katibu Chadema Jimbo la Mafinga Mjini
(politician) Human rights activist/Mfungwa wa kisiasa wa kesi No:206/2019 (Sumbawanga). survival to tell the tale
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 5
Mhe. Lissu anamuuliza Katuganga nani anaevunja amri ya mahakama kati ya Wakili Mkuu wa Serikali na team yake yote ambao wamewaweka wazi wote.
Kile walichoambiwa na Mahakama Kuu wasikifanye ndo wamekifanya, mwenye kosa ni nani hapo mimi au wao?
Walishawaweka hadharani wao.
Nisingejua makazi yao, makabila yao na mitaa yao. Wameleta wenyewe.
Halafu hapa wanasema wakitajwa hawatafika.π€£π€£π€£π€£
Majaji wanateta kidogo hapa.
Ngoja tusubiri.
Kumenuka.
Kazi ishakuwa ngumu hapa.π
Majaji wanateta.
Kimeumana.
Jaji: anawasha kipaza sauti kinapiga kelele hakiwaki. Vurugu tupu mahakamani.
Anasema tumewasikia.
Mahakama inasema tayari kuna amri ya mahakama hii hii hiyo amri inaendelea kuwa valid kama ambavyo ilivyo.
Kwahiyo tuiheshimu tu hiyo amri maana haijatenguliwa.
Anatuomba pia tuwe watulivu hapa mahakamani.
Mhe. Lissu : Anasema sasa niendelee. Sitawasoma hao watu.
Nawaomba muangalie kwenye rekodi maelezo ya shahidi P2,3,4,5,6,7,8,9,1 na 11.
Maelezo yao yanafuatana na maelezo yote hayo yanakiuka amri ya Jaji Mtembwa kuna mahali wametoa namba za simu, mitaa kazi, familia, hadi idadi ya wake na watoto wamesema.
Amri ilisema wafiche mambo hayo.
Anasimama tena KATUGA anasema pingamizi linahusu mahakama hii haina mamlaka kusikiliza shauri hili.
Anachotuletea hapa ni kama anatoka kwenye point ya kisheria.
Naona mwenzetu anachallenge namna information inavyokuwa challenged.
Tunaweza mkamatia mbali sana tukimuacha hivi au tusimkamate kabisa.
Mahakama π€£π€£π€£
Katuga anasema tunaweza chukua siku saba au sita.
Anamkaribisha Wakili Job wa serikali anasema upande wetu turejee kwenye shauri la Mahakama ya rufaa Civil Application No 656/2021 ilisema
Pingamizi linapaswa kuwa la kisheria huyu mtu (Lissu) mkimuacha ataenda mbali sana.
Angalieni namna ya kumdhibiti, atatuacha nawaambieni waheshimiwa majaji.
Mhe Lissu : Hoja ya pingamizi lao haina msingi wowote kisheria.
Kama niliyosema jana mahakama hii haina mamlaka juu ya shauri hili on the face of records kuna irregularities.
Kwahiyo kusema kwamba hizo zinaonekana kwenye rekodi ya mahakama zisisemwe hiyo hoja haina maana yoyote.
Pia hiyo kesi waliyoitaja wangejua kesi maarufu ni Mukisa Biscuits anataja citation yote kutoka kichwani anasema hiyo kesi inasema PO ni nini?
Sasa wao wanacite kesi gani sijui hapa. Haya mambo yapo kwenye Mukisa.
Jamaa hii kichwa yake sijui ikoje. π€£π€£
Ningekuwa naingiza mambo mapya lakini nazungumzia kuhusu makaratasi ambayo nimepewa jana hapa mahakamani wanayakataaje sasa?
Dr. Nshalla ameenda kuongea na Lissu kidogo wamemaliza.
Na majaji nao wanateta.
Mahakama iko kimya majaji wanateta kuna POLISI moja hapa simu yake imepiga wimbo wa BONGE LA DADA ameona sana aibu. π€£π€£π€£
Lissu anasema sasa nimetaja sheria kuhusu namna committal proceedings inavyopaswa kufanya. Hizi rules ni zao wamezitengeneza juzi hapa wao wenyewe sio mimi.
Tusipozungumzia makosa yao ambayo hawataki nizungumzie wanataka tuzungumzie makosa ya nani? Either nazungumzia nini kama hoja yao iko sahihi maana yake yote yafutwe. Ninachosema ni kwamba toka jana nilikuwa nazungumzia nini? Basi kama ni hivyo futeni hadi niliyosema jana.
Jaji anamuuliza KATUGA kama ana rejoinder.
Katuga anasema anachokufanya yeye ni kwamba yuko aggrieved na maamuzi ya mahakama kwahiyo naomba tena Mahakama jamani Mheshimiwa imuelekeze. Tumeona hadi yamejadiliwa hadi maamuzi ya mahakama kuu. Muelekezeni kuendana na kilichopo tu tafadhali.
Naomba Wakili Mrema aongezee, anasimama na kusema tunatofautiana nae kwasababu baadhi ya mashahidi aliowasema kwamba wangekuwa ni mashahidi wake kwenye proceedings hawapo na amesema kanuni ametungiwa yeye lakini hazipo kwneye proceedings.
Huyu mtu asipodhibitiwa anaingiza mambo mengi hapa. Yanatuvuruga sisi. Hayapo kwenye makaratasi. Anachomeka sana vitu. Anasema jambo moja ukizubaa anachomeka mengine tisa. Adhibitiwe.
Part 6 itaendelea post inayofuata,
Naomba Repost yako.
@tanpol Kanuni ya wapi hii mtuhumiwa akajichunguza mwenyewe acheni kutchezea akili, Mdude kafunguliwa mashitaka ya kubumba na polisi mara kadhaa amepigwa na kuteswa na polisi mara kadha leo hii jeshi la polisi mnakwepea wapi kwenye hili ata mtu asie na knowledge ya kiuchunguzi anaelewa
Only 1K Repost Itβs enough to tell the world that Tanzania is not safe. Police brutality is increasing day by day because of the election, and the president @SuluhuSamia remains silent.
Polisi wanateka, wanavunja wa tz miguu na mikono , wanaua na kudhalilisha wa tanganyika kwa kuwapiga na kuwatupa maporin ilikutetea ccm na serikali yao ,Niwakati wakuitetea tanganyika na watanganyika kwa style hiyo hiyo babu zetu walifanikiwa kwa wakoloni weus hi nizamu yetu
Ni wakati wa kuibua hasira na hisia kali dhidi ya matendo haya watanzania sio wakimbizi na hata wangekuwa wakimbizi hawastahili kutendewa haya na serikali yao tunapaswa tuchukie na kuonesha hasira dhidi ya unyama huu wakati wakumwachia Mungu umekwisha huu ni wakati wa kudhibiti
@ChiefLumanyika ili uhalali wakuzuia uchaguzi upatikane nilazima upumbavu huu unaofanywa na polisi ufanyike ilikuta uhalali wakuzuia tena kwa hasira zinazotokana na huu upumbavu
Viongozi wa DINI ni RAIA wa Tanzania, kama walivyo wengine, na chini ya ibara ya 3(1) ya KATIBA ya Tanzania, wanayo HAKI ya KUSHIRIKI SIASA. Jitihada zozote za KUWAZUIA Viongozi hao KUSHIRIKI SIASA, ni kuthibitisha UTAPIAMLO WA AKILI. Jibuni HOJA zao, acheni UPUMBAVU.
Kama kuna mtu kawadanganya ACT kuwa Chadema imesusia uchaguzi amekosea sana. Chadema haijasusia uchaguzi, Chadema inapigania Reforms ili ishiriki uchaguzi wa HAKI na KWELI. Na maaskofu wamesema muda unatosha wa kuzipata Reforms.