Huwezi kumkemea mtu mzima mwenzio —hata kama unamzidi cheo na madaraka—na utegemee akuheshimu. Kuzungumza na watu wazima na unajifanya huujui ukweli ni kujidhalilisha.
Usimdharau mtu yeyote, hata kama kwa macho yako unaona hana msaada wowote kwako. Kwa MUNGU hakuna mtu asiye na thamani ndiyo maana humuinua yeyote kwa wakati wake sahihi
Rafiki anayekusaliti na kugeuka adui hakuwa rafiki tangu mwanzo.
Rafiki anaweza kusitisha urafiki, akaendelea na maisha yake, na kamwe hageuki mbaya wako.
1)
Mjadala wa nafasi ya #AkiliMnembe katika elimu, kwa sasa una sura mbili kubwa. Kwanza, tishio la kweli kweli kwa mamlaka (ukuu) wa mwalimu katika ujifunzaji hasa kwa elimu ya juu.
Kwa kasi hii ya ukuaji wa teknolojia, kwa mfano, hatujui ujifunzaji utakuwaje kesho. Je, mwalimu atabaki na kazi ipi na kipi mwanafunzi anaweza kukifanya mwenyewe bila msaada wa mwalimu.
Katika mazingira ambayo mwalimu anajichukulia kuwa mmiliki wa taarifa na maarifa asiyehojiwa na mwanafunzi, #AkiliMnembe inahatarisha umuhimu wetu sisi walimu.
#ElimikaWikiendi
Unapompigia mtu simu na hapokei, chukulia ana sababu (zake) za msingi. Hata kama una dharura, kumpigia mtu mara ishirini ni uvamizi wa faragha yake.
Huwezi kujua unayemhitaji yuko wapi, anafanya nini na kipi hawezi kukizungumza kwa wakati huo. Heshimu haki yake ya kuamua kwa kuomba miadi ya mawasiliano. Usipopewa fursa hiyo heshimu haki ya mtu kutokuwasiliana na wewe.
Kumtumia (kumsomea) mtu mwingine ujumbe uliotumiwa wewe bila ruhusa yake ni kumkosea heshima. Mwandani wako si mwandani wa aliyekutumia ujumbe huo.
Kumweka mtu ‘loudspeaker’ asikike na asiojua wanamsikiliza ni kukosa nidhamu ya faragha ya mtu. Inaweza isiwe siri, na wala isiwe na madhara, lakini ikaonesha usivyoheshimu utu wa watu wanaokuamini.
UNATAFUTA mwenzi wa maisha?
Shughulikia mapungufu uliyonayo uwe bora zaidi bila kulazimika kuwa bandia. Bandia haidumu. Bandia ni utumwa. Bandia huvutia bandia. Bandia huanzisha mahusiano shikizi. Bandia huleta majuto.