#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 6
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Duuh sasa mawakili binafsi neno utaratibu halijasemwa kokote lakini hawa wa Serikali neno Utaratibu ndio limewekwa. Haya soma pia kokote walipokuja mawakili wa serikali pameandikwaje?
Wakili Maduhu: Wasikilizwe na wapewe nafasi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo kuna ubaguzi kati ya mawakili wa serikali na mawakili binafsi?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Ubaguzi wa aina hii unaruhusiwa kwa sheria za Tanzania?
Wakili Maduhu: Hauruhusiwi kabisa kabisa.
Mhe. Lissu: Mawakili waliotendewa hivi ni zaidi ya mawakili 36 ukiachana na wakwangu ni mawakili wa watu wengine pia.
Wakili Maduhu: Kwa kiasi kikubwa mawakili wote tunatendewa huo unyama.
Mhe. Lissu: Annexure A3 ni hukumu ya Jaji Mkwizu ya Tar. 11/07/2025 haya malalamiko ya kuingiliwa mawasiliano kati ya mawakili wangu sikuyafikisha mahakamani ya yakatolewa maamuzi na mahakamu kuu.
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Na malalamiko haya yanahusiana na ukiukwaji wa kanuni ya 13 ya uendeshaji wa Magereza?
Wakili Maduhu: sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Licha ya maelekezo hayo ya Jaji Mkwizu kwamba watekeleze sheria je ulitekelezwa na magereza?
Wakili Maduhu: Haukutekelezwa kabisa.
Mhe. Lissu: Je mambo haya niliyaeleza pia kule Kisutu kuhusu mawasiliano yangu?
Wakili Maduhu: Sahihi. Hata hapa Mahakama Kuu ukisema hayo Mahakama kuu kwenye kesi yako ya uhaini.
Mhe z Lissu: Kwahiyo malalamiko yangu nimeyawasilisha kwa watu wanaotambulika kisheria.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Mhe. Lissu: Twende annexure A4 kwamba kikosi kazi kinachoshughulikia watu wanaofungwa hovyo hovyo cha umoja wa mataifa mimi nimetajwa na kesi yangu kwasababu kikosi kazi cha umoja wa mataifa kimepelekewa malalamiko yangu na wamesema haya mambo yakomeshwe? Kweli au si kweli.
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa hawa ambao hawataki kutii sheria akiwemo Bwana Jela wakati kuna mwongozo wa umoja wa mataifa?
Wakili Maduhu: Sijui wanataka waambiwe na nani hawa.
Mhe. Lissu: au wanataka twende kwa Mungu tufe ndio tutapata hiyo haki yetu?
Wakili Maduhu: Nafikiri hatujakosea kuja hapa mahakamani.
Mhe. Lissu: Nimemaliza mimi.
Anasimama Wakili wa Serikali Kalokola na yeye anataka kumuuliza swali Wakili Maduhu william.
Anasimama Lissu anasema hilo jambo hawakuomba.
Jaji anasema Stanley Kalokola na wewe uulize hayo maswali yako.
Wakili wa Serikali Kalokola: Wewe ni Wakili.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Wakili wa Serikali Kalokola: Una uzoefu wa miaka mingapi?
Wakili Maduhu: Miaka 6.
Wakili wa Serikali Kalokola: Respondent wa nne nae mmemshitaki hapa? Ambae ni Lissu.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Wakili wa Serikali Kalokola: kuna mahali kokote ulililalamikia suala hili kwa Jaji Mkwizu?
Wakili Maduhu: Halipo.
Wakili wa Serikali Kalokola: Ulibaguliwa kwasababu ya rangi yako kuna muhali umesema kwenye kiapo chako?
Wakili Maduhu: Siwezi kuwa na uhakika.
Wakili wa Serikali Kalokola: Onesha uliposema asikilizwe?
Wakili Maduhu: ameonesha maeneo matatu.
Wakili wa Serikali Kalokola: ulitembelea magereza mara nyingi na je jina lako lipo kuonesha uliandikwa jina?
Wakili Maduhu: niliandikwa mara tatu tu baada ya hapo sikuwahi kuandikwa tena licha ya kwenda.
Wakili wa Serikali Kalokola: Je waliokuwa wanakusikiliza ni akina nani?
Wakili Maduhu: Mkuu wa gereza na wenzake walikuwa wananisikiliza. Surveilance ya kufa mtu.
Wakili wa Serikali Kalokola; Ni hayo tu Waheshimiwa majaji.
Wakili Maduhu William amemaliza kuhojiwa sasa muda unaangaliwa kama unatosha. Tayari saa 10 na nusu kwahiyo Wakili wa Serikali ameomba waahirishe tuanze kesho asubuhi.
Majaji wanasema tukutane kesho asubuhi saa tatu.
Naomba Repost yako.
[Baada Ya Muda Mfupi Ardhi Ndio Kaburi Lako]
Anasema Al-Hasan Al-Baswrī [Allah Amrehem]
يا ابنَ آدمَ! ضَع قَدَمَكَ على أَرْضِكَ ، واعلم أَنَّها بعدَ قليلٍ قَبرُكَ
Ewe! Mwana Wa Adamu; Weka Mguu Wako Juu Ya Ardhi Yako, Na Tambua Ardhi Hiyo Baada Ya Muda Mfupi Ndio Kaburi Lako
[صحيح]
[كتاب الزهد للإمام أحمد بن حنبل (٥٥)]
Jana niliandika ujumbe nikikosoa kitendo cha Mzee MBOWE kumuombea msamaha SABAYA. Nimepata maoni mengi; wengine wakisema sikuwa sawa.
Ipo hivi. Kuna mambo katika siasa hayawezi kufutwa na maneno laini na mepesi ya “msamaha,” hususani msamaha usiotoka kwa mtenda dhambi mwenyewe.
Utawala wa SABAYA katika wilaya ya Hai haukuwa wa kisiasa tu; ulikuwa ni utawala wa chuma na ukatili uliopitiliza. Hata Mzee MBOWE anafahamu hilo.
Makosa ya uhujumu uchumi na unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery) yaliyomfunga gerezani wakati ule, ni tone dogo sana katika bahari ya unyama wake.
Wapo watu walitekwa, kuteswa, na kuachwa na vilema vya kudumu. Kusema mtu huyu anastahili msamaha bila toba ya dhati kwa wahanga, si tu ni kosa, ni dhihaka.
Miongoni mwa wahanga wa genge la SABAYA ni ndugu yetu Simon MNYAMPANDA, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai. Ndugu yetu aliteswa.
Simon Mnyampanda aliteswa kwa umeme. Ameeleza wazi kwamba, alihojiwa kuhusu mahusiano yake na Mzee MBOWE. Mwisho, alipigwa misumari ya miguu.
Huyu ni mtu aliyepata mateso hayo akimlinda Mzee MBOWE na CHADEMA. Leo Mzee MBOWE anajigeuza kadinali na kumuombea msamaha mtesaji SABAYA?
Genge hilo halikuishia hapo. Genge hilo lilikuwa kama MAHARAMIA. Walivamia nyumbani kwa mgombea udiwani wa kata ya Narumu katika jimbo la Hai.
Baada ya kumkosa, walitoa adhabu ya kinyama kwa watu waliokuwepo nyumbami kwa kuwakata masikio na sehemu nyingine. Nyumba nzima ilitapakaa damu.
Hawa ni binadamu, si takwimu za kisiasa. Hawa watu waliotendewa mambo hayo wapo. Baadhi ya ushahidi wa masuala hayo nimeambatanisha katika makala hii.
Inasikitisha kuona Mzee Mbowe anatumia mateso ya wafuasi wake kama mtaji wa kisiasa (political capital). Binafsi nimejiuliza maswali mengi tangu hiyo jana.
Je, wahanga wameombwa msamaha na kufidiwa? Je, mateso yao yamekuwa ngazi ya makubaliano ya kisiasa? Hii si dharau kwa wale walioteswa wakikupigania?
Sabaya anapaswa kuomba msamaha kwa waathirika, si kuombewa. Vinginevyo, hii ni michezo ya kumtengenezea mazingira ya kupata uteuzi katika Serikali ya CCM.
Watu wa Hai hawajasahau. Damu na machozi ya wahanga bado vinadai haki. Msamaha bila toba ni baraka kwa ukatili mwingine ujao. Haki kwanza, msamaha baadaye.
Binafsi, nilimheshimu Mzee Mbowe kiasi cha kumpa mwanangu wa tatu jina la “Freeman”. Leo hii, nahisi usaliti mkubwa moyoni mwangu kwa mambo hayo.
Kunyamaza mbele ya usaliti huu si busara, bali ni upumbavu ambao kesho utatunyong’onyesha. Nimeandika ili kulinda hadhi ya jina la mwanangu.
Siku mtoto wangu akiniuliza, nitamjibu kwa utimamu kabisa. “Nilitetea maana halisi ya ‘Freeman’ wakati jina hilo lilipotaka kuchafuliwa na siasa za kimaslahi.”
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imefuta (imeondoa) zuio (injunction) lililotolewa na Mahakama Kuu (Masjala ya Dar es Salaam) Juni 10, 2025 na Jaji Hamidu Mwanga (ambaye ndiye aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo).
Zuio lilikuwa linazuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya shughuli zozote za kisiasa, kutumia mali zake, kushiriki katika shughuli za chama hadi kesi ya msingi isikilizwe na kumalizika.
Kesi (Civil Case No. 8323 ya 2025) ilifunguliwa na Said Issa Mohamed (Makamu Mwenyekiti wa Freeman Mbowe) pamoja na wenzake wawili (waliohusishwa na mgawanyo wa mali za chama kati ya Bara na Zanzibar).
Walidai kuna mzozo wa ndani kuhusu mali na uongozi wa CHADEMA. Jaji Mwanga alitoa amri ya muda (interim injunction) ikizuia chama kufanya shughuli zozote za kisiasa na kufungia mali zake ili kesi yao isikilizwe.
Amri hiyo ilikuwa ilikuwa ya muda wa siku 14 mwanzoni, lakini iliendelea kuwepo kwa miezi mingi (hadi karibu mwaka mmoja). Hadi kufikia leo April 15, 2026 ni jumla ya siku 310 tangu kuwekwa zuio hilo haramu kabisa.
CHADEMA ililalamika kwamba: Zuio lilikuwa kali sana na liliathiri haki yao ya kufanya siasa. Jaji Mwanga alikiuka taratibu za haki ya kusikilizwa (right to fair hearing). Zuio lilikuwa limezidi muda unaoruhusiwa kisheria.
Mahakama ya Rufaa iliyoketi Dodoma ilianza kusikiliza maombi ya marejeo (revision) Machi 24, 2026. Leo (Aprili 15, 2026) jopo la majaji limetoa maamuzi yake na kufuta zuio hilo lililowekwa na Jaji Hamidu Mwanga.
CHADEMA sasa iko huru kuendelea na shughuli zake zo za kisiasa, mikutano, kampeni na matumizi ya mali yake bila kizuizi hicho. Hivyo shughuli ya kushughulika na Serikali katili ya CCM inaanza pale ilipoishia.
Kesi ya msingi (mgawanyo wa mali) itarudi Mahakama Kuu ya Tanzania, lakini kwa jaji mwingine (sio Jaji Hamidu Mwanga tena) kuamua suala moja tu la msingi, kama kesi hiyo ililetwa ndani ya muda au vinginevyo..
Hakuna zuio la kufanya shughuli za kisiasa kwa CHADEMA. Chama chetu kiko huru kutoka katika minyororo ya ukatili wa Serikali katili ya CCM. CHAMA kitatoa taarifa rasmi kwa umma na kueleza vizuri.
NB; Siku 310 za CHADEMA gerezani, ‘vyama mpango wa kando’ wa CCM hawajafanya hata kongamano la jando na unyago. Tumerudi, tupatane kwa ground tuwaoneshe kazi inavyofanywa. PEOPLE’S POWER.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limewaonya baadhi ya Watu wanaosambaza taarifa za uongo mitandaoni kuhusu madai ya Wachimbaji wadogo zaidi ya 200 kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa Msasa, uliopo Kata ya Runzewe Magharibi, Wilaya ya Bukombe Mkoani humo.