Mnakumbuka mnavyo tutesa, ndivyo mtakavyo teseka, mnaona mlivyo tudharau , ndivyo mtakavyo dharauliana, mnakumbuka mnavyo tuweka jela kwa ushahidi na kesi za uongo , ndivyo mtakavyo pelekana magereza, mnajua tunavyoishi kwa hofu ? sasa ni zamu yenu.
Mnakumbuka mlivyoteka na kuua watu , sasa ile mbegu imeota kwenu. Hali yenu itakuwa mbaya sana, kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti. Bahati mbaya Nchi pia inaharibika.
@NJENJE_255 Hapana haujasahau bro, ni vile huyo jamaa mwenye sufuria kichwani anachelewesha kuwamwagia hayo maji hao wawili upande wa chini molali iwe juu 😅😅
UDALALI WA KISIASA NA MACHOZI YA MAMBA
Katika medani ya siasa za Tanzania, ni rahisi sana kuwatambua wanasiasa wanaosimama upande wa umma nyakati zote, na MADALALI wanaosubiri upepo uvume ili wajivike koti la ushujaa.
Kauli za hivi karibuni za Zitto Kabwe kuonyesha kuguswa na kusikitishwa na kusota gerezani kwa Tundu A.M. Lissu, pamoja na ukandamizaji wa uchaguzi uliofanywa na CCM, zinaibua hisia nyingi.
Kabla ya kuingia katika uchaguzi uliosababisha maafa, CHADEMA ilisimama ikitaka vyama vya upinzani viungane kudai: Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi na marekebisho ya sheria za uchaguzi.
Hata hivyo, Zitto Kabwe na chama chake walikataa ushirikiano huo. Walichagua kushiriki uchaguzi huo licha ya kuwepo kwa viashiria vingi vya udhalimu. Hawakujali kabisa hisia za watu wengi. Ubinafsi.
Walisaini kanuni za maadili ya uchaguzi, wakatoa dhihaka kwa waliokuwa wakisisitiza msimamo wa “NO REFORMS, NO ELECTION”, na wao wakaamua kusema “TUTAPAMBANA, TUKISHIRIKI”.
Zitto Kabwe alifika hatua ya kusema hao wanaosusia uchaguzi hawajielewi na hawajitambui huku akidai kuwa chama pekee chenye uwezo wa kuitisha maandamano makubwa ni ACT-Wazalendo.
Wakaibuka na kauli mbiu za kitapeli “OKTOBA LINDA KURA”, wakati hawakuwa na mkakati wowote wa kulinda kura zaidi ya kutumika kuhalalisha ushindi wa kishindo wa 98% kwa wapiga kura hewa.
Baada ya mfumo huo huo waliouhalalisha kuonyesha sura yake halisi, leo anasimama kuzungumzia dhuluma za uchaguzi kana kwamba hakuwa sehemu ya waliochangia kuupa uhalali mchakato huo.
Kwa mtazamo wangu, ACT-Wazalendo na Zitto Kabwe walishiriki kuisafisha CCM mbele ya macho ya umma na kuhalalisha ushindi wao. Huu ni usaliti mkubwa kwa harakati za ukombozi wa kisiasa.
Zitto Kabwe ambaye amefanyiwa ‘endorsement’ na mgombea URAIS wa CCM jimboni, na hakuwahi kulitaja jina la mgombea wa CCM, anaibua mashaka makubwa kuhusu dhamira yake wakati huu.
Zaidi ya hayo, tangu Tundu A.M. Lissu akamatwe, kuwekwa rumande, kufunguliwa mashtaka ya uongo ya uhaini na kupelekwa gerezani, Zitto Kabwe hajawahi kuonekana gerezani au mahakamani.
Usiku unakula na watawala, mchana unawatetea wahanga wa mfumo huo. Huwezi kuwa mshirika wa mfumo unaokandamiza haki za wapinzani halafu ukataka kutambulika kama mtetezi wao.
Ndio maana Zitto Kabwe akiongea anaonekana mnafiki, na akinyamaza anaonekana msaliti; Ni matokeo ya kuchagua kuishi katikati ya mstari (playing both sides). Hatakiwi kuaminika.
Kwa nini sasa? Je, ni baada ya kuona mashinikizo mazito kutoka kwa jumuiya za kimataifa, hususani Jumuiya ya Ulaya na Marekani, yakiongezeka dhidi ya ukandamizaji mkubwa wa kisiasa nchini?
Zitto Kabwe ameanza kujionyesha kama mtetezi wa haki mwishoni kabisa. Lakini anapozungumzia matatizo yaliyopo, anaelekeza lawama kwa viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama pekee yake.
Huku akijaribu kuwatenga watawala wa kisiasa ambao kikatiba na kiutendaji wanawajibika moja kwa moja kwa maamuzi makubwa ya nchi. Hili linazua maswali kuhusu dhamira halisi ya kauli zake.
Ni mkakati wa kupunguza makali ya mapambano yanayofanywa na wapigania haki hslisi, kuwatenga watawala wa CCM ambao ndiyo waliotoa amri haramu, na kuharibu uchaguzi hadi mauaji
Hu ni mkakati unaotengenezwa kutusogeza katika meza ya MARIDHIANO kwa kuwatoa kafara wachache katika vyombo vya ulinzi na usalama huku watawala wa kisiasa wakibaki bila kuwajibika.
Katika siasa za mapambano, katika nchi demokrasia bado inapiganishwa kwenye matone ya jasho na damu, hakuna eneo la kijivu (gray area); ama uko upande wa haki au uko upande wa dhalimu.
Watanzania wanaona, wanasikia na wanakumbuka. Ni muhimu kutambua waliosimama katika misingi ya mapambano tangu mwanzo na hawa MADALALI wanaojitokeza baada ya upepo kubadilika.
Waliokuwa mstari wa mbele kubeba gharama za harakati hawapaswi kuruhusu historia yao kutwaliwa na MADALALI wanaotaka kujijengea taswira ya kishujaa bila kubeba gharama za mapambano.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila