‼️EXCLUSIVE‼️
Wale ambao hamkuweza kufika Mahakamani November 6, 2026 na mlitamani kumsikia Mhe. Lissu wakati anawashona Majaji kabla hawajasoma “Hukumu waliyopewa”.
Nimewaletea full clip ya Dakika 56 za Mhe. Lissu aisee ni noma na nusu.🙌
#FreeTunduLissu
Tundu Lissu amepewa namba ya mfungwa ambayo ni 623.
Ukisoma Luka 6:23 inasema “Furahini siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.”
Kila kitu kinachotokea kwenye maisha ya Tundu Lissu ni kusudi la MUNGU tusihuzunike sana.
USHINDI UNAKUJA NA HAUPO MBALI.
GOOD MORNING.
REPOST 200
#FreeTunduLissu
‼️HABARI MBAYA KUTOKA TUNDUMA‼️
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Songwe Isakwisa Tobias Lupembe amekamatwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Momba.
Leo asubuhi, alipigiwa simu na OCD wa Momba akiwa njiani kwenda Hospital kwa ajili ya matibabu ambapo OCD alimjulisha kwamba anahitajika kituoni kwa ajili ya mazungumzo ila alipofika kituoni aliambiwa yupo chini ya ulinzi kisha akawekwa lock up.
Mpaka sasa Polisi hawataki kusema kosa lake ni nini?
#FreeIsakwisaLupembe
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amesema endapo atapata nafasi atamtembelea Tundu Lissu, akieleza kuwa wana uhusiano wa karibu na kwamba Lissu ni mmoja wa watu waliomshawishi kusomea taaluma ya Sheria.
Akizungumza na Clouds TV leo Jumamosi, Nape amesema anatambua kuwa katika maisha kuteleza kunawezekana, huku akieleza kuwa alitamani matokeo ya hukumu ya Lissu yawe tofauti na yalivyokuwa, lakini kutokana na kuheshimu mifumo, ni muhimu kukubali matokeo yake.
Amesema magereza si sehemu nzuri ya kwenda kumtembelea mtu, huku akimpa pole Lissu na kueleza kuwa anapaswa kutumia muda wake akiwa peke yake kutafakari mwenendo wa maisha yake na kumkimbilia Mungu ili apate mwongozo.
Kuhusu hatua yake binafsi baada ya kutenguliwa katika nafasi ya Waziri, Nape amesema alijiondoa kwenye mitandao yote ya kijamii ili kupata muda mwingi zaidi wa kuzungumza na Mungu. Kauli hiyo ameitoa akieleza namna alivyokabiliana na kipindi hicho cha mabadiliko katika maisha yake ya kisiasa.
Jana, Novemba 6, 2026, Mahakama Kuu ilimuachia huru Lissu dhidi ya shtaka la uhaini, lakini ikamkuta na hatia ya uchochezi na kumhukumu kifungo cha miaka minne jela.
Muda mchache kabla ya Yesu kuhukumiwa kuuawa bila hatia, Jaji Mkuu wa Yudea (Pilato) aliwaita viongozi wakuu wa serikali (wakuu wa makuhani, na viongozi wengine wakubwa). Ingekua leo tungesema aliwaita Waziri mkuu, DPP, IGP, Mwanasheria mkuu wa serikali etc. Kisha akawaambia;
"Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimechunguza mambo yake mbele yenu, wala sikuona kwake kosa lo lote katika mambo hayo mliyomshitaki" (Luka 23:14).
Wale wakuu wa serikali wakapaza sauti wakisema "Asulubiwe" naye Pilato akatwaa maji, akanawa mikono yake, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe (Ikiwa mtamhukumu) basi damu yake na iwe juu yenu na watoto wenu (Mathayo 27:24-25).!
All the bst my Chairman. Haijalishi hukumu gani itatoka leo, lakini wewe Sio Mhaini. Dunia inajua na mbingu zinajua
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#TANZANIA: NANI KAMUELEWA MWABUKUSI KWENYE ANDIKO LAKE HILI?
Anaandika Rais wa Chma cha Mawakili Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi kwenye kurasa zake za kijamii.
"Nasikia kuna jitihada za kulazimisha Jogoo atage mayai na Kuatamia huko Malawi. Watu wote wenye akili timamu wanasubiri kuona namna sarakasi za hovyo na aibu zinavyopigwa mbele za wakwe na Taulo kiunoni.Hala hala kidole na jicho. Ukweli,Haki na Uwajibikaji vitaliponya Taifa" - Boniface Mwabukusi, Rais wa TLS