Msikilize vizuri BONGO ZOZO na haya ndio maswali ambayo tulitaka majibu yake.
Sasa walichofanya wakina KYANDE ni kuongeza maswali mengine magumu yanayoumiza mioyo yetu afu wanataka "Mardhiano".
KYANDE alichofanya ni kumsafisha DIKTETA jike kimataifa mikopo iendelee kuingia ila deep down wao ndio waliuwa na hatuna cha kuwafanya.
Inaumiza sana na hili wakoloni weusi wakae wakijua HAIWEZEKANI nchi ikarudi kama zamani bila kutibu majeraha tuliyonayo hilo HALIWEZEKANI.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Baba zao walikuwa wabunge, kisha wakawa Mawaziri na mwisho wakawa MARAISI sasa watoto na wao wanafuata nyayo za BABA ZAO.
Mimi na wewe watoto wetu watarithi uwinga, udalali, kuhangaika mpaka kufa kwao. Na watoto wetu watakuja kuongozwa na hawa watoto ambao baba zao walituongoza. Na itakuwa hivyo mpaka kwa vizazi vya ujukuu wetu na vilembwe.
Tunatengenezewa Taifa ambalo tunaaminishwa Familia fulani ndio zinaakili sana za kutuongoza na sisi wengine kuishi kama watumwa wao. Tulipopinga huu uchaguzi ni pamoja na haya mambo. Hii nchi sio ya KIFALME, tayari ilitoka huko miaka mingi sana na tukapata UHURU ambao unanyang’anywa kinguvu na kikundi fulani ambacho kimejimilikisha nchi.
Leo hii KAMA taifa tuna bunge la KIFAMILIA, humo ndani usitegemee lolote la maana kujadiliwa ya kukuhusu wewe mwananchi. Humo ufisadi wa kutisha utapitishwa kwa mgongo wa “Bunge la wananchi” na hakuna kitu mtafanya kama wenye nchi.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Raia wanakufa,wanapotea,wanatekwa na jeshi la polisi wanatuhumiwa wanakana na kusema wanafanya uchunguzi na hawaleti majibu inapita siku Hadi miaka. Najiuliza kama kazi ya kulinda raia na mali zake ni ya polisi na hawaitekelezi ipasavyo maana yake si imewashinda? Mbona aliyewapa hii kazi hatuoni akiwakemea au kutoa adhabu like kushushwa cheo au kujiuzulu? Ni kina nani wanafanya haya matukio na jeshi la polisi lipo? Na linasifiwa na waliowapa vyeo kwamba linafanya vizuri? Je hayo ndio mazuri kwao?
Naomba anayejua anielezee hii serikali inaenda kufanya Nini kikubwa(sera Yao kuu ni Nini) achana na mambo ya kuleta,kuboresha,kujenga..Mfano Lowasa alikuwa na Elimu,Magu alikuwa na Viwanda na uchumi wa kujitegemea