Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kinapatikana Moshi, mkoani Kilimanjaro, Tanzania. Chuo hiki kimejikita katika elimu ya ushirika, biashara, na masuala ya ujasiriamali. Kinatoa programu mbalimbali za shahada za awali, za uzamili, na hata za uzamivu katika nyanja hizo.
UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA FEDHA ZA KUJIKIMU KWA ROBO YA NNE
Ijumaa, Mei 17, 2024
Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na umma kuwa tunakamilisha malipo ya fedha za kujikimu (Chakula na Malazi) kwa robo ya nne (Quarter IV) na wanafunzi watarajie kupokea fedha hizo kuanzia Jumatatu, Mei 20, 2024.
Ufafanuzi huu unafuatia maoni na maswali yanayoulizwa na wanafunzi wanufaika kupitia barua pepe, mitandao ya kijamii kuhusu hatua ya malipo iliyofikiwa hususan kwa vyuo ambavyotarehe za malipo (due dates) ya robo ya nne zimefika.
Aidha, tunapenda kuwasihi wanafunzi kuendelea kuwa watulivu na kuwasiliana na Maafisa Mikopo waliopo katika vyuo vyote nchini pale watakapokuwa na maoni au kuhitaji ufafanuzi.
Katika mwaka wa masomo 2023/2024, Serikali imetenga TZS 786 bilioni kwa ajili ya mikopo na ruzuku kwa wanafunzi zaidi ya 220,000 wanaosoma shahada na stashahada mbalimbali katika taasisi za elimu nchini.
Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya HESLB (https://t.co/31vAUVVNH7) na mitandao ya kijamii ILIYOTHIBITISHWA ya X (zamani Twitter), Facebook na Instagram kwa jina la HESLB Tanzania.
Imetolewa na:
Dkt. Bill Kiwia
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Jengo la PSSSF, Barabara ya Makole,
S.L.P. 984,
DODOMA
Ijumaa, Mei 17, 2024
#WeweNdoFuture
#TimizaWajibu
📢CALL FOR PAPERS!!
Submissions for papers for the Midterm Review of the 13th Africa Ministerial Cooperative Conference are now open.
🗓️Submission deadline: 4th March 2024
More information ➡️ https://t.co/cdGLR99Tvq
Timu ya wanafunzi wa Chuo wanaoshiriki michezo mbalimbali katika mashindano ya Vyuo Vikuu (TUSA) mwaka 2023.
Michuano hiyo imeanza tarehe 13 na itahitimishwa 21 Desemba
MoCU, Timu ya Ushindi.......💪💪
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Mhe. Anne Makinda amekuwa mgeni rasmi katika majilisi (Convocation) ya tisa yaliyohusisha wanafunzi, wahitimu waliosoma Chuo cha Ushirika, MUCCoBS na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, watumishi waliowahi kufanya kazi na wanaofanya kazi chuoni
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Mhe. Anne Makinda amekuwa mgeni rasmi katika majilisi (Convocation) ya tisa yaliyohusisha wanafunzi, wahitimu waliosoma Chuo cha Ushirika, MUCCoBS na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, watumishi waliowahi kufanya kazi na wanaofanya kazi chuoni
Timu ya wanafunzi wa Chuo wanaoshiriki michezo mbalimbali katika mashindano ya Vyuo Vikuu (TUSA) mwaka 2023.
Michuano hiyo imeanza tarehe 13 na itahitimishwa 21 Desemba
MoCU, Timu ya Ushindi.......💪💪
#PoleniHanang
Tunatoa salamu za pole kufuatia maafa yaliyosababishwa na mafuriko na maporomoko yaliyotokea.
Tunawaombea marehemu pumziko la amani na ahueni kwa manusura.
#PoleniHanang
Wanafunzi 2,177 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 7.26 bilioni baada ya kuwasilisha maombi ya rufaa kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kwa kujaza taarifa na kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha uhitaji wao.
Tembelea SIPA kupara taarifa zaidi.
#WeweNdoFuture#TimizaWajibu
#Cooperatives play a crucial role in addressing the challenges faced by micro, small and medium-sized enterprises. With their networks and expertise, SACCOs can help MSMEs access the funding they need to grow and succeed.
Read more 👉 https://t.co/mneJOjLgzK
@Coopnewsmedia
We were happy to host our members from Moshi Cooperative University led by the Vice Chancellor, Prof. Alfred Sife.
Thank you @MoshiUniversity for your continued support and collaboration.🙏
#teamworkmakesthedreamwork