Wiki mbili mpaka tatu zijazo vyuo vikuu vitafungwa. Wanafunzi wa Chuo watarudi makwao!
So far kutakuwa na Makundi makubwa mawili, kundi la kwanza ni la wale waliomaliza Chuo mwaka huu na kundi la pili ni lile la wanafunzi wanaoenda likizo ndefu kutokana na kumaliza mwaka.
Sasa, kwa wale ambao ndo wamemaliza kabisa tunawakaribisha mtaani na nataka kuwaambia kuwa Chuo ilikuwa ni sehemu ya kukupa expossure na kukufungulia dunia. Chuo haikuwa sehemu ya kukuandaa kuwa Tajiri. Mtaani mambo ni tofauti, kulala Njaa na kuchanganyikiwa ni kitu cha kawaida. Huku watu wana stress za Kodi, Chakula, Pesa ya Taka, pesa ya Umeme, Pesa ya Nauli, Pesa ya Matibabu, Pesa ya bando, Pesa ya Maji na Hekaheka zingine zinazohitaji pesa kutatua.
Hakuna wa kukupa Boom wala wa kukuajiri. Tangu nimeondoka Chuo cycle yangu naiona bado iko kitaa, imestrugle kutafuta kazi na ina GPA nzuri kuliko yako lakini ni mtu 1/10 walioajiriwa mahali. Ajira ni ngumu na washkaji mtaani wanapeana madili kwa kujuana, hatakaama ni dili la saidia Fundi.
Kuna vitu vingi sana mmedanganyana, umedanganywa au umejidanganya wewe na nafsi yako kuwa mambo yatakuwa mazuri baada ya kumaliza. Huku ulimwengu ni wa tofauti sana. UTASHANGAZWA!!
Sasa wewe ambae ndio umemaliza chuo, jipe miezi 10-1year chagua ujuzi JIFUNZE. Master skills then jiajiri, tafuta elfu tano tano za kuendesha Maisha mpaka ndoto zitimie.
Na nyie ambao mmeenda Likizo, muda utawalea kwa namna mnavyo utizama. Jiandaeni kui-face zaidi Kesho. Usikae Lazzy, kwenda kutembelea ndugu au kujikusanya na washkaji kuingia viwanja. Iandaeni kesho yenu baada ya kurudi mtaani. Huku mambo ni tough!!
2027 imebaki miezi 6 tu.
2016 ilikuwa miaka 10 iliyopita.
COVID ilianza zaidi ya miaka 6 iliyopita.
Waliozaliwa 1990 wamebakiza miaka 14 tu kutimiza miaka 50.
Na leo, 2007 iko mbali zaidi kuliko 2040.
Muda unakimbia.
Acha kusubiri. Anza sasa.
Nimemaliza VIKINGS season zote 6. Rating yangu ni 8/10.
Season bora ingeishia alipokufa RAGNAR-Seaon mbili za mwisho ni kama walikuwa wanafosi unyama iwe ndefu.
Kategart kubaki mikononi mwa demu mchawi pale ndio nimemaindi kinoma. Mwisho mbaya huu.
Kisa cha ROLLO pia hakijawa na mwisho mzuri au kwasababu aliokoka alimjua bwana?
Nimefurahi kumuona FLOKI mpaka mwisho (JITU LA MIZIMU).😂