojiwa wakisema kama walivyoogopa kumuokoa Tarimo wanaogopa pia kuongea…. #AyoTV inaendelea na juhudi za kumpata Tarimo mwenyewe ili kulifahamu kwa undani sakata hili. #MillardAyoUPDATES